top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Umuhimu wa kulia machozi|ULY CLINIC

Kulia machozi huondoa homoni zinazoleta msongo mwilini


Kulia ni kitendo muhimu sana katika maisha ya binadamu, watu wengi wanadhania kulia ni kuonyesha udhaifu, hata hivyo tafiti za kisayansi zinaonyesha tendo hili lina faida ya kuondoa sumu mwilini, kutuliza mwili na hisia, hupunguza maumivu makali, hupunguza msongo, huondoa majonzi, kurejesha uwiano wa hisia za furaha na majonzi na huongeza usingizi.Mwitikio wa kulia kwenye jambo linalokupa furaha au huzuni ni jambo la kawaida kwa binadamu


Kwanini watu wanalia?


Kuna sababu mbalimbali zinaweza kufanya mtu alie machozi


Vitu vinavyoweza kufanya mtu mzima alie ni kama vile

  • Kupoteza kitu au watu wa thamani

  • Kuangalia tamthilia zinazosikitisha

  • Maumivu ya mwili

  • Kupoteza tumaini la jambo au mambo fulani

  • Kuoa au kuolewa

  • Kusikiliza mziki wa kusikitisha

  • Kurudiana kwa watu waliopotezana


Nini knatokea ndani ya mtu akilia machozi?


Kutoa machozi ni sawa na kufungua sufuria inayochemka maji huku imefunikwa na mfuniko mzito, unapofungua sufuria hii, presha kubwa ya mvuke itatoka kutoka. Presha inayotoka ni sawa na msongo ulionao ndani ya mwili unaotakiwa kutolewa kwa njia ya machozi. Machozi yanapotoka huachilia nguvu haribifu kutoka ndani ya mwili na akili pia. Endapo nguvu hii haitatoka mwilini kwa njia ya machozi, mwili na akili itajawa na msongo unaoweza leta madhara makubwa.


Nini kinatokea ndani ya mwili unapokuwa unalia machozi


Kuna maelezo mbalimbali yanayosema kuwa, endapo ukilia unaondoa msongo ndani ya mwili, hii ni kweli kwani wakati unalia, machozi yanayotoka hutoa sumu na homoni mbalimbali ikiwapamoja na homo cortisol inayosababisha msongo mwilini. Homoni hizi zinnapopotea kupitia machozi, mtu hupata tumaini, hufikiria vema na wengine hupata usingizi.


Wakati gani kulia machozi huwa na msaada katika mwili wako?


Sio kila kulia machozi kutasaidia kupunguza msongo mwilini mwako, ni kweli kwamba hii inategemea unalilia nini na kwenye mazingira gani. Vitu vinavyoweza kufanya kulia kukawa na faida au hasara ni,

  • Utu wa mtu, endapo una utu wa kuwa na mawazo mengi kulia hakutakusaidia. Tafuta namna ya kumaliza mawazo hayo kwa kuongea na watu au kupata majibu ya matatizo yako

  • Hali ya kisaikolojia- endapo una ugonjwa wa msongo wa mawazo, hata kama ukilia vya kutosha haitakusaidia kuimarisha hali ya moyo wako.

  • Matukio ambayo hayarekebishiki,

  • Mwitikio wa wengine kwenye uliaji wako, endapo utapokelewa na kusikilizwa na kutiwa moyo, utapata faraja moyoni, endapo watuw engine wataitikia kwa kukuona dhaifu au wakachukulia tofauti na ukarimu, kulia huku hakutakupa faraja ya moyo.

Wakati gani kulia machozi si kawaida na unatakiwa onana na daktari?


Endapo unalia pamoja na kuwa na dalili zifuatazo, hiyo si kawaida na inawezekana una msongo wa mawazo. Ukipata dalili zifuatazo ni vema ukawasiliana na daktari wako

  • Mawazo ya kujiua

  • Maumivu ya mwili yasiyoelezeka

  • Kuwa mkali kwa vitu vidogo

  • Kukosa usingizi au muda mwingi sana

  • Kukosa hamu ya kula, kupoteza uzito au kuongezeka uzito

  • Kuishiwa nguvu

  • Hisia za huzuni au kukata tamaa


Hitimisho


Kulia kwa kutoa mchozi ni moja ya njia ya binadamu kuonyesha hisia zake na tendo hili hubadilika kwenye kipindi kizima cha maisha yake na hutegemea jinsia. Kulia kwa kutoa machozi hufahamika kuongeza ukaribu na watu jamaa kwenye jamii, kuamsha faraja, umoja, kusaidiana n ahata kuzuia kufanyiwa matendo mabaya kama vile kuuawa kwa ukatili na kufanyiwa vurugu.


Rejra za mada hii


  1. Asmir Gračanin , et al. Is crying a self-soothing behavior?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6402489/#R29. Imechukuliwa 21.02.2021

  2. Breuer, Josef, and Sigmund Freud. Studies on hysteria. Hachette UK, 2009. Imechukuliwa 21.02.2021

  3. Frey WH (1985). Crying: The mystery of tears Minneapolis, MN: Winston Press. Imechukuliwa 21.02.2021

  4. Gračanin A, et al. Is crying a selfsoothing behaviour? Frontiers in Psychology, 28(5), 502. doi:10.3389/fpsyg.2014.00502. inapatikana https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24904511/. Imechukuliwa 21.02.2021

  5. Bowlby J (1980). Loss: Sadness and depression New York, NY: Basic Books

  6. Nelson JK (2005). Seeing through tears: crying and attachment New York, NY: Routledge.

  7. Hasson O (2009). Emotional tears as biological signals. Evolutionary Psychology, 7, 363–370.

  8. Nelson J. K. (2008). “Crying in psychotherapy: Its meaning, assessment and management based on attachment theory,” in Emotion Regulation: Conceptual and Clinical Issues eds Vingerhoets A. J. J. M., Nyklicek I., Denollet J. (New York, NY: Springer; ) 202–214

  9. Hendriks M. C. P., Nelson J. K., Cornelius R. R, Vingerhoets A. J. J. M. (2008b). “Why crying improves our well-being: an attachment-theory perspective on the functions of adult crying,” in Emotion Regulation: Conceptual and Clinical Issues eds Vingerhoets A. J. J. M., Nyklicek I., Denollet J. (New York, NY: Springer; ) 87–96

  10. Is Crying Good for You?. https://www.webmd.com/balance/features/is-crying-good-for-you#. Imechukuliwa 22.03.2021

  11. Chronic stress puts your health at risk. Chronic stress can wreak havoc on your mind and body. Take steps to control your stress.https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/stress-management/in-depth/stress/art-20046037#. Imechukuliwa 22.03.2021

165 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentarios


bottom of page