Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
Dalili za ugonjwa wa seliak
Dalili na viashiria vya ugonjwa wa seliaki ni pamoja na
-
Kuharisha
-
Uchovu
-
Kupoteza uzito
-
Tumbo kujaa gesi na kubeuka
-
Kichefuchefu
-
Kutapika
-
Konstipeshen
Dalili zingine ambazo zinaweza kuonekana zisizohusiana na mfumo wa chakula ni pamoja na;
-
Upungufu wa damu kutokana na kukosa madini chuma
-
Kupoteza kwa uimara wa mifupa(osteoporosisi)
-
Mifupa kuwa laini(osteomalasia)
-
Kkuwashwa Ngozi
-
Kutokwa na malengelenge na harara kwenye Ngozi (demataitiz hepatifomiz)
-
Vidonda mdomoni
-
Maumivu ya kichwa na uchovu
-
Magonjwa ya mfumo wa neva
-
Maumivu ya maungio ya mwili
-
Kupungua kwa utendaji kazi wa Bandama
Dalili zingine zinazoweza kuwapata Watoto ni
-
Kuvimba tumbo
-
Tatizo sugu la kuharisha
-
Kubeuka gesi
-
Kinyesi cha rangi mpauko na kinachonuka kama kimeoza
-
Kutokua vema
-
Kuharibika kwa kichwa cha meno
-
Upungufu wa damu
-
Kuwa msumbufu
-
Kuwa mbilikimo
-
Kuchelewa kubarehe
-
Dalili za mfumo wa neva ikiwa pamoja na ugonjwa wa kutotulia
ULY clini inakukumbusha kwuasiliana na daktari wako wakati wowote kabla ya kuchukua hatua yoyote kulingana na ulichokisoma hapa.
Imeboreshwa 12.03.2020