top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

 

Kushuka kwa shinikizo la damu

​

Utangulizi

​

Kushuka kwa shinikizo la damu ama Shinikizo la la damu la chini kupita kiasi huweza kuonekana ni hali nzuri kwa baadhi ya watu, lakini ukweli ni kwamba kwa watu wengi hupelekea wapate kizunguzungu na kuzimia. Kama presha ya damu ikishuka kwa kiwango kikubwa mtu anaweza poteza maisha.

Ili kusema kwamba presha ya mtu isemekane imeshuka kupita kiasi huwa hivi, namba ya juu huwa chini ya 90 na ile ya chini kuwa chini ya 60.

Visababishi vya shinikizo la chini la damu huweza kuwa vya tofauti kama vile kuishiwa maji mwilini, au magonjwa. Ni muhimu kujua kisababishi ili kupata matibabu sahihi

 

Dalili

​

Dalili za shinikizo la damu la chini huweza kumaanisha kuna tatizo la kutiliwa umaanani endapo hali hii inaambatana na

​

Shinikizo la damu la chini kupita kiasi huweza kusababisha mtu kupata mshituko wa damu au shock. Hali hii huweza kumsababisha mtu apoteze maisha endapo hata pata matibabu ya haraka.

​

Dalili za mtu mwenye mshituko wa damu ni

  • Kuchanganyikiwa, hasa kwa watu wazima

  • Kuhisi baridi, ngozi kupauka rangi yake(kuwa nyeupe)

  • Kupumua kwa haraka haraka na juu juu

  • Midundo ya mapigo ya mishipa ya damu kuongezeka na kutokuwa na nguvu

​

Endapo unapata dalili zinazoashiria kuw auna mshituko wa damu inakupasa kuonana na daktari haraka. unaweza wasiliana nasi kwa ushauri. Endapo pia shinikizo lako la dmau hushuka mara kwa mara, inakupasa kuonana na daktari.

 

Visababishi

​

Shinikizo la damu ni kipimo cha kasi na mzunguko wa damu katika mishipa ya artery wakati wa midundo ya moyo. Shinikizo la damu limegawanyika kwenye sehemu mbili, shinikizo la systolic na shinikizo la diastolic

 

Shinikizo la sistolic hutokea pale moyo unapokuwa unadunda, na lile la diastolic hutokea moyo unapomaliza kudunda. Visababishi vya kupanda kwa shinikizo la dmau huweza kuwa pamoja na sababu zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu la juu au ala chini. Kwa sasa inafahamika kuwa shinikizo la damu la kawaida hutakiw akuwa chini ya 120/80mmHg.

 

Shinikizo la damu hubadilika mara nyingi kwa siku, ikitegemea shughuli mtu anazofanya au kama amekaa na kutembea, akipata mshituko au akiwa na furaha au akiwa anakula au kunywa dawa aina Fulani. Hata hivyo shinikizo la damu huwa la chini kupita wakati wote wakati wa usiku mtu akiwa amelala na hupanda Zaidi mtu akisimama au kuamka ghafla

Mtu anaposimama au kuamka ghafla kutoka kwenye pozi la kulala, husabaisha shinikizo la damu kushuka na kupata dalili za kizunguzungu au kuzimia, hii ni kwa sababu ubongo wako unakosa damu ukisimama ghafla.

 

Hali zinazoweza kusababisha shinikizo la dmau kushuka ni pamoja na

​

Ujauzito

​

Mishipa ya damu hutanuka wakati wa ujauzito, mishipa ya damu ikitanuka shinikizo la damu hushuka. Hii ni sawa na endapo maji yatatembea katika bomba kubwa yatakuwa na msukumo mdogo, vilevile yakipitishwa kwenye bomba jembamba yatakuwa na msukumo mdogo na kuruka mbali. Hali hii ni sawa na damu inayotembea kwenye mishipa. Ujauzito unapoisha shinikizo la damu hujirudia kwenye hali yake ya kawaida

​

Matatizo ya moyo

​

Matatizo ya moyo yanayoweza kusababisha tatizo la kushuka kwa shinikizo la damu ni pamoja na moyo kudunda taratibu sana, magonjwa ya milango ya moyo, kushikwa kwa moyo na kufeli kwa moyo

 

Matatizo ya kihomoni

​

Magonjwa ya tezi shingo mfano, ugonjwa wa parathyroid, kuzalishwa kwa uchache kwa homoni za tezi ya adrenal, sukari kuwa chini mwilini na ugonjwa wa kisukari huweza kuleta shinikizo la chini la damu.

​

Kuishiwa maji mwilini

​

Matatizo yoyote yanayopelekea kusababisha uishiwe maji mwilini husababisha kwa shinikizo la damu kushuka. Mfano ni pipa likiwa na maji mengi ukaweka mpira ili kuyatoa, mwanzoni yatatoka kwa kasi na kuruka mbali lakini yakifika mwisho yatapungua na kuruka karibu, hii ni sawa na shinikizo la dmau, endapo maji kwenye damu yamepungua basi mtu huyu hupata shinikizo la dmau la chini. Magonjwa na hali zinazoweza kusababisha shinikizo la dmau la chini huwa pamoja na, homa, kutapika, kuharisha sana, kutumia madawa ya kupunguza maji(kuongeza kukojoa)  na kufanya mazoezi makali sana

​

Kutokwa na damu

​

Kutokwa na dmau kunaweza sababishwa na kujikata, kutokwa damu haimaanishai ni lazima uione damu inamwagika kwa nje, baadhi ya sababu husababisha damu kuvilia ndani ya mwili, mfano kupasuka kwa ini, bandama au mimba ilitotungiwa nje ya kizazi. Hata hivyo huambatana na dalili zingine za tumbo kuuma. Kutokwa na damu nyingi kutokana na kujikata au kupata ajali husababisha kupoteza maji na chembe za damu. Matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.

​

Maambukizi makali

​

Maambukizi makali au kwa jina la kitaalamu septicemia ni maambukizi yanayoingia kwenye mzunguko wa damu. Huweza kuwa maambukizi ya bakteria au virusi, maambukizi haya husabaisha kushuka kwa shinikizo la damu

​

Aleji kali/mzio mkali

​

Mizio au aleje hweza kusababishwa na mambo mbalimbali mfano poleni za maua, vumbi, au kula chakula aina Fulani. Pia baadhi ya dawa zinaweza kusababisha aleji kwa mtu zikiwepo kama antibiotics jamii ya penicillin, sumu ya wadudu warukao na nyoka pia huweza kuleta aleji. Mtu akipata aleji kali huweza kupata dalili za kushindwa kupumua, kutoa miruzi kwenye nia ya hewa, kuwashwa ngozi, kuvimba koo na kushuka kusiko kwa kawaida kwa shinikizo la damu.

 

Madawa yanayoweza kusababisha shinikizo la damu la chini ni pamoja na;

​

  • Madawa ya kuongeza kukojoa( au kupoteza maji) mfano frusemide au Lasix, hydrochlorothiaxide

  • Dawa aina ya alpha blockers kama prazosin

  • Dawa aina ya beta blocker kama atenolol, propranolol

  • Dawa kwa matibabu ya tatizo la parkinsonism mfano pramipexole na levodopa

  • Dawa za kuzuisa huzunika mfano doxepin na imipramine

  • Dawa za kutibu matatizo ya kushindwa kusimamisha uume mfano sildenafir, tadalafil

​

Aina za shinikizo la chini la damu

​

Shinikizo la damu la chini limegawanyika kulingana na visababishi na vitu mambo mengine

​

Shinikizo la damu la chini wakati wa  kusimama

​

Hutokea endapo mtu amekaa ghafla au amesimama ghafla kutoka kwenye pozi la kulala.

Kwa kawaida Gravity huvuta damu ikae kwenye mishipa ya damu ya miguuni  wakati unasimama. Kwa asili mwili   huongeza mapigo ya moyo na mishipa ya damu husinyaa ili kuongeza shinikizo la damu kwenye mishipa na hivyo damu iweze fika kwenye ubongo.  Watu wanao pata shinikizo la chini la damu wakati wa kusimama, njia hii ya asili ya kupandisha shinikizo la damu hufeli na shinikizo la damu hushuka chini na kupelekea kupata dalili zote za shinikizo la damu la chini.

Shinikizo la damu kutokana na kubadili pozi huweza kusabaishwa na mambo mablimbali ikiwa pamoja na kuishiwa maji mwilini, kulala kwa mda mrefu, ujauzito, kisukari, kuungua, joto kali, kuvimba kwa mishipa ya vein na magonjwa Fulani ya mishipa ya fahamu.

​

Baadhi ya dawa zinazoweza kusabaisha shinikizo la damu la chini wakati wa kusimama ni pamoja na dawa jamii ya diuretics, beta blockers, calcium channel blockers na angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors pia na antidepressants na dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa  Parkinson's na kushindwa kusimamisha uume

Tatizo hili hutokea sana kwa wazee, lakini pia hudhuru vijana wadogo ambao wanasimama kwa ghafla kutoka kwenye pozi la kukaa wakiwa wamekunja nne au kuchuchumaa kwa mda mrefu.

Kwa baadhi ya wakati shinikizo la damu la chini la aina hii huweza kuchelewa kwa dakika 5 hadi 10 baada yamtu kusimama kutoka kwenye pozi la kulala

 

Shinikizo la damu la chini baada ya kula chakula

​

Hutokea mara tu baada ya mtu kumaliza kula chakula na hudhuru wazee. Mtu anapokula chakula damu huwa inaelekea sana tumboni na kwenye utumbo kwa kusudi la kuchukua chakula kilichomeng’enywa. Kwa kawaida mwili husinyaza baadhi ya mishipa na kuongeza mapigo ya moyo ili kuhakikisha mwili unabaki na shinikizo la damu la kawaida, bahati mbaya kwa baadhi ya watu kitendo hiki hufeli kufanyika na kusababisha shinikizo la damu la chini. Matokeo yake ni mtu kupata dalili zote za shinikizo la damu la chini

​

Shinikizo la damu la chini hudhuru mara nyingi watu wenye shinikizo la juu la dmau na wale wanaougua magonjwa ya mfumo wa fahamu mfano ugonjwa wa Parkinson's

Ili kujikinga na madhara haya, kula chakula chenye wanga kiasi na punguza dozi za dawa za kushusha presha.

​

Shinikizo la damu la chini kutokana na kufeli kwa mfumo wa fahamu wa ubongo

Hili tatizo hutokea kwa vijana wadogo wanaosimama kwa mda mrefu na husababishwa kwa kufeli kwa mawasiliano kati ya moyyo na ubongo. Mtu huanza kupata dalili za shinikizo la dmau la chini kabla ya kuanguka.

 

Shinikizo la damu la chini kwa sababu ya kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu  inayoongoza matendo yasiyo ya hiari mfano mapigo ya moyo, kupumua, kubeng’enya chakula na shinikizo la damu. Uharibifu huu huweza kusababishwa na tatizo la shy-Drager syndrome

​

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada na ushauri zaidi kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote inayodhuru afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kupiga simu au kubonyeza "Pata Tiba" chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa mara ya mwisho, 03.07.2020

​

Rejea za mada

​

  1. Hypotension. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/book/export/html/4880. Imechukuliwa 16.04.2020

  2. Low blood pressure. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/AboutHighBloodPressure/Low-Blood-Pressure_UCM_301785_Article.jsp. Imechukuliwa 16.04.2020

  3. Kaufman H, et al. Mechanisms, causes and evaluation of orthostatic hypotension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 16.04.2020

  4. Understanding blood pressure readings. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/AboutHighBloodPressure/Understanding-Blood-Pressure-Readings_UCM_301764_Article.jsp. Imechukuliwa 16.04.2020

  5. Kaplan NM, et al. Ambulatory and home blood pressure monitoring and white coat hypertension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 16.04.2020

  6. Kaufman H, et al. Treatment of orthostatic and postprandial hypotension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 16.04.2020

​

dalili
utangulizi
visababishi
Aina

Sehemu hii utasoma kuhusu

Utangulizi

Dalili

Visabaishi

Aina

Vihatarishi

Vipimo

Matibabu

Matibabu ya nyumbani

bottom of page