top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Makovu ya keloid | ULY CLINIC

Updated: Nov 25, 2020



Hii ni picha ya mfano wa kovu la keloid katika sikio

Keloid ni uvimbe katika ngozi ya sikio ama sehemu nyingine ya mwili, husababishwa na kukua sana kwa kovu pasipo kuthibitiwa. Ngozi hupona kwa kutengeneza kovu baada ya kuchanika ama kuumia na kwa mara ya kwanza kovu huwa na rangi nyekundu(kwa watu weupe) na muinuko mdogo. Mda unavyopita kovu hupungua na kupoteza mwinuko huo

Kwa bahati mbaya, wakati mwingine makovu huweza hukua sana na kutengeneza kovu gumu au laini na kusambaa zaidi ya eneo lililoathirika au chanika. Kwa kawaida makovu haya yanayoitwa keloid huwa yanawasha na kuuma kwa baadhi ya watu


Nini husababisha keloid?


Hakuna anayefahamu kwanini makovu haya yanatokea, ingawa baadhi ya watu huwa hawapati makovu haya kabisa, wanaopata makovu haya kufuatiwa na hali mbalimbali kama kujikata, kungatwa na mdudu, kupata michubuko ya ngozi ama baada ya kupata chunusi. Mara nyingi makovu haya hutokea maeneo ya masikio, mgongoni, kifuani na mabegani kuliko maeneo mengine ya mwili.

Wa afrika (watu wenye ngozi nyeusi) hupata makovu haya ya keloid kwa kiasi kikubwa sana kuliko watu wa mataifa mengine, ingawa kila mtu anaweza kupata makovu haya. Makovu ya keloid huwa haya badiliki kuwa saratani


Matibabu


Matibabu ya keloid ni magumu, ingawa kama mtu akizingatia yanaweza kuondoka kabisa 

Matibabu yapo ya aina tofauti yanayohusisha dawa za kukausha uvimbe pamoja na upasuaji.


Kujua matibabu yapi yanakufaa, endelea kusoma kwa kubonyeza hapa.

672 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page