Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
Utangulizi
Mashino kwenye jino husababishwa na kutoboka kwa sehemu ngumu ya jino, mashimo hayo yanaweza kusababishwa na mkusanyiko wa mambo mablimbali. Meno kuoza na kutoboka hutegemeana, yaani meno yakioza hupelekea kuwa rahisi kutoboka. Tatizo la meno kuwa na mashimo au kuoza husababishwa na kushambuliwa na bakteria waliopo ndani ya kinywa, kula vyakula vyenye sukari kwa wingi, na kutosafisha meno yako vema
Tatizo la meno kutoboka linajulikana duniani kote na hutokea sana kwa watoto, vijana wadogo na wazee. Hata hivyo ifahamike kwamba kila mtu anaweza kuoza meno na kutoboka ikiwa ni kichanga au mtu mzima.
Endapo tatizo la meno kuoza na kutoboka halijatibiwa mapema, matobo hayo huweza kwenda chini mpaka kufika kwenye mzizi wa jino na kuanza kuleta Matatizo ya meno kuuma na jino kulegea na kutoka.
Dalili za meno kuoza
Kupata maumivu ya jino bila kuwa na sababu ya msingi
Jino kuwa na hisia sana, mfano kuuma dhidi ya kula vitu aina kadhaa
Kupata maumivu makali unapokula kitu cha baridi, moto au chenye sukari
Meno kubadilika rangi, rangi ya ugoro, kuwa na michirizi mweupe
Kupata maumivu wakati wa kung’ata meno
Visababishi
Meno kuoza husababisha matobo kwenye meno, tukio hili si la ghafla bali hutumia muda kutokea, baadhi ya maelezo ya namna ya Matatizo ya meno kuoza yanavyotokea yameelezewa hapa chini;
Kula vyakula vyenye sukari na wanga kwa wingi
Vyakula hivi husababisha kufanyika kwa kuta nje ya jino ambayo huliwa na bakteria, jinsi bakteria wanavyovamia kuta hii na kuila hupelekea kutengenezwa kwa kuta ingine ngumu ambayo haiwezekani kutolewa na bakteria
Kuta iliyotengenezwa kuvamiwa
Kuta ngumu iliyotengenezwa hapo juu huwa na asili ya u tindikali(asid) hivyo huvamia mfupa wa jino nan a kuuozesha na kusababisha vitobo. Vitobo vinapofanyika, asidi hupita na kuingia kwenye vitobo hivyo na kusababisha vitobo viendelee chini zaidi kwenye mzizi wa jino ambako kuna mishipa ya fahamu na damu. Mtu kwa hatua hii huwa anapat amaumivumakali ya jino.
Uvamizi kuendelea
Endapo mtu asipopata matibabu mapambano dhidi ya bakteria na kuta zilizofanyika huendelea, asidi huendelea kuharibu mzizi wa jino na kuleta maumivu zaidi, matokeo yake huweza kusambaa hadi kwenye mfupa unaoshikilia jino na kufanya uharibifu huko
Madhara
Madhara mengi yanayoweza kujitokeza ni kama vile
Maumivu ya meno
Usaha kwenye meno
Kuvimba kwa fizi
Kuvunjika na kuharibika kwa meno
Matatizo ya kushindwa kutafuna
Kucheza kwa meno na kung’oka
Kama mashimo yakiendelea kwa muda mrefu Matatizo yanayoweza kutokea ni pamoja na
Maumivu makali yanayoharibu ubora wa maisha ya mtu
Kupoteza uzito kutokana na kushindwa kula
Kung’oka kwa meno
Kufanyika kwa usaha kwenye mzizi wa meno
Kujikinga
Osha meno yako na dawa ya meno yenye madini ya fluoride, angalau mara mbili kwa siku, au kila baad aya kula chakula
Suuza mdomo wako kwa maji yenye fluoride(yanawezaekana yakawa maji maalumu)
Mwone daktari mara kwa mara kwa uchunguzi endapo una Matatizo ya meno
Ziba meno yaliyo mazima kujikinga na meno kutoboka haswa kwa watoto walio kwenye umri wa kwenda shule
Kunywa maji ya bomba- maji haya huwa na fluoride ambayo hulinda meno
Usile mara kwa mara vyakula vyenye sukari kwa wingi na vinywaji vyenye sukari
Pata matibabu ya mara kwa mara ya madini ya fluoride kutoka kwa daktari wako ili kujikinga na kmeno kutoboka
Tumia dawa za kuua bakteria endapo una maambukizi kwenye meno
Tumia dawa asilia ambazo zinasemekana kuponya meno na kuzuia yasitoboke. Kumbuka unabidi utumia dawa zilizothibitishwa na kuwa hazina madhara.
Endapo una shida ya meno kutoboka wasiliana nasi kwa namba za simu zilizo chini ya mtandao huu kwa ushauri na tiba. Kusoma zaidi kuhusu vihatarishi bonyeza hapa
Toleo la 3
Imeboreshwa14/2/2019
댓글