top of page

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic

 

​

Zipi ni Dalili za saratani ya tezi dume?

 

Kutoka kwenye historia ya mgonjwa

 

Kwa sasa ugonjwa huu hutambuliwa kwa mtu asiye na dalili yoyote na kutambuliwa huko hutokana na kupima kemikali aina ya PSA mwilini inayotolewa na tezi dume na pia kutokana na uchunguzi unaofanyika kwa kupima tezi hii kwa njia ya DRE yaani kupimwa kwa kuwekewa ama kuingiziwa kidole kwenye njia ya haja kubwa na mtaalamu wa afya kutambua kama kuna mabadiliko yoyote. Na pia saratani ya tezi hii huweza kuonekana kwenye vinyama vinapotolewa kwa uchunguzi kwa mtu aliyevimba tezi dume

 

Dalili za awali

 

Watu wengi kabla ya ugunduzi wa kipimo cha PSA, walikua wanalalamika dalili kwenye njia ya mkojo kama kubakiza mkojo wakiwa wanakojoa ( urine retension) maumivu nyuma ya mgongo, na kukojoa damu. Dalili hizi kutokea haimaanishi una saratani hii moja kwa moja, bali inaweza kumaanisha magonjwa mengine pia. Kwa mfano mtu anayekojoa mara kwa mara, kushindwa kuzuia mkojo, na kupungua kwa wingi wa mkojo wakati wa haja ndogo  maranyingi hutokana na kuvimba kwa tezi dume

 

Dalili za ugonjwa kusambaa

 

Hutokana na kusambaa kwa ugonjwa huu sehemu zingine za mwili kwa njia ya damu au mitoki

 

  • Kupungua uzito

  • Kupungukiwa damu

  • Maumivu ya mifupa pamoja na au bila mifupa kuvunjika

  • Kupoteza hisia (mfumo wa fahamu kuharibiwa)

  • Maumivu miguuni na miguu kuvimba kutokana na kuzibwa njia ya mitoki(lymphatic)

  • Kupanda kwa urea mwilini (uremic symptoms) inaweza kutokea kutokana na kuziba mirija inayotoa mkojo kwenye kibofu na hivo kuletea mtu kuchanganyikiwa na

 

Dalili zinazoonekana kutokana na vipimo vya dakitari

 

Kipimo  hichi hakiwezi kutofautisha saratani na uvimbe wa kawaia wa tezi dume kwa hivyo kipimo cha kupima nyama (biopsy) hufanyika kuondoa utata huu

 

  • Kukonda kutokana na Saratani

  • Maumivu ya mifupa ikishikwa

  • Uvimbe miguuni au/pamoja na ugonjwa wa kutokwa damu kutokana na chembe mgando kuisha ama DVT

  • Mitoki kuvimba hasa maeneo ya nyonga

  • Kibofu kuwa kikubwa kwa sababu ya mkojo kuzuiwa ndani ya kibofu

 

Uchunguzi wa mfumo wa fahamu unaweza kuwa kama kupima uwezo wa mkundu kubana ( sphincter tone) unatakiwa ufanyike ili kugundua kama kuna mkandamizo kweye mishipa ya fahamu ya uti wa mgomgo kutokana na Saratani hii.

 

Uchunguzi kwenye njia ya haja kubwa DRE

 

Inategemea uzoefu wa mpimaji, na uchunguzi wa mara kwa mara wa tezi hii huweza kumfanya mtaalamu kutofautisha au kuweza kujua kama kuna uvimbe wa kawaida au usio wa kawaida

 

Vitu kama tezi kutokuwa na usawa na kubadilika kwa  umbo halisi (texture) ..kipimo hiki kinaweza kuofautisha magonjwa tofauti kama vile  vifuko vya mvilio wa maji katika tezi dume ama prostate cyst na hivo ni muhimu kuchukua vinyama ili kuweza kupima kama uvimbe huu ni wa kawaia au ni Saratani

 

Magonjwa gani yanaweza kufanana dalili na Saratani ya tezi dume?

 

  • Usaa kwenye tezi dume au maambukizi ya ghafla ya tezi dume

  • Maambukizi ya bakiteria kwenye tezi dume( bacterial prostatis)

  • Uvimbe wa kawada wa tezi dume ama BP

  • Maambukizi ya TB kwenye tezi dume (tuberculosis prostatis)

  • Maambukizi yasiyo ya bakiterial kwenye tezi dume (nonbacterial prostatis)

 

 

 

Imechapishwa 3/3/2014

Imeboreshwa 5/11/2018

bottom of page