top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Makovu na kusinyaa kwa Ini


Kusinyaa kwa ini husababishwa na magonjwa mbalimbali ya ini kama Michomo kwenye ini inayoweza kuletwa na maambukizi ya virusi vya hepatitis B na C na unywaji wa pombe wa kupindukia. Ini hufanya kazi mbalimbali mwilini ikiwa kuondoa sumu mwilini na kemikali hatari, kusafisha mwili na kuunda virutubisho vya masingi.

Makovu na Kusinyaa kwa ini hutokea kama madhara ya majeraha kwenye tishu za ini. Mara ini linapojeruhiwa, hujaribu kujirudisha kwenye hali ya kawaida sehemu iliyojeruhiwa, kufanya hivi makovu hutengenezwa. Jinsi makovu yanavyoendelea kutokea husababisha ini kusinyaa na hutengeneza makovu makubwa na kufanya ini lishindwe kufanya kazi zake.

Kufeli kwa ini kutokana na kusinyaa huweza kusababsha dalili Fulani ambazo hutokea, na kufeli kwa ini ni hatua ya mwisho inayotishia uhai wa mtu.

Uharibifu wa ini unaoelekea kusinyaa hauwezi kutibika au kuondolewa. Lakini kama ugonjwa ukigunduliwa mapema na kisababishi kimejulikana, uharibifu zaidi huweza kuzuiwa na sio kuondolewa kabisa kama ushafanyika.

Soma zaidi katika tovuti kwa kubonyeza hapa

48 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page