top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Ni maisha gani mgonjwa wa kisukari anatakiwa kuishi?


Mgonjwa wa kisukari anapofuata masharti ya matibabu huweza kuzuia madhara makubwa ya kisukari yanayoweza kumpata

Haijalishi una kisukari aina gani mambo ya msingi ya kuzingatia ni


Weka mikakati ya kudumu

Jifunze mambo yote unayoweza. Kuwa na wahusiano na mtoa elimu ya kisukari na muulize anayekutibu kama unataka msaada wowote ama unamaswali kuhusu maisha na kisukari


Kupunguza uzito asilimia 7 tu ya uzito wako endapo kama unauzito kupita kiasi kutafanya mabadiliko makubwa katika kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Chakula chenye afya ni kile chenye kiwango cha mafuta yenye rehani(cholesterol) kidogo na chenye matunda, mboga mboga, unga usiokobolewa, na mimea jamii ya kunde kwa wingi(maharagwe, kunde, mbaazi, n.k)


Fanya mazoezi kama sehemu ya maisha yako

Mazoezi ya kuzingatia yanaweza kumsaidia mtu kuzuia kupata kisukari ama kupata kisukari aina ya pili na pia huweza kumsaidia mtu mwenye kisukari kuwa na kiwngo kidogo cha sukari katika damu. Dakika 30 za mazoezi ya kawaida kama kutembea katika siku za wiki hushauriwa sana. Mazoezi haya kwa pamoja ,kucheza au kutembea na mazoezi mazito kama ya kunyanyua kitu ama kukimbia mara mbili kwa wiki mara nyingi husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwa ufanisi mkubwa sana pekee


Aina ya maisha ya kuishi kwa watu wenye kisukari


Jitambue mwenyewe

Vaa kitu kinachoonyesha kuwa unakisukari na uwe na kit yako ya kisukari karibu nawewakati wowote kama shida ya haraka itatokea, hakikisha marafiki ama ndugu wa karibu wanajua kwamba unakisukari ili wawe msaada kwako endapo shida itatokea ya haraka


Panga muda wa kuonana na daktari na kufanya vipimo vya macho kila mwaka

Si kwamba uonane na dr kila mwaka unapopita, bali utaonana na dr kama alivyokupangia kwa ajili ya clinic ya kisukari. Ni jambo la msingi sana kuwa na uchunguzi wa macho kila mwaka na uchunguzi huu utasaidia kutambua madhara makubwa yanayoletelezwa na kisukari na kutambua matatizo mengine. Mtaalamu wa macho atatazama kama una mtoto wa jicho, kama retina zako zimehariika na kama una ongezeko la shinikizo ndani ya jicho(glaucoma)


Pata chanjo kwa wakati


Kisukari hufanya kinga ya mwili kupungua sana hivyo ni vema kupata chanjo ya mafua na homa ya ini inayosababishwa na hepatitis B kama hujawahi pata chanjo


Kagua miguu yako kila mara

Osha miguu yako kila siku kwenye maji ya uvuguvugu, ikaushe taratibu kwa kitambaa haswa katikati ya vidole chunguza miguu yako kwa kioo kama ina malenge na vidonda wekundu na kuvimba. Mwone dr kama una kidonda ama unatatizo jingine kwa sababu vidonda huwa haviponi kirahisi kwa mtu mwenye kisukari


Hakikisha kiwango cha cholesto na shinikizo lako la damu lipo kawaida

Kula chakula chenye afya na mazoezi kunaweza kudhibiti shinikizo la damu na kiwango cha rehamu mbaya kwenye damu. Dawa pia zinaweza kuhitajika hapa


Chunguza meno yako

Brush meno yako vizuri kila unapokula


Acha kuvuta sigara


Kunywa pombe kwa kiasi kidogo sana

Pombe huweza kusababisha kupandisha ama kushusha kiwango cha sukari mwilini. Hivo unashauriwa unapokunywa kunywa hata glasi moja ama 2 kwa wiki ya pombe isiyo kali na wakati wote uwe na chakula unapotaka kunywa pombe. Chunguza kiwango chako cha sukari kabla ya kwenda kulala


Ondoa/jiepushe na mawazo sana

jifunze kuishi bila mawazo kwani itakusaidia kupunguza kiwango cha sukari. Mawazo husababisha kupandisha kiwango cha sukari katika damu na hivo kukusababishia sukari kutoshuka. Endapo utaishi bila mawazo ama kupunguza mawazo itakusaidia sana


Kumbuka hakuna dawa ya kutibu kisukari mpaka sasa. Dawa unazotumia husaidia kudhibit tu kiwango cha sukari na ni vema kutumia kama ulivyoshauriwa na dr.


67 views0 comments

Recent Posts

See All

Commentaires


bottom of page