top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

10 Juni 2020 14:54:00

Malengo ya kushusha shinikizo la damu la juu
Malengo ya kushusha shinikizo la damu la juu

Malengo ya kushusha shinikizo la damu la juu

Unapokuwa unatibiwa au kutibu mgonjwa mwenye shinikizo la damu, ni vema ukafahamu ni malengo gani unatakiwa kufikia na kwa kipindi gani. Maoni ya malengo ya kushusha shinikizo la damu la juu kwa kutumia dawa yaliyoandikwa hapa yanatokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa.

  • Kwa watu wenye umri Zaidi ya miaka 60, endapo presha yao ya SBP ni juu ya 149 na ile ya DBP ni juu ya 89, malengo ya matibabu ni kushusha shinikizo la damu la SBP kuwa chini ya 150 na DBP liwe chini ya 90

  • Kwa watu wenye umri chini ya miaka 60, anzisha matibabu endapo presha yao ya SBP ni juu ya 139 na ile ya DBP ni juu ya 89, malengo ya matibabu ni kushusha shinikizo la damu la SBP kuwa chini ya 140 na DBP liwe chini ya 90

  • Kwa watu wenye umri kati ya miaka 18 na chini ya 70, na ikiwa wana magonjwa sugu ya figo(CKD) anzisha matibabu endapo presha yao ya SBP ni juu ya 139 na ile ya DBP ni juu ya 89, malengo ya matibabu ni kushusha shinikizo la damu la SBP kuwa chini ya 140 na DBP liwe chini ya 90. Matibabu lazima yahusishe dawa za angiotensini konventing enzaimu Inhibita au angiotensin risepta bloka sababu tu ni kuboresha na kuleta matokeo mazuri ya utendaji kazi wa figo.

  • Kwa wagonjwa wa kisukari wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendeea, endapo presha yao ya SBP ni zaidi ya 139 na ile ya DBP ni zaidi ya 89, malengo ya matibabu ni kushusha shinikizo la damu la SBP ni kuwa chini ya 150 na DBP liwe chini ya 90

  • Kwa watu wote wenye kisukari na shinikizo la juu la damu, matibabu dawa yanatakiwa kuhusisha dawa jamii ya thayazaidi na kalisiamu chaneli bloka.

Kumbuka

Malengo ya matibabu ya shinikizo la juu la damu ni kulishusha chini ya kiwango kama kinavyoonekana kwenye malengo. Kama malengo yasipofikiwa ndani ya mwezi wa matibabu, dozi ya dawa ya awali itatakiwa kuongezwa au kuongeza dawa ya pili kutoka kwenye dawa pendekezwa jamii ya (thayazaidi dyuretiki, kalisimau chaneli bloka, ACEI au ARB)


Endelea kupima presha ya mgonjwa mpaka malengo yatakapofikiwa, unaweza ongeza dawa ya tatu endapo itahitajika ikiwa tu umeshaongeza dozi ya dawa za awali kwa kiwango kinachoruhusiwa. Usitumie dawa jamii ya ARB na ACE kwa pamoja. Endapo malengo hayajafikiwa licha ya kutumia dawa kutoka kwenye kundi hili la ACE au ARB, tumia dawa kundi jingine badala ya kutumia makundi haya mawili kwa pamoja.


Endapo mwili wa mgonjwa hausikii dawa au mgonjwa amepata madhara ya shinikizo la damu, mpeleke mgonjwa kwa mbozezi wa kutibu shinikizo la damu.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 10:42:42

ULY Clinic inakushauri siku zote usichukue hatua yoyote ile inayoathiri afya yako bila kuwasiliana na daktari wako. 

Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kutumia namba za simu chini ya tovuti hii kwa elimu suhauri na Tiba

Rejea za mada hii,

​

  1. Beckett  NS, Peters  R, Fletcher  AE,  et al; HYVET Study Group.  Treatment of hypertension in patients 80 years of age or older.  N Engl J Med. 2008;358(18):1887-1898.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  2. SHEP Cooperative Research Group.  Prevention of stroke by antihypertensive drug treatment in older persons with isolated systolic hypertension: final results of the Systolic Hypertension in the Elderly Program (SHEP).  JAMA. 1991;265(24):3255-3264. ArticlePubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  3. Institute of Medicine.  Clinical Practice Guidelines We Can Trust. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Clinical-Practice-Guidelines-We-Can-Trust.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020

  4. Staessen  JA, Fagard  R, Thijs  L,  et al; The Systolic Hypertension in Europe (Syst-Eur) Trial Investigators.  Randomised double-blind comparison of placebo and active treatment for older patients with isolated systolic hypertension.  Lancet. 1997;350(9080):757-764.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  5. Hsu  CC, Sandford  BA.  The Delphi technique: making sense of consensus.  Pract Assess Res Eval. 2007;12(10). http://pareonline.net/pdf/v12n10.pdf. Accessed October 28, 2013.Google Scholar. Imechukuliwa 09.06.2020

  6. Institute of Medicine.  Finding What Works in Health Care: Standards for Systematic Reviews. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Finding-What-Works-in-Health-Care-Standards-for-systematic-Reviews.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020

  7. https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-in-adults-beyond-the-basics?topicRef=4415&source=see_link. Imechukuliwa 10.06.2020

  8. https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-diet-and-weight-beyond-the-basics.Imechukuliwa 10.06.2020

  9. Hypertension. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/1791497. Imechukuliwa 11.06.2020

  10. Dash Diet- 365 Days of Low Salt, Dash Diet Recipes For Lower Cholesterol, Lower Blood Pressure and Fat Loss Without Medication ( PDFDrive.com )

bottom of page