top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Maswali ya majibu 1,000

Updated: Nov 6, 2021


Majibu ya kitaalamu ya maswali 1000 ya kiafya yaliyoulizwa kwa daktari wa ULY CLINIC

Karibu katika kurasa huu, katika kurasa hii utasoma kiundani kuhusu majibu ya maswali 100 yaliyoulizwa kwa daktari wa ULY CLINIC

Dalili za UTI


Katika makala hii, UTI linatumika kama neno tiba linalomaanisha Urinary tract Infection. Haya ni maambukizi yanayotokea katika mfumo wa mkojo.

Mfumo wa mkojo umegawanyika katika sehemu kuu mbili, mfumo wa chini ya mfumo wa juu, Dalili katika mfumo wa juu wa mkojo huwa pamoja na

  • Maumivu chini kidogo ya mbavu na upande wa kushoto au kulia au pande zote

  • Homa kali

  • Kukojoa damu au mkojo mchafu

Dalili katika mfumo wa chini wa mkojo ni pamoja;

  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

  • Maumivu wakati wa kukojoa

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Kutokwa na mkojo mchafu

  • Homa kiasi (si lazima)

​Soma zaidi kuhusu makala hii kwa kutafuta katika tovuti hii kuhusu, Bonyeza hapa maambukizi ya UTI, dalili za UTI, dawa za kutibu UTI.


2. Makundi ya vyakula


Kuna aina tano za makundi ya vyakula, aina hizi 5 za makundi ya vyakula humwongoza mtu kupata afya njema ya mwili na kiakili pia. Makundi hayo ni;


  • Matunda

  • Mboga mboga

  • Wanga

  • Protini

  • Maziwa

Bonyeza hapa kuendelea kusoma zaidi


3. Kuuma kwa chuchu ni dalili ya mimba?


Maumivu ya chuchu/titi ni moja kati ya dalili za mapema za ujauzito, huweza kutokea wiki la kwanza au la pili toka umepata ujauzito. Hata hivyo si kila maumivu ya chuchu husabaishwa na ujauzito. . Sababu zingine zinazoweza kupelekea maumivu ya chuchu ni maambukizi ya titi wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua, komahedhi, na maumbile ya titi.Soma zaidi kuhusu maumivu ya titi ndani ya tovuti hii.


4. Dawa ya kuzuia kutapika


Yapo makundi mbalimbali ya dawa zinazozuia kutapika, baadhi ya dawa zinazozuia kutapika ni;

  • Promethazine (phenergan)

  • Prochlorperazine(compazine)

  • Metoclopramide(reglan)

  • Diphenhydramine

Soma zaidi kuhusu dawa hizi ndani ya tovuti hii kwa kutafuta neno Dawa za kuzuia kutapika



5. Kifua kubana


Kifua kubana ni dalili kuu inayomaanisha kutumika sana kwa misuli au majeraha kwenye misuli, asilimia 20 hadi 49 ya kisababishi cha kifua kubana huletwa na matatizo ya isuli ya kifua. Haya huweza kutokea kwa sababu ya kuitumikisha misuli, uchovu mkuuu wa mwili au kuitumia misuli ndivyo sivyo. Kutumika sana kwa misuli ya kifua huleta dalili za kifua kubana. Sababu zingine zinazoweza kuchangia kifua kubana ni pamoja na;


  • Maambukizi ya COVID 19

  • Nimonia

  • GERD

  • Madhaifu ya Ang'zayati

  • Pumu ya kifua

  • Vidonga vya tumbo

  • Henia ya hayatazi

  • Kuvunjika kwa mbavu

  • Maambukizi ya herpes zosta kwenye ngozi(shingoz)

  • Mawe kwenye kifuko cha nyongo

  • Pankriataitizi

  • Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu

  • Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo

  • Kostokondraitizi

  • Madhaifu ya mojongeo ya misuli ya esofagasi

  • Kuchanika kwa esofagasi

Soma zaidi kuhusu makala hii katika tovuti ya ULY CLINIC kwa kutafuta maumivu ya kifua, kifua kuuma.


Bonyeza hapa kuendelea kusoma kuhusu maswali mengine

45 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page