Imeandikwa na ULY CLINIC
Pumu ya kifua- Asthma
Pumu ya kifua ni hali ambayo huyoke pale njia za mfumo wa hewa/mfumo wa upumuaji ikivimba na kuzalisha ute ute wa utelezi kupita kiasi. Hali hii huweza kusababisha kushindwa kupumua vema, kukohoa, sauti za miruzi katika kifua na kuishiwa pumzi.
Kwa baadhi ya watu, pumu huwa si tatizo sana kwao ikiwa na maana huwa haileti dalili za kutisha. Lakini kwa watu wengine wenye pumu huambatana na dalili kali zinazoweza kupunguza ubora wa amaisha yake
Pumu huwa haitibiki, lakini dalili zake zinaweza kutibiwa. Na kwa sababu pumu ya kifua hubadilika badilika mda hadi mda, ni vema kuongea na daktari wako ili aulize kuhusu dalili zako na afanye matibabu kulingana na dalili ulizonazo wakati husika.
Dalili za pumu ya kifua
Dalili za pumu ya kifua hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingiine. Unaweza kuwa na dalili za mara kwa mara ama unaweza usipate dalili kwa kipindi kirefu sana na unaweza kuwa na dalili za kila siku pia. Na kwa watu wengine wanaweza kuwa na dalili wakiwa wanafanya kazi Fulani kama wakiwa wanafanya mazoezi
Dalili na viashiria vya pumu ya mapafu ni kama
-
Kuishiwa pumzi
-
Kifua kubana au maumivu ya kifua
-
Kushindwa kulala kwa sababu ya kuishiwa pumzi, kukohoa ama miruzi kwenye kifua.
-
Miruzi kwenye kifua ukiwa unatoa pumzi(miruzi ni dalili muhumu sana ya pumu ya kifua kwa watoto)
-
Kukohoa au miruzi kutokea kwa kipindi Fulani ambayo huendelea kuwa kubwa zaidi endapo una maambukizi ya virusi njia ya hewa, kama mafua
Viashiria vya pumu ni kama vile
-
Kupata Dalili za pumu amabazo zinatokea m ara kwa mara na zinakusumbua
-
Hali ya kushindwa kupumua kuongezeka makali zaidi
-
Kutumia dawa za pumu kutuliza dalili zake haraka mara nyingi zaidi
Baadhi ya watu pumu zao huamka kwenye mazingira kama
-
Akiwa anafanya mazoezi- huweza kuwa hatari zaidi kama hewa ikiwa ya ubaridi ama kavu
-
Pumu ya mazingira Fulani- huamshwa endapo mtu akiwa mazingira Fulani yenye vichochezi au viamsha pumu kama harufu ya kemikali, gesi ama vumbi, mende, poleni kutoka kwenye maua ya mimea n.k
-
Pumu mzio/aleji- hutokea endapo mtu ana mzio kwenye bidhaa au vitu Fulani akiwa karibu navyo ama akitumia kama sabuni
Viamsha pumu vingine ni kama
-
Vikereketa katika njia ya hewa kama vile poleni, mavi ya wanyama au wadudu, mende, vumbi na poleni
-
maambukizi kwenye mapafu kama vile mafua na baridi
-
Mazoezi
-
hewa ya ubaridi
-
Uchafuzi wa hewa/uchafu kwenye hewa wa hewa kama moshi
-
Madawa fulani kama ibroprofen n.k
-
Kuwa na msongo wa mawazo
-
Vidonda vya tumbo(GERD)
-
Baadhi ya vinywaji na chakula vyenye allergen kwako kama bia, wine na viazi vilivyosindikwa
Wakati gani wa kumwona daktari
-
Kushikwa na pumu ghafla kunaweza kuleta hatari katika afya yako na uhai kwa ujumla. Ongea na daktari wako kujua nini cha kufanya endapo unapata dalili na viashiria vya pumu na endapo dalili pia zinakuwa mbaya. Dalili zinazohitaji matibabu ya haraka ni kama
-
Kuongezeka kwa shida ya kupumua, kuishiwa pumzi au miruzi kifuani
-
Kutopata unafuu hata ukitumia dawa za kupuliza kwenye mapafu kupitia mdomoni kama albuterol//salbutamol
-
Kuishiwa pumzi unapokuwa unafanya kazi ndogo sana
-
Wasiliana na daktari wako kama unafikilia una pumu
Vihatarishi vya kupata pumu ya kifua
Vitu vingi vinaweza kumweka mtu hatarini kupata pumu. Vitu au mambo hayo ni kama
-
Kuwa na ndugu wa damu mwenye tatizo la pumu(kama mzazi na mdogo wako)
-
Kuwa na allegy kwenye vitu vingine kama pumu ya ngozi, au kusumbuliwa na tatizo la mafua(homa ya hay)
-
Kuwa na uzito kupita kiasi
-
Kuvuta sigara
-
Kukaa karibu na mtu anayevuta sigara
-
Kukaa kwenye nyumba inayotumia kuni kupikia(kwenye moshi wa kuni_)
-
Kuwa kwenye mazingira yenye kemikali zinazoamsha asthma/pumu kama madawa ya shambani, madawa ya nywele, na madawa mengine
Pumu imegawanywa kwenye dalili kuu nne
-
Pumu ya wakati(inayotokea kwenye muda fulani) na yenye dalili zisizo kali-dalili chache na ndogo ndogo zinaweza kutokea hadi mara mbili mchana kwa wiki au mara mbili usiku katika mwezi
-
Pumu endelevu na yenye dalili kiasi- dalili zaidi ya mara mbili kwa wiki lakini si zaidi ya mara moja kwa siku
-
Pumu ya wastani na endelevu- dalili hutokea mara moja kwa siku, na zaidi ya mara moja wakati wa usiku kwa wiki
-
Pumu kali endelevu- ni pumu inayotokea siku nzima na mara nyingi wakati wa usiku
Vipimo na matibabu
Ili kujihakiki ama kuondoa uwezekano wa magonjwa mengine ambayo si pumu na kufanya matibabu sahihi ya pumu basi daktari ataagiza baadhi ya vipimo ili vifanyike kujihakiki
Magonjwa mengine yanayoweza kuwa na dalili kama za pumu ni COPD
Vipimo vya kupima uwezo wa ufanyaji kazi wa mapafu yako
Spirometry- kipimo ambacho unapuliza hewa kwenye mashine hii na inapima uwezo wa mapafu yako kuondoa hewa baada ya kuvuta mpaka uwezo wako wa mwisho na kupuliza hewa nje kwa uwezo wako wote, na pia hupima kwa haraka gani unaweza kupumua
Peak flow
-
Ni kipimo kinachopima uwezo wako wa kutoa hewa nje ya mapafu
-
Vipimo hivi hufanyika kabla na baada ya kutumia dawa ili kuona utofauti na kama dawa zitakusaidia na vipimo hivo huitwa vipimo vya kupima uwezo ufanyaji kazi wa mapafu
Vipimo vya ziada ni kama
-
Picha ya mionzi ya kifua
-
Kipimo cha allergy kinachofanyika kwa kupima damu au kuweka allergy katika ngozi
-
Kipimo cha makohozi kwa ajili ya kuangalia chembe za esinophili
-
Kipimo cha kuamsha asthma kama mazoezi na baridi
Dawa
-
Inhaled corticosteroids.
-
Leukotriene modifiers.
-
Combination inhalers
-
Theophylline
Madawa ya kuzuia madhara ya pumu kwa haraka
-
Short-acting beta agonists
-
Ipratropium (Atrovent)
-
Oral and intravenous corticosteroids
Madaya ya kuzuia Mzio/allegy
-
Kama immunotherapy
-
Omalizumab
Matibabu ya nyumbani
Namna ya kuzuia kuamsha pumu ukiwa nyumbani
Kuna baadhi ya mambo ambayo yakifanywa yanaweza kuzuia mtu kuamka kwa pumu mara kwa mara au pumu kuwa kali zaidi, ingawa watu hutumia sana dawa kujikinga na pumu hizi mbinu hapa chini zinaweza kuwa msaada pia
Zuia viamsha pumu
-
Tumia air conditioner
-
Air conditioner huondoa hewa chafu ndani ya nyumba ambayo ina vumbi vumbi kutoka kwenye vinyesi vya wanyama, majani na magugu au magari yanayopita nje au viwanda. Air conditioner hupunguza unyevu kwenye hewa ndani ya nyumba pia. Kama huna air conditioner kwenye nyumba yako basi jaribu kufunga milango na madirisha ya nyumba yako msimu wa maua.
-
-
Toa vumbi maeneo ya kulala- Fanya usafi kwenye chumba chako mara kwa mara ili kutoa vumbi sehemu za uvunguni na kwenye kitanda, kung’uta godoro, mito na safisha paa kwa ufagio na kila sehemu ya nyumba yako. Safisha maeneo ya kapeti kwa kuliondoa au kupiga deki. Epuka kufagia ndani maana hutengeneza vumbi dogo na kukaa kwenye mashuka na kuta. Tumia maji kusafisha nyumba yako vema
-
Ishi maeneo yenye unyevu unaofaa- ni ngumu kufanya hili kama unaishi mazingira ambayo yana unyevu wa juu sana, lakini kama unaweza unaweza kuondoka kwenye mazingira hayo au kutumia mbinu zingine
-
Jikinge na vumbi na nywele za wanyama wa ndani- kama una mzio na manyoya ya wanyama au vumbi lao, mfano paka, kuku, mbwan.k hakikisha unakaa mbali navyo maana huwa na vumbi ambalo linaamsha pumu
-
Safisha nyumba mara kwa mara- safisha nyumba yako mara kwa mara na usiache kwa muda mrefu ili kuhakikisha vumbi limeondoka
-
Funika kinywa chako kama nje kuna baridi- kama pumu yako inaamshwa na baridi basi ni vema ukatumia mask kufunika mdomo na pua wakati ukiwa unatembea nje.
Tumia baadhi ya dawa asilia zinazofahamika kupunguza pumu kuamka
Baadhi ya dawa asilia zinazoweza kukinga pumu yako kuamka mara kwa mara ni kama
-
Kahawa, na vitamin aina ya choline
-
Dawa aina ya yunzi essence,micro2 na condycepts ambazo unaweza kuzipata kwa kuwasiliana na daktari kwa namba kwa hapo chiniya tovuti hii
Dawa aina ya yunzi hufanya kazi nyingi kama vile
-
Inaondoa mizio na aleji kwa wagonjwa wa pumu
-
Humkinga mtu kuamkwa kwa pumu
-
Inaondoa magonjwa ya pumu
-
Huondoa mizio aina yote, kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la mizio, kupata mafua ya mara kwa mara na kupiga chafya sana
-
Huongeza uhai wa ini na mapafu
-
Inazuia ukuaji wa seli za kansa
-
Inazuia na kuondoa uvimbe kwenye kizazi
-
Huleta hamu ya tendo la ndoa kwa kina mama
-
inaongeza uwiano wa homoni mwilini
-
huzuia hedhi inayoenda muda mrefu
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au bonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa, 2.12.2020