top of page

Saratani ya Shingo ya Kizazi/ Seviksi

 

Shingo ya kizazi ni mlango wa kuingilia kwenye kizazi, sehemu hii ni sehemu ya chini kwenye mlango wa kuingilia ndani ya mfuko wa uzazi. Kama ilivyo kibuyu, sehemu nyembamba ambayo inaenda kukutana na mdomo wa kibuyu, hufananishwa kuwa  mfano mzuri wa shingo ya kizazi. Angalia kwenye picha kwa maelezo sehemu ilipo shingo ya kizazi.

 

Saratani ya shingo ya kizazi ni ya tatu  kutokea kwa wingi kwa wanawake Duniani na inaongoza katika kusababisha vifo.

 

Saratani hii imepungua huko Marekani kwa sababu ya vipimo vya awali vinavyofanywa kugundua mabadiliko ya kisaratani katika shingo ya kizazi katika hatua za awali sana pamoja na kugunduliwa na kutumika kwa chanjo ya kinga juu ya kirusi anayesababisha saratani hii.

 

Ingawa wagonjwa wa saratani hii wamepungua huko marekani bado ugonjwa huu unaongezeka katika nchi zinazoendelea ambapo upimaji wa awali wa kugundua saratani hii na matibabu bado ni changamoto.

 

Saratani ya shingo ya kizazi mara nyingi hukua taratibu. Kabla ya saratani hii kuonekana kwenye shingo ya kizazi kuna mabadiliko hutokea,mabadiliko hayo ni kuonekana kwa chembe zisizo za kawaida zilizofanyika katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya kwa kitaalamu huitwa dysplasia(chembe zinazotokea zinaitwa dysplastic cells).Chembe hizi zinaweza kutoweka kwa baadhi ya watu bila au pasipo matibabu.

 

Chembe hizi (dysplastic cell ) zisipotibiwa zinaweza kubadilika kuwa saratani baada ya miaka fulani kupita, inaweza kuchukua miaka mingi kwa chembe hizi kubadilika kuwa saratani

 

Dalili zipi za mtu mwenye saratani ya shingo ya kizazi?

 

Dalili za mtu mwenye saratani ya shingo ya kizazi huanza kujitokeza pale ambapo chembe hizi zinapo badilika tabia kuzaliana kwa kiasi kikubwa na kuleta madhara. Hivo awali kabisa saratani hii huwa haina dalili na ikiwa dalili zinaanza kuonekana huwa ni hizi/kati ya zifuatazo;

​

  • Maumivu makali ukeni wakati wa tendo la ndoa

  • Kutokwa na majimaji  ukeni yanayonuka 

  • Kutokwa na damu ukeni, baada au kabla ya damu ya mwezi

    • kwa mara ya kwanza mwanamke anaweza kutokwa na damu anapokuwa anajisafisha kwa mkono au anaposhiriki tendo la ndoa na baadae tatizo likiwa kubwa damu huweza kutoka bila hata ya kujisafisha au kushiriki tendo la ndoa na humaanisha hari ya mtu ni mbaya zidi

 

Visababishi, vihatarishi, vipimo na matibabu

​

ULY clinic inakushauri kufuata ushauri wa dakatari wako kwa tiba na uchunguzi kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya afya yako

​

Wasiliana na dakatari wa ULY clinic kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza hapa, au kuwasiliana kwa kutumia namba za simu chini ya tovuti hii.

saratani-ya-shingo-ya-kizazi-ulyclinic
bottom of page