top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Ngono na Ujauzito

Updated: Nov 6, 2021

Kujamiana wakati wa ujauzito



Kuna maswali mengi watu wameuliza kwenye tovuti hii ya ULY CLINIC kuhusu kujamiana wakati wa ujauzito, baadhi ya maswali ni


  • Je inaruhusiwa kujamiana wakati wa ujauzito?

  • Ni wakati gani wa kujamiana wakati wa ujauzito?

  • Tahadhari gani natakiwa chukuwa nikiwa najamiana wakati wa ujauzito?

  • Je kuna faida za kujamiana wakati wa ujauzito?

  • Je ni pozi lipi zuri la kujamiana wakati wa ujauzito?

  • Ni vema kutumia kondomu wakati wa ujauzito?


Makala hii imejibu maswali hayo

Kujamiana wakati wa ujauzito kitaalamu haikatazwi kabisa, hukubalika na huonekana kuwa ni moja ya njia nzuri ya kufanya upate uchungu na kujifungua kirahisi haswa ukijamiana katika kipindi cha miezi ya mwisho wa ujauzito.


Je nitamwumiza mtoto tumboni wakati huu wa ujauzito?


Hapana. Mtoto huwa amefichwa ndani ya misuli ya kuta za mji wa uzazi na kwenye chupa ya maji ya amniotiki. Mtoto hupata ulinzi dhidi ya migandamizo tumboni kupitia maji haya yaliyo na sifa ya kufyonza mitikisiko yote inayoingi kwenye mwili wa mama na tumboni. Kufanya mapenzi hakuwezi mdhuru mwanao tumboni endapo tu huna shida ya kupata uchungu kabla ya wakati na tatizo ya kujishikiza vibaya kwa kitovu cha mtoto.


Hata hivyo ujauzito utabadilisha uwezo na uhuru wako kutumia mapozi mbalimbali ya kujamiana uliyokuwa umeyazoezi wakati haupo mjamzito. Baadhi ya watu hupata hamu ya kujamiana wakati huu na wengine hamu hupungua.


Pozi zuri la kujamiana ni lipi?


Unaweza kutumia pozi lolote ambalo una uhuru nalo, hata hivyo jinsi ujauzito unavyokuwa utakosa uhuru wa kukaa baadhi ya mapozi. Utahitaji kufanya uchunguzi ili kutambu ni pozi gani linakufaa wewe na unalifurahia.

NAruhusiwa kutumia kondomu wakati wa kujamiana?


Matumizi ya kondomu sio lazima wakati huu endapo

  • Una mpenzi mmoja tu na mwaminifu

Tumia kondomu endapo,

  • Unafanya mapenzi na mtu mwingine mbali na mumeo mwaminifu

  • Una dalili za magonjwa ya zinaa

Je kuna wakati hutakiwi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?

Kusisimuliwa kwa chuchu, kupata ogazimu na kuingia kwenye shingo ya kizazi kwa homoni ya prostaglandini iliyo kwenye shahawa huweza kuamsha uchungu kabla ya wakati wake. Hivyo hutakiwi kufanya mapenzi endapo;

  • Unatokwa na damu ukeni bila sababu ya msingi

  • Unavuja maji kutoka chupa ya uzazi

  • Shingo ya uzazi imefunguka

  • Unatatizo la kutojiweza kwa shingo ya uzazi

  • Plasenta previa --- kondo la nyuma limejishikiza karibu shingo ya kizazi

  • Una historia ya kupata uchungu kabla ya wakati

  • Una historia ya kujifungua kabla ya wakati

Je kuna madhara ya Kutofanya mapenzi

Hakuna madhara yoyote ya kutofanya mapenzi wakati wa ujauzito, kuna njia nyingi unaweza kuzitumia ili kujiridhisha kimapenzi kama vile kufanyiana masaji, kubusiana.

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

Rejea za makala hii,


  1. NHS.sex in pregnancy. https://www.nhs.uk/conditions/pregnancy-and-baby/sex-in-pregnancy/. Imechukuliwa 13.09.2020

  2. STDs during pregnancy — CDC fact sheet. Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/std/pregnancy/STDFact-Pregnancy.htm. Imechukuliwa 13.09.2020

  3. Lockwood CJ, et al. Prenatal care: Initial assessment. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 13.09.2020

  4. Butler Tobah YS (expert opinion). Mayo Clinic, Rochester, Minn. Imechukuliwa 13.09.2020

  5. Gabbe SG, et al., eds. Preconception and prenatal care. In: Obstetrics: Normal and Problem Pregnancies. 7th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 13.09.2020

  6. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ090. Early pregnancy loss. American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Early-Pregnancy-Loss. Imechukuliwa 13.09.2020

310 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page