Kujamiana na mwanaume mwingine wakati wa ujauzito
Neno kuchekupa katika makala hii limetumika kumaanisha kujamiana na mtu mwingine mbali na uliyenaye sasa
Ni maswali mengi sana yameulizwa kupitia tovuti hii kuhusu kichwa cha mada hii kama yalivyoorodheshwahapa chini
Je Kuna madhara yeyote kwa mtoto aliye tumboni endapo baba atajamiana na mwanamke mwingine tofauti na aliyebeba ujauzito wake?
Naweza kujamiana na mwanaume mwingine kwenye ujauzito pasipo mtoto kupata madhara?
Madhra gani mtoto anaweza kupata endapo nitajamiana na mwanaume mwingine?
Kuna madhara ya kupata mimba ya pili kutoka kwa mwanaume mwingine?
Makala hiiimeandikwa makusudi ili kutoa majibu ya maswali hayo
Endapo una ujauzito na ukawa na haja ya kujamiana na mwanaume mwingine ni vema ukafikiria mara mbili kwanza. Kama umeachana na mpenzi wako mara baada ya kufahamu kuwa una ujauzito au mmegombana tu, si vema ukafikiria kujamiana mara moja tu isipokuwa endapo huna mpango naye tena. Hata hivyo unatakiwa kujipa muda kipindi hiki ili mwili ukabiliane na mabadiliko ya msongo wa mawazo na ang'zayati ambao huleta mabadiliko ya kihomoni ndani ya mwili wako. Mabadiliko ya kihisia na kiakili wakati huu wa kuachana husabanisha mabadiliko ya homoni ndani ya mwili ambayo huwa na uwezo mkubwa wa kudhuru ujauzito wako na mtoto aliye tumboni.
Ikiwa umekata shauri kuwa hamuwezi kurudiana na mwanaume aliyekupa mimba, unaweza kujamiana na mwanaume mwingine ikiwa tuendapo mwanaume huyo hana magonjwa ya zinaa. Tumia kondomu endapo hamjapima na usishiriki ngono kinyume na maumbile.
Magonjwa ya zinaa huwa na madhara kwa mama na mtoto kama vile kutoa mimba, kujifungua kabla ya umri, na mtoto kuzaliwa akiwa na upofu au njiti. Soma zaidi kuhusu madhara ya magonjwa ya zinaa kwenye ujauzito katika makala za ULY CLINIC
Pia unapaswa kufahamu kuwa mtoto tumboni huwa hachafuki na shahawa za mwanaume wala kupata majeraha kwa kujamiana na mwanaume mwingine, isipokuwa wakati wa kujifungua endapo kuna shahawa ukeni, mwanao anaweza kuchafuliwa nazo. Bila shaka utakuwa umejisafisha wakati huu wa uchungu katika maeneo yako ya siri
Je kuna madhara ya kupata mimba ya inayofuata kutoka kwa mwanaume mwingine?
Kisayansi inaonyesha kuwa kuna madhara yanaweza kutokea pale endapo mama aliyepata mimba ya kwanza kutoka kwa mwanaume A atapata mimba inayofuata kutoka kwa mwanaume B.
Mama huyu huwa na hatari ya kupata madhara yafuatayo kwake au mtoto wake;
Kujifungua kabla ya wakati
Kujifungua mtoto njiti
Kuongezeka hatari ya mtoto kufariki utotoni
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kujichukuliwa hatua yoyote ile ya kiafya.
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na tiba kwa kupiga simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.
Rejea za makala hii,
Babycentre. Can I have sex with a new partner now I’m pregnant?.https://www.babycentre.co.uk/x25009181/can-i-have-sex-with-a-new-partner-now-im-pregnant
NCBI. Effects on pregnancy outcome of changing partner between first two births: prospective population study.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC261811. Imechukuliwa 15.08.2020
ULY CLINIC. Kifafa cha mimba. https://www.ulyclinic.com/kifafa-cha-mimba-eclampsia. Imechukuliwa 15.08.2020
NHIS.Sex in pregnancy. https://www.nhs.uk/conditions/pregnancy-and-baby/sex-in-pregnancy/. Imechukuliwa 15.08.2020
Opmerkingen