Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;
Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Huduma ya kwanza kwa mwenye shambulio la moyo (heart attack)
​
Shambulio la moyo kwa jina jingine mshituko wa moyo ni moja ya ugonjwa wa moyo unaotishia uhai wa mtu Tanzania na Duniani kote. Endapo mtu aliyeshambuliwa hajapata matibabu ya haraka huweza poteza maisha mara moja
​
Kama unafikili kuw amtu ana au alipata shamulio la moyo piga simu mara moja kwa namba 112 na kisha muweke kwenye pozi la uhuru la kukaa
​
Dalili za shambulio la moyo huwa pamoja na
-
Maumivu ya kifua- Maumivu huwa katikati ya kifua au upande wa kushoto na huhisiwa kama hisia za mgandamizo, kubana au kubinywa
-
Maumivu sehemu zingine za mwili- yanaweza kuhisiwa endapo maumivu ya moyo yanatembea kuelekea sehemu zingine kama kutoka kifuani kwenda kwenye mikono , taya, mgongoni au tumboni
-
Mkalishe mgonjwa chini vizuri
Kama anafahamu, mpe tumaini na mwombe anywe atafune taratibu miligramu 300 ya dawa aspirin. Ikiwa haruhusiwi kutumia aspirini mfano akiwa na mzio na dawa hii au akiwa chini ya umri wa miaka 16
​
Kama mgonjwa ana dawa zozote za tatizo la Angina mfano dawa ya kupuliza au vidonge msaidie aweze kunywa.
Hakikisha unakagua ishara muhimu za uhai wake,( upumuaji, midundo ya mishipa ya damu na moyo) mpaka afike hospitali
​
Kama hali ikiendelea kuwa mbaya na kupoteza fahamu, fungua njia ya hewa, tizama kama anapumua vema na uanze kufanya CPR ili kuokoa maisha yake
Pga simu namba 112 kwa msaada Zaidi
​
​
Imeboreshwa 14.08.2020