Namna ya kujikinga na gono
Gono ni ugonjwa mojawapo ulio katika magonjwa ya zinaa, huambukizwa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye ugonjwa huo. Maambukizi ya gono kwenye koo na njia ya haja kubwa hutokea endapo mtu atagusana na vidonda au majimaji yenye maambukizi au kushiriki kujamiana kinyume na maumbile. Makala hii inazungumzia Zaidi kujikinga na ugonjwa huu wa gono
Gono mara nyingi huwa haiambatani na dalili yoyote ile kwa wanawake, ndio maana mara nyingi wanawake wenye ugonjwa huu huweza kuona kama vile wana UTI ndogo tu bila kufikiria kuwa wana ugonjwa huu wa gono.
Dalili zinazoweza kutokea kwa wanawake hata hivyo ni;
Kutokwa na uchafu wa njano ukeni
Maumivu wakati wa kukojoa
Kukojoa mara kwa mara
Kutokwa na damu ukeni katikati ya mwezi
Maumivu ya tumbo la chini
Kutokwa na damu njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile
Kutokwa na uchafu njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile
Maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile
Kwa wanaume
Dalili za mwanzo ni muwasho katika tundu la njia ya mkojo
Maumivu ya kuungua njia ya mkojo wakati wa kukojoa
Kutokwa na usaha kwenye njia ya mkojo
Kushindwa kabisa kupitisha mkojo
Kupitisha mkojo kwa shida ambapo itakua inazidi kadri siku zinavyoenda
Kuonekana kwa damu kwenye mkojo
Maumivu ya pumbu upande mmoja
Kuvimba kwa pumbu upande mmoja
Vipimo
Hakuna haja ya kufanyia kipimo endapo utakuwa na dalili zinazoelezea tatizo hili. Hata hivyo vipimo vinavyoweza kufanyika ili kutambua gono ni pamoja na
Kipimo cha culture ya majimaji ya maambukizi kutoka ukeni au kwenye uume
Kipimo cha gramu stain
Matibabu ya gono
Gono hutibiwa kwa matumizi ya dawa zinazoitwa antibayotiki, kwa mujibu wa miongozo ya matibabu kwa Tanzania, mgonjwa ataanza kutumia dawa za vidonge kwanza na endapo zikishindikana atatumia dawa ya kuchoma ikifuatiwa na vidonge. Mpenzi wako pia atatakiwa kutumia dawa hizi ili kuzuia kupata maambukizi tena kutoka kwake kwa mara nyingine, endapo una wapenzi wengi ni vema wote pia wakatibiwa.
Madhara
Endapo ugonjwa huu hautatibiwa unawez akuleta madhara sawa na magonjwa mengine ya zinaa ikiwa pamoja na;
Kwa wanawake
Kwa wanaume
Kuharibika kwa njia ya kupitisha mkojo na shahawa
Namna ya Kujikinga na gono
Ili uweze kujikinga na gono ni vema kuzingatia mambo yafuatayo
Kutokufanya ngono zembe
Epuka mahusiano ya mpenzi zaidi ya mmoja
Epuka kujamiana na mtu wmenye vidonda aina yoyote sehemu za siri
Endapo una shiriki sana ngono, hakikisha kila mwaka unapima maambukizi ya gono
Muulize mpenzi wako endapo ameshawahi kuugua gono, pata vipimo na matibabu kwa pamoja
Fahamu na fanya Matumizi sahihi ya kondomu
Unapopata dalili za Gono wahi ukapimwe ili ugonjwa ugunduliwe na kutibiwa mapema bila kuleta madhara.
Endapo umetambulika kuwa una gono, hakikisha wapenzi wako wote wanatibiwa kwa kuwa wasipotibiwa watakuambukiza tena
Penda kujisomea kuhusu magonjwa ya zinaa ili kupata elimu zaidi na Zaidi
Rejea za mada hii
ACOG. Chlamydia, gonorrhea and syphilis. https://www.acog.org/womens-health/faqs/chlamydia-gonorrhea-and-syphilis. Imechukuliwa 10.11.2020
ULY CLINIC. Gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono. Imechukuliwa 10.11.2020
MSD. Gonorrhea. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea?. Imechukuliwa 10.11.2020
ULY CLINIC. Ugumba. https://www.ulyclinic.com/ugumba. Imechukuliwa 10.11.2020
Comments