Matege ama rickets ni hali ya mifupa kuwa laini na dhaifu, hali hii husababishwa na kuwepo kwa upungufu endelevu wa madini ya vitamini D kwa watoto.
Vitamini D huongeza ufyonzaji wa madini ya kalisium na phosphorua kutoka kwenye mfumo wa chakula-utumbo na kuingia kwenye damu. Upungufu wa vitamini D husababisha uwiano wa madini ya kalisium na phosphorus kuharibika na hivyo mifupa kuwa dhaifu na kupata tatizo la matege-rickets.
Kijikinga na upungufu wa vitamini D
Watoto wakubwa na vijana hupata kiasi cha kutosha cha vitamini D kutoka kwenye jua. Vichanga na watoto wadogo kabisa huweza kukosa kiasi cha vitamini D kinachohitajika kwa sababu hawakai kwenye mwanga wa jua
Kama ndo hivyo basi hakikisha mwanao anapata kiasi cha kutosha cha vyakula vyenye vitamini D kama mafuta ya samaki, kiini cha yai au vyakula vya kusindikwa kama
Maziwa ya kopo
Nafaka
Maziwa
Juisi ya machungwa
Kwa sababu maziwa ya binadamu huwa na kiwango kidogo cha vitamini D watoto wote wanaonyonya tu wanahitaji kupata vitamini D kiasi cha 400IU kwa njia ya mdomo kila siku.
|Soma zaidi kuhusu makala hii bonyeza hapa
Comments