top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Kupunguza uzito na kitambi pasipo mazoezi | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Utangulizi

Chakula chenye wanga kidogo ni kile kinachodhibiti matumizi ya wanga unaopatikana kwenye nafaka, mboga za majani na matunda yenye wanga. Vyakula hivyo hutilia mkazo matumizi ya vyakula vyenye protini kwa wingi na mafuta. Zipo aina kadhaa za vyakula vyenye wanga kidogo, aina hizo ni lazima hutumika kulingana na ushauri wa daktari na afya ya mtu.

Madhumuni ya matumizi ya chakula chenye wanga kidogo

Matumizi ya chakula chenye wanga kidogo malengo yake makuu ni kupunguza uzito. Baadhi ya aina ya vyakula vyenye wanga kidogo huwa na faida zingine za kiafya mbali na kupunguza uzito ikiwa pamoja na kukuondoka katika kihatarishi cha kupata kisukari aina ya 2 na magonjwa mengine ya kimetabolik

Maelezo ya ziada kuhusu chakula chenye wanga kidogo

Kama jina linavyosema, chakula chenye wanga kidogo humdhibiti mtu kula wanga kwa wingi, wanga ni kirutubisho kinachotoa nishati. Wanga hupatikana kwenye vyakula vingi na vinywaji kama sukari, maziwa, matunda, unga, na mbegu za mimea pamoja na maharagwe na mboga za majani

Watengenezaji wa vyakula visivyo asili hutumia wanga katika vyakula wanavyotengeneza ulio kwenye mfumo wa sukari au unga. Mfano wa vyakula vyenye wanga ni mkate, chapati, keki, glukosi, soda na vinywaji vingi.

Mwili hutumia wanga kama chanzo kikuu cha nishati, wanga huvunywa vunjwa tumboni na kuwa sukari kisha hufyonzwa na kuingia kwenye mishipa ya damu ili kutumika kwenye chembe hai za mwili. Vyakula halisi vya wanga mfano unga wa mahindi usiokobolewa n.k humeng”enywa taratibu kwenye utumbo wa binadamu hivyo huchangia sukari kiasi kidogo kwenye mfumo wa damu kuliko vyakula ambavyo si halisi, mfano glukos, keki, soda n.k. hata hivyo vyakula halisi huwa na faida nyingi mbali na ile ya kukupa sukari kidogo, kwa kuwa huwa na virutubisho na madini.

Sukari inapofyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu husababisha kongosho kuzalisha homoni ya insulin kwa wingi, homoni hii hufanya kazi ya kuwezesha chembe hai za mwili zitumie sukari kutoa nishati, nishati hii husaidia chembe hai kuweza kufanya kazi zake mfano, moyo uendelee kusukuma damu, ubongo uendelee kufikiria, misuli ikusababishie uweze kutembea au kukimbia n.k. kiwango cha sukari iliyozidi mahitaji ya mwili katika damu hubadilishwa na homoni hii kuwa mafuta na kuhifadhiwa katika ngozi maeneo ya tumbo, makalio na mapaja, kifuani n.k


54 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page