Umri wa kuota meno ya kwanza kwa mtoto
hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine, baadhi ya watoto huzaliwa na meno ya awali na wengine huota meno baada ya miezi 4 hadi mwaka. Hata hivyo tegemea mwanao kupata meno akiwa ndani ya mwaka wake wa kwanza toka amezaliwa. Tafiti zinaonyesha watoto wengi huota meno yao ya kwanza wakiwa na miezi sita. Dalili zifuatazo zinaweza kuwa ishara ya mtoto kuota meno ya kwanza.
Dalili za meno kuota kwa mtoto
Maumivu ya fizi na kubadilika rangi (kuwa na rangi nyekundu wakati meno yanataka kutoka nje)
Shavu moja la mtoto hubadilika rangi
Mtoto huchokonoa masikio(kwa sababu ya miwasho au maumivu)
Kutoa udenda zaidi ya kawaida
Hupenda kutafuna na kusugua fizi zaidi ya kawaida
Mtoto kulialia na kusumbua isivyo kawaida
Kuweka mikono kinywani na kuinyonya
Kung'ata ziwa la mama anapokuwa ananyonya
Kuharisha(hii ni baadhi ya dalili ambayo huripotiwa na wazazi)
Pitia makala ya dalili zinazoambatana na kuota meno kwa maelezo zaidi.
Kumbuka endapo mtoto akipata homa halisi yaani joto la mwili kupanda kiasi cha nyuzi joto za centigredi 38, wasiliana na daktari kwa sababu kuota meno huwa hakusababishi kupata hivi kwa joto.
Kwa sababu watoto wengi huota meno kwenye umri wa kuanzia miezi sita, ni vema mzazi ukawa na tabia ya kusafisha meno hayo, tumia mswaki wa watoto kusafisha meno ya mtoto kwa kutumia dawa ya meno yenye fluoride mara mbili kwa siku ili kuimarisha meno yake. Hakikisha mtoto hamezi dawa.
Pia katika kipindi hiki msaidie mtoto kuondoa maumivu ya jino kwa kutumia panado kulingana na dozi uliyoelekezwa na daktari wako. Kanda sehemu jino linapoota ili kuondoa maumivu na kumtuliza mtoto. Tumia vifaa maalumu pia kumwekea kinywani ili mtoto apate kung'ata na kujisikia vema dhidi ya miwasho ya meno kuota. Kuwa makini hata hivyo mtoto asimeze au kupaliwa.
Meno huota kwa mpangilio upi?
Maelezo ya hapa chini yameelezea wastani wa umri wa kuota meno kwa watoto walio wengi, hii ndio maana kuna utofauti wa maelezo haya na picha hapo juu. Ili kufahamu meno yanayozungumziwa ni yapi, tazama picha juu kufananisha.
Meno ya insiza ya chini kwanza
Huanza kuota kwenye umri wa miezi 5 hadi 7
Meno ya insiza ya juu
Huanza kuota kuanzia miezi 6 hadi 8
Meno ya insiza ya pembeni juu
Huanza kuota kuanzia miezi 9 hadi 11
Meno ya insiza ya pembeni chini ya taya
Huanza kuota kuanzia miezi 10 hadi 12
Meno ya kwanza ya mola
Huanza kuota kuanzia miezi 12 hadi 16
Meno ya kanaini
Huanza kuota kati ya miezi 16 hadi 20
Meno ya pili ya mola
Huanza kuota miezi 20 hadi 30
Kwa maelezo zaidi pitia picha hapo juu.
Ni umri gani meno yote ya kwanza huwa yameota?
Watoto wengi huwa wameshaota meno yao yote ya awali mpaka wanapfikia umri wa miaka 2 na nusu
Soma zaidi kuhusu makala zingine kwa kubofya makala zingine zinazohusu:
Chanjo kwa mtoto
Hatua za ukuaji wa mtoto
Namna ya kumfanya mtoto ale chakula zaidi
Namna ya kuandaa lishe ya mtoto
Namna ya kunyonyesha mtoto
Wakati gani maziwa ya mama huanzakutoka baada ya kujifungua?
Utapiamlo
Uandaaji wa lishe ya mtoto
Ukuaji wa mtoto wa kawaida(uzito na urefu
Maendeleo ya mtoto Mwaka 1 hadi 2
Maendeleo ya mtoto Miaka 2 hadi 3
Maendeleo ya mtoto Miaka 3 hadi 5
Angalia video fupi ya makala ya umri wa kuota meno kwa maelezo ya ziada.
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote utafute maelezo zaidi kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu chini ya tovuti hii au bonyeza Pata Tiba
Rejeza za mada hii,
NHIS. Baby teething symptoms.https://www.nhs.uk/conditions/pregnancy-and-baby/teething-and-tooth-care/. Imechukuliwa 17.08.2020
Healthchildren. https://www.healthychildren.org/English/ages-stages/baby/teething-tooth-care/Pages/Babys-First-Tooth-Facts-Parents-Should-Know.aspx. Imechukuliwa 17.08.2020
When do baby start teething?. https://www.medicinenet.com/teething/article.htm. Imechukuliwa 17.08.2020
Comentarios