top of page
Writer's pictureDr. Benjamin Lugonda, MD

Matibabu ya UTI ya kujirudia rudia| ULY CLINIC

UTI ni ugonjwa ulio maarufu sana katika jamii, wagonjwa wengi wamekuwa wakifika hospitali pia kwa ajili ya kupata tiba. Licha ya kuwa UTI ina tibika, ugonjwa huu huweza kujirudia rudia kwa baadhi ya watu ndani ya miezi sita toka umepata tiba na hivyo kuwa usumbufu kwa baadhi ya watu.


Kwanini UTI hujirudia?

UTI ya kujirudia rudia hutokea sana kwa wanawake kuliko kwa wanaume, kupata UTI ya kujirudia haimaanishi siku zote kuwa huzingatii usafi wa maeneo ya siri bali ni kwa sababu tu ya baadhi ya miili yao ina udhaifu wa kupata UTI aina hii.


Kwanini unapata UTI ya kujirudia?


Maambukizi ya UTI kwa asilimia zaidi ya 80 husababishwa na bakteria Eschelician coli, bakteria huyu huishi kwenye utumbo. Wakati wa kujisafisha bakteria anaweza kuhamishwa kutoka kwenye njia ya haja kubwa kwenda ukeni na kwenye mrija wa mkojo wa urethra


Vihatarishi


Vihatarishi vya kupata UTI ya kujirudia ni


  • Ngono(Kujamiana)

  • Kuwa na ugonjwa wa kisukari

  • Matumizi ya dawa za kupunguza kinga za mwili

  • Matumizi ya dawa za kuua shahawa ambazo pia huua viumbe walinzi(lactobacilli) walio ukeni

  • Koma hedhi- Kwa wanawake ambao wapo kwenye kipindi cha koma hedhi idadi ya viumbe walinzi(lactobacilli) hupungua na uwezo wa kibofu kusinyaa ili kutoa mkojo hupungua kutokana na mabadiliko ya mwili

Kinga ya UTI ya kujirudia


Ili kujikinga na UTI ya kujirudia rudia fanya mambo yafuatayo;


  • Kunywa maji ya kutosha, kiasi cha lita mbili hadi tatu kwa siku.

  • Tumia dawa za uzazi wa mpango zisizoua shahawa

  • Kojoa haraka baada ya kushiriki ngono

  • Usivaen nguo za ndani za kubana

  • Kama umeingia komahedhi, tumia homoni ya estrogen kukukinga kupata UTI ya kujirudia

  • Wakati wa kujisafisha njia ya haja kubwa, safisha kutoka mbele kwenda nyuma

Vipimo


Kipimo kizuri kwa ajili ya UTI sugu na ile ya kujirudia rudia ni kipimo cha culture & sensitivity. Kipimo hiki huweza kutambua aina na dawa ambayo inauwezo wa kuua bakteria huyo.


Kipimo hiki huweza kuwa cha gharama kubwa kwa baadhi ya watu lakini ni kipimo kizuri na cha uhakika


Matibabu


Watu wengi wamekuwa wakitafuta matibabu ya UTI sugu na ya kujirudia bila mafanikio, wengi baada ya kupata dalili huenda kununua dawa bila kuandikiwa na daktari wala kufanya kipimo.


Baadhi ya wagonjwa hufanya kipimo cha mkojo cha kawaida yaani urinalysis ambacho huonyesha una UTI bila kutoa majibu kwamba UTI hiyo ina sababishwa na kiini gani na dawa gani inauwezo wa kuua kiini hicho cha maradhi. Kufanya hivi kunaongeza usugu wa viini kwenye dawa na mwisho wa siku mgonjwa huyu huosa kabisa dawa za kumtibu au kuhitaji kutumia dawa zenye gharama zaidi kwa matibabu yake.


Kwa wataalamu wa afya ambao wanafahamu kuhusu UTI ya kujirudia na UTI sugu, utaagizwa kufanya kipimo cha culture & sensitivity. Baada ya majibu kutoka utapatiwa dawa ambayo imeonekana inafanya kazi kwako.


Baadhi ya dawa zinazotibu UTI ni;


Baadhi ya madhara ya UTI ya kujirudia rudia ni

  • Kupata UTI sugu

  • Usugu wa vimelea kwenye dawa


Soma Zaidi kuhusu UTI kwa kubonyeza hapa


ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii.


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elmu na ushauri zaidi kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kupiga namba za simu chini ya totuvi hii.


Rejea za mada hii;


  1. Health Harvard. When urinary tract infection keep coming back. https://www.health.harvard.edu/bladder-and-bowel/when-urinary-tract-infections-keep-coming-back. Imechukuliwa 24.11.2020

  2. AFP. Recurrent Urinary Tract Infections in Women: Diagnosis and Management. https://www.aafp.org/afp/2010/0915/p638.html. Imechukuliwa 24.11.2020

  3. Julien Renard, Stefania Ballarini, etal. Recurrent Lower Urinary Tract Infections Have a Detrimental Effect on Patient Quality of Life: a Prospective, Observational Study. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4363217/. Imechukuliwa 24.11.2020

  4. Shawn Dason etal. Guidelines for the diagnosis and management of recurrent urinary tract infection in women. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3202002/. Imechukuliwa 24.11.2020

  5. Patient education: Urinary tract infections in adolescents and adults (Beyond the Basics). https://www.uptodate.com/contents/urinary-tract-infections-in-adolescents-and-adults-beyond-the-basics/print. Imechukuliwa 24.11.2020

  6. Introduction to Urinary Tract Infections (UTIs). https://www.msdmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/urinary-tract-infections-utis/introduction-to-urinary-tract-infections-utis. Imechukuliwa 24.11.2020

  7. ULY CLINIC. UTI. https://www.ulyclinic.com/uti. Imechukuliwa 24.11.2020

715 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentários


bottom of page