Vihatarishi
Umri wa mtu-watoto kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 huwa na kihatarishi cha kupata maambukizi haya kwa sababu ya umbo na ukubwa wa mrija(eustachian) wa sikio na kuwa na kinga za mwili kidogo
Mtoto kusoma shule zenye watoto wengine
Watoto wanaosoma shule za boording huwa na kihatarisi cha kupata mafua na maambukizi ya masikio kuliko watoto wanaokaa nyumbani, hii ni kwa sababu wanajiweka kwenye hatari ya maambukizi kama vile homa ya baridi(mafua)
Kunyonyesha mtoto kwa chupa
Mtoto kunyonyeshwa kwa njia ya chupa haswa akiwa amelala chali hupata maambukizi haya sababu ikiwa maziwa huwa yanaingia kwenye mrija wa sikio. Watoto wanaonyonya maziwa ya mama kwenye chuchu huwa hawapati maambukizi hay asana.
Hali ya msimu
Hali za kimsimu huwa sababu kuu ya kupata maambukizi ya masikio hasa kipindi cha baridi na mvua ambapo watu hupata sana mafua na homa ya baridi. Watu wenye aleji na maua hupata sana maambukizi ya masikio wakati wa msimu wa maua
Hewa chafu
Hewa iliyochanganyika na moshi wa sigara au tumbaku au maeneo yenye uchafuzi wa hewa huwa kihatarishi kikubwa cha kupata maambukizi ya masikio
Kusoma zaidi bonyeza hapa
Comments