Ukuaji wa kichanga wa kawaida na mtoto hadi miaka 10
Watoto huzaliwa na uzito tofauti na kila mtoto anaweza kukua tofauti kutegemea chakula anachokula mama na idadi ya kunyonya mtoto. Hata hivyo kama hali zote za kina mama na watoto zikiwa zinafanana watoto hao hukua katika kiwango sawa. Hapa chini kuna maelezo namna mtoto anavyotakiwa kuongezeka uzito na urefu kwa mwaka wa kwanza wa maisha yake;
Mtoto anapozaliwa mpaka miezi sita, mtoto atakuwa kwa sentimeta 1.5 hadi 2.5 kwamwezi, and kuongezeka uzito wa gramu 140 hadi 200 kwa wiki. na mtoto anapofikisha umri wa miezi mitanoanakuwa na uzito mara mbili wa ule aliozaliwa nao.
Miezi sita na kuendele hadi mwaka 1. Mtoto huongezeka urefu wa sentimita 1 kila mwezi na uzito wa gramu 85 hadi 140 kwa wiki moja. Kwa ujumla mtoto huwa na uzito mara tatu zaidi ya kilo alizozaliwa nazo anapofikisha umri wa miezi 12(mwaka 1)
Kati ya umri wa mwaka mmoja na miaka miwili mtoto atakuwa kilo 2.2 tu
Kuanzia miaka 2 hadi mi 5 mtoto atakuwa kwa kilo 2.2 kila mwaka
Kati ya miaka 2 hadi 10 mtoto hukua taratibu sana, lakinihuanza kukua haraka sana kuanzia miaka 10 na kuelekea wakati mwingine huanza kukua haraka kuanzia miaka 9
Comentarios