Epidemiolojia ya saratani ya tezi dume
​
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
​
Kimataifa Saratani ya tezi dume inaonekana kwa wingi kwenye Bara la Amerika kaskazini , Australia na na Kaskazini na Ulaya ya kati na inaonekana kwa kiasi kidogo zaidi kusini mashariki na kusini ya kati huko bara Asia
Katika bara la America inaonekana kwamba mzungu 1 kati ya wazungu 6 na mwafrika 1 kati ya Waafrika 5 wanapata Saratani hii maishani mwao
Saratani ya tezi dume ni marachache kugundulika kwa wanaume walio chini ya miaka 40 na pia hutokea marachache kwa wanaume wenye umri chini ya miaka 50. Saratani hii pia imeonekana kwa watu waliokwisha kufa kwa magonjwa mengine ila walipofanyiwa uchunguzi ulionesha kwamba ugonjwa huu ulikuwepo kwa watu hao bila dalili yoyote. hivyo watu wachache huonesha dalili za ugonjwa huu. Asilimia zaidi ya 80% ya wanaume walio na miaka 80 wanaweza kuwa na Saratani hii, katika tafiti zilizofanyika sigara huambatana na ugonjwa huu ukilinganisha na wale ambao hawakuwahi kuvuta sigara maishani mwao kwa mtu aliyevuta sigara nyingi maishani mwake ilionekana kuhusiana kupata Saratani hii kuliko wale waliotumia kwa kiasi kidogo
Tofauti za kirangi
Tafiti pia zinaonyesha kwamba Waafrika waishio amerika wana hatari zaidi ya kupata Saratani hii kuliko wazungu, Wahispania wana hatari sawasawa ya kupata Saratani hii ukilinganisha na wazungu. Waasia wenye Asili ya Asia wana hatari ndogo kupata Saratani hii
Nini mwisho wa saratani hii?
Vipimo vya msingi vinavyoonesha maendeleo ya Saratani hii ni gleason score grade, ukubwa wa Saratani na kama Saratani imepasua kuta ya tezi
Watu waliogunduliwa na Saratani hii mapema na kutolewa tezi hii, katika miaka 15 asilimia saba tu wanaweza kufa kutokana na Saratani hii. Hii inamaanisha ukigunduliwa mapema, umri wa kuishi bila madhara ya Saratani hii huongezeka
Wanaume wenye matatizo kwenye vinasaba kama mabadiliko kwenye kinasaba p53 wanahatari ya kuishi maisha mafupi kutokana na maendeleo ya kasi ya ugonjwa huu
Saratani ya tezi dume ni ya pili miongoni mwa Saratani zinazoongoza kwa kusababisa vifo kwa wanaume duniani
​
Imeboreshwa 5/11/2018