Pumu ya ngozi (eczema-atopic dermatitis)
​
Imeandikwa na daktari wa uly clinic
​
Ni hali ambayo hufanya ngozi kuwa nyekundu na kuwasha. Ni hali inayojitokeza sana kwa watoto lakini huweza kutokea kwenye umri wowote ule. Tatizo hili huwepo kwa maisha yote ya mtu ama kwa muda mrefu na huweza kuibuka kwenye muda flani na wakati mwingine dalili zinaweza zikapotea kabisa.
Tatizo hili linaweza kuambatana na pumu ya kifua na mafua yamara kwa mara(hay fever)
Hakuna tiba ponyaji iliyopatikana kwa ajili ya kutibu pumu ya ngozi. Lakini matibabu ya dalili na kujitunza kwa mtu huweza kupunguza dalili na kuzuia kuibuka ibuka kwa dalili.
Kwa mfano mwathirka anatakiwa kuzuia sabuni zenye pafyumu na vikereketa vya ngozi, kuzuia kutumia sabuni zenye madawa au mafuta na kufanya mambo yanayofanya ngozi iwe raini
Unatakiwa kumwona daktari wako endapo dalili unazopata zinakufanya usifanye kazi zako kama ipasavyo au zinakuzuia kulala.
​
Unataka kuwasiliana na daktari wa ngozi wa ulyclinic kupata tiba? Bonyeza hapa, au wasiliana na namba chini ya tovuti hii, huduma zinakufikia mahali ulipo.
​
Dalili, Visababishi,Vihatarishi, Madhara, Matibabu