top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Kujikinga na saratani ya koo | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Utangulizi

Saratani ya koo ina vihatarishi ambavyo vinamweka mtu kupata saratani hii, kwa kawaida endapo kuna vihararishi mtu anaweza kuepuka baadhi ya vihatarishi na kumwondoa katika hatari ya kupata saratani hii. Hapa chini kuna maelezo ya namna ya kuepuka kupata saratani ya koo


Acha kuvuta sigara na usianze kuvuta sigara kama huvuti

Unaweza kupata msaada wa daktari akufundishe namna ya kuacha kuvuta sigara


Jikinge na virusi vya HPV


Acha kufanya mapenzi kwa njia ya kunyonya uke au uume na kuwa na wapenzi wengi, hakikisha mmepima Virusi hivi na hamna mnapokuwa mnafanya mapenzi kwani kirusi huyu huweza kusababisha saratani zingine ikiwa pamoja na saratani ya shingo ya kizazi. Ukipima na mpenzi wako ni vema ili kujikinga na saratani hizi, epuka wapenzi wengi au kufanya mapenzi na wanawake au wanaume wanaojiuza.


Kwa baadhi ya nchi kinga dhidi ya kirusi huyu hutolewa hospitalini, ongea na daktari wako ili akuelekeze kama chanjo inapatikana kwenye hospitali yake. Kinga dhidi ya kirusi huyu humlinda mtu asipate madhara ya kirusi huyu na pia husaidia kupambana na kirusi huyu na kumwondoa mwilini.


Kunywa pombe kwa kiasi

Kuna tafiti zimefanywa zikionyesha kunywa pombe haina faida kimwili ya kukukinga na saratani, lakini tafiti zingine zinaonyesha unywaji wa pombe huhusiana na baadhi ya saratani kama saratani ini, koo n.k


Mtu anashauriwa kunywa uniti kati ya 14 na 21 kwa wiki, kwa mwanamke anaweza kunywa unit 14 za pombe kwa wikina mwanaume unit 21 za pombe kwa wiki. Muulize daktari wako akuambie unit hizi inamaanisha pombe za aina gani na ngapi au wasiliana na namba za simu chini ya tovuti hii


Kula chakula chenye afya njema


Chakula chako kihusishe mboga za majani kwa wingi na matunda, vyakula hivi vinasemekana kumkinga mtu ana saratani. Chagua matunda na vyakula vinavyosemekana kukinga mtu dhidi ya saratani


Soma zaidi kuhusu saratani ya koo(dalili, visababishi vipimo na matibabu) kwa kuingia kwenye tovuti yetu kwa kubonyeza hapa

54 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page