Tafiti zinaonyesha kuwa vyakula aina Fulani hususani vile vyenye sukari na mafuta kwa wingi, huwa ni zawadi nzuri kwa ubongo. Ubongo unapopata zawaidi hii hutoa ishara endelevu kwa mwili ili utake kula zaidi aina hizi za vyakula hata kama hakuna mahitaji yake, hali hii huwa endelevu endapo mtu atatumia vyakula hivi kwa muda mrefu na kuacha huhitaji matibabu nguvu ya ziada. Jambo hili lilikuwa ni zuri kipindi cha enzi za mababu zetu kwa sababu kipindi kile watu walisafiri umbali mrefu na kufanya kazi ngumu bila kuwa na chakula. Chakula kilichohifadhiwa kwa njia ya mafuta kwenye mwili baada ya kula vyakula vyenye sukari namafuta kwa wingi kilikuwa kikitumika kuupa mwili nguvu katika kipindi hicho na hivyo ilikuwa faida kwao ukilinganisha na wakati huu ambapo watu wamezungukwa na vyakula kila mahari na kila aina na pia hawafanyi kazi ngumu.
Mfumo wa utengenezaji wa vyakula vya viwandani na vile visivyo vya asilia huwa na uwezo mkubwa wa kuharibu mfumo wa kawaida wa ubongo kwani huwekewa sukari na mafuta pamoja na kemikali zinazofanya utake kuvitumia wakati wote. watu wenye uwezo wa kutafuta maarifa kwa kusoma au kuwa na uwezo asilia wa kutambua chakula bora ni kipi cha kula huepukana na tatizo hili na pia huwa na afya njema.
Nimepita katika tafiti mbalimbali za nchi zilizoendelea wanaofanya tafiti nyingi, tafiti hizo zinaonyesha kuwa 1/3 ya watu wa bara la amerika wana uzito mkubwa kupita kiasi wenye BMI inayozidi 25 (Soma BMI kwenye kurasa za tovuti yetu). BMI huonyesha mahusiano kati ya uzito na urefu wa mtu, mtu mwenye BMI ya 25 na zaidi huwa na uzito mkubwa kupita kiasi usioshauriwa kiafya, na mtu mweye BMI ya 30 na kuendelea huwa na uzito mkubwa na mwenye kitambi. Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi pamoja na kitambi ni kihatarishi kikuu cha kupata magonjwa ya moyo, kisukari na mengine mengi ya kimetaboliki. Katika tafiti moja iliyochapishwa mwezi mei mwaka 2011 na Idara ya tafiti ya Bugando( BMC public health) iliyofanyika Kinondoni dar es salaam na mtafiti anayeitwa Dr.Grace A Shayo mwaka 2007 hadi 2008 naonyesha kuwa asilimia 19.2 ya wakazi wa kinondoni( kati ya wakazi 1249) walio fanyiwa tafiti wana uzito mkubwa kupita kiasi hii ni sawa na watu 240. Wanawake wameonekana wakiongoza kwa idani ya namba
Kommentare