top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Uimara wa mwili kiafya | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020

Maswali ya kujiuliza kabla ya kusoma makala hii


  • Mwili wako upo imara kiasi gani?

  • Je ili kusema mwili wako ni imara unatakiwa kuwa na vitu gani?

  • Ufanye nini ili mwili wako uwe imara?

  • Ufanye nini ili kuendeleza uimara wa mwiliwako?




Utangulizi

Katika makala hii utajifunza na utaweza kujibu maswali hayo mbalimbali kuhusu uimara wa mwili na endapo utachukua hatua utafanya mwili wako uwe imara kutokana na elimu utayoipata hapa.

Inawezekana ukawa na uelewa zaidi au kidogo kuhusu uimara wa mwili na ukajielewa pia kuhusu mwili wako upo imara kiasi gani. Kwa kusoma makala hii utajua kiuhalisia mwili wako upo imara kiasi gani na kuweza kuweka mikakati halisi ya kufikia malengo yako.

Ili kupima uimara wa mwili wako unahitaji kuwa na vifaa vya aina tofauti ambavyo ni;

Saa ya mkononi, nzuri ukiwa na ya mshale au inayopima sekunde

  • Futi ya kupimia urefu

  • Mzani

  • Mtu mwingine pembeni yako

  • Gundi ya plaster imara

  • Peni au penseli

  • Kitabu cha kuandika kumbukumbu

Kwa kawaida uimara wa mwili hupimwa kwenye maeneo muhimu mbalimbali ambavyo makuu ni uimara dhidi ya mazoezi ya aerobic, uimara wa misuri na kuhimili ukinzani, uwezo wa kujikunja na kilichotengeneza mwili wako


Uimara wa ki aerobic- Mapigo ya moyo ukiwa umekaa

Kupima idadi ya mapigo ya mishipa ya damu

Kupima Idadi ya mapigo ya moyo ukiwa umekaa hulenga kupima afya ya moyo na uimara wake. Watu wakubwa mioyo yao hupiga/hudunda mara 60 hadi mia kwa dakika mojo (mapigo/dakika)

Mapigo ya moyo yanaweza kupimwa kwa kutumia mapigo ya mishipa ya damu haswa ile iliyo karibu au inayowasiliana na moyo moja kwa moja.mshipa mzuri na rahisi kufikika ni mshipa unaoitwa carotid artery unaoweza kuushika shingoni upande wa kushoto au kulia kwa koromeo la hewa, mshipa wa radial artery unaopatikana chini ya kidole gumba baada ya maungio ya kiganja cha mkono. Tafadhari angalia picha kuelewazaidi

Ili kupima mapigo ya mishipa ya damu Weka vilele vya vidole viwili shingoni au kwenye mkono ikihusisha kidole cha pili na tatu baada ya kidole gumba.

Tumia saa yako ya mkononi kuhesabu mapigo ya mishipa ya damu kwa muda wa sekunde15 kisha zidisha mara 4 au hesabu kwa muda wa sekunde 60 kama utaweza. Mfano umehesabu kwa sekunde 15 kisha ukapata mapigo 20, ukizidisha kwa 4 unapata 80 mapigo kwa dakika



Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC

Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.

39 views1 comment

Recent Posts

See All

1 Comment


Bernard
Bernard
Oct 01, 2021

Hello mate great blog.

Like
bottom of page