top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Njia za kujifungua mtoto

Updated: Nov 6, 2021

Njia gani uchague kujifungua mtoto wako?


Zipo njia mbili mama anaweza kuchagua endapo anataka kujifungua mtoto, hata hivyo uchaguzi wa njia ya kujifungua unaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na uchaguzi wa mama au matatizo ya kiafya kati ya mtoto au mama. Njia ya upasuaji imekuwa maarufu sana katika karne ya 21 ambapo wanawake wengi wamekuwa wakichagua njia hii kwa sababu imeonekana kuwa ni salama na haina madhara. Licha ya njia hii kuwa maarufu kutokana na sababu mbalimbali, yapo madhara ambayo mtoto na au mama anaweza kuyapata kwa kujifungua kwa njia hii.


Katika makala hii utajifunza njia mbalimbali za kujifungua na faida zake.

1. Kujifungua kwa njia ya upasuaji

Kujifungua kwa upasaji ni njia mojawapo ya kujifungua kupitia uwazi mdogo unauchnwa na mikasi chini ya kitovu chako. Njia hii imerekodiwa kutumika kwa mara ya kwanza huko Swaziland miaka 1580 ambapo Jacob Nufer alimfanyia mkewe mara baada ya kuona hatua za uchungu haziendelei. Hata hivyo njia hii iliendelea kutumika kama njia ya kuwatoa watoto tumboni kwa wamama wajawazito waliofariki kabla ya kujifungua.


Maendeleo ya sayansi na kujifunza zaidi kuhusu upasuaji kwenye maiti na ugunduzi wa dawa za kupooza mwili katika karne ya 19, ilifanya wanasayansi waanze kufikiria na kutumia njia hii kuwa sehemu ya njia ya kujifungua.



Soma kuhusu uchungu kwa kubonyeza hapa


ULY clinic inakushauri siku zote wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya.

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga simu au bonyeza 'Pata Tiba' kupitia neno Pata Tiba chini ya tovuti hii. au Bonyez ahapa

74 views0 comments

Recent Posts

See All

Commenti


bottom of page