Maumivu katika ya kifua
Maumivu katikati ya kifua mara nyingi hutokana na magonjwa ya ogani mbalimbali zilizo ndani ya kifua ya kifua na mara chache sababu zinaweza kuwa nje ya kifua au sehemu ya mbali na kifua. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya moyo, mapafu na ukuta wa dayaframu. Baadhi ya sababu zinahitaji matibabu ya haraka zaidi kwani mtu anaweza poteza uhai endapo hata pata msaada.
Endapo unapata maumivu yafuatayo unahitaji kupata msaada wa haraka.
Maumivu ya kifua yanayokuwa makali zaidi na kuhisi kama kifua kinachanika kwenye maeneo ya titi
Maumivu ya kifua yanayosambaa kwenye taya, mkono wa kushoto au mgongoni
Maumivu yanayoambatana na Kupoteza fahamu, mapigo ya moyo kwenda kasi na kupummua harakaharaka
Visababishi
Visababishi vya maumivu katikati ya kifua vinaweza kuwa;
Homa ya mapafu(nimonia)
Homa ya kifuko cha kongosho
Infaksheni ya mayokadiamu
Kolesistaitizi
Kubana kwa misuli ya kifua
Majeraha kwenye mbavu
Vidonda vya tumbo
Kucheua tindikali
Pumu ya kifua
Kostokondraitizi
Kusinyaa kwa mapafu
Magonjwa ya mijongeo ya misuli ya esofagasi
Kuchanika kwa mrija wa esofagasi
Henia ya hayatasi
Magonjwa ya mishipa ya moyo
Kuchanika kwa mshipa wa aotiki
Pankreataitizi
Bonyeza hapa kuendelea kusoma zaidi kuhusu makala hii
ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
Comentários