Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
​
SARATANI YA TEZI DUME
Saratani ya tezi dume ni mojawapo ya saratani maarufu zinazowapata wanaume kwa wingi, kwa Waamerika na Waafrika pia. Mwafrika mmoja kati ya sita 1/5 atapata Saratani ya tezi dume, na mzungu mmoja kati ya sita 1/6 atapata saratani ya tezi dume maishani mwake (kutokana na tafiti). Kadiri ya umri unavyoongezeka na hatari ya kupata Saratani hii huongezeka pia. Ingawa hukua taratibu, maelfu ya wanaume hufa kila mwaka kutokana na Saratani hii na saratani hii ni ya pili miongoni mwa Saratani nyingi zinazosababisha vifo kwa wanaume kutokana na Saratani Duniani. Upataji wa Saratani hii unahusishwa na sababu za kibaologia na pia urithisaji ndani ya familia pia umeonekana, na hivyo vinasaba vinahusika katika hatari ya kupata Saratani hii
Saratani ya tezi dume maranyingi hugunduliwa kwa wanaume wasio na dalili yoyote. Kipimo cha kemikali iitwayo prosrtate specific antigeni (PSA) ambayo hutolewa na tezi hii au mabadiliko ya tezi dume (umbo ukubwa na tabia-hupimwa na mataalamu wa afya kwa kuingiziwa kidole kwenye haja kubwa) hupelekea kugundua mabadiliko yoyote katika tezi dume yanayoweza kuwa saratani
Elimu juu ya Saratani hii na vihatarishi ni muhimu katika kuleta uelewa wa tatizo hili na kuweza kujua kinga na matibabu yaliyopo kwa wanaume na jamii kwa ujumla.
​
Tezi dume imekaa chini ya kibofu na na imepitiwa na mrija upitishao mkojo kutoka kwenye kibofu(urethra) na imetengwa na sehemu ya haja kubwa kwa ukuta uitwao kwa kitaaramu denovillurious aponeurosis kama uonavyo kwenye picha hapo juu
Nini hutokea kwenye tezi hii hii?
Saratani ya tezi dume hutokea endapo idadi ya uzalishaji wa viini ama chembe hai za tezi hii inapita uwezo wa mwili kuharibu viini hiyo. Hivyo uvimbe unatokea kutokana na viini vya tezi hii kuongezekana. Tatizo hili hutokea endapo vinasaba vya mwili zimebadilika tabia yake au kutofanya kazi kama ipasavyo na huhusishwa sana na geni yenye jina la p53 ambayo huhusika katika kuvunja viini hai mwilini na kuzuia saratani
Saratani inayoongoza kwenye tezi dume ni aina ya adenocarcinoma (95%) na zinazofuata ni kama Saratani ya squmous cell
Jinsi Usambaaji wa Saratani hii unavyotokea
Saratani hii inaposambaa huanzia kwenye shingo ya kibofu na zingine kwenye mirija inayopitisha mbegu (ejaculatory duct) njia za usambaaji wa Saratani hii sehemu nyingine za mwili bado haijulikani vizuri
Saratani hii husambaa kwenye mifupa bila hata kuonyesha dalili ya kuvimba mitoki na kwa sasa njia ya kusambaa kwa mirija inayopitisha mitoki na mirija ya damu kwenda kwenye uti wa mgongo. Kusambaa kwenye mifupa mapafu ini na tezi ya adrenal iliyopo juu ya figo imeonyeshwa kutokea kwa njia ya kujipandikiza.
Saratani hii hukua marambili kwa kipindi cha miaka 4 kama inavyooneshwa kwenye tafiti na Saratani chache sana zinazotokea kwenye tezi hii huweza kukua mara mbili nani ya miaka miwili (2)
Imechapishwa 3/3/2014
Imepitiwa 5/11/2018