Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Charles W, MD
10 Juni 2020 12:55:10
Elimu kwa mgonjwa
Shinikizo la juu la damu endapo lisipotibiwa kisahihi huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile kiharusi, moyo kufeli, mshituko wa moyo na kifo. Katika matibabu ya shinikizo la juu la damu, elimu kwa mgonjwa ni jambo la kwanza na la msingi kufanyika. Endapo mgonjwa atapata elimu ya namna ya kudhibiti shinikizo la damu kwa njia zingine mbali na dawa, mfano kufanya mazoezi na kuzingatia ushauri wa matumizi ya chakula kutoka kwa mtaalamu wa lishe itamsaidia kudhibiti shinikizo hilo na hatimaye moyo na mishipa ya damu kutopata madhara yanayotokana na tatizo hili kwa muda mrefu.
Ni nini cha kufanya ili kudhibiti shinikizo la damu pasipo dawa?
Punguza matumizi ya chumvi
Chumvi huwa na tabia ya kutunza maji mwilini, ukipunguza kiasi cha chumvi unayotumia kwenye chakula unapunguza kiasi cha maji yanayofyonzwa na kukaa katika msihipa ya damu. Kwa kufanya hivi kiwango cha maji kwenye damu hupungua hivyo moyo hautafanya kazi kubwa ya kusukuma kiwango kikubwa cha damu. Vyakula vyenye chumvi kwa wingi ni kama vile vya kusindikwa, vyakula vya migahawani.
Mwili wa binadamu unahitaji kiwango kidogo tu cha chumvi, miligramu 2400 kwa siku zinahitajika kwa ajili ya afya ya binadamu. Vyakula vingi vinavyopikwa migahawani na nyumbani huwa na Zaidi ya miligramu 3000. Mtu mwenye shinikizo la juu la damu akipunguza kiwango cha chumvi kufikia miligramu 1500mg kwa siku kitamsaidia kupunguza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa.
Soma Zaidi kuhusu Makala ya kiwango cha chumvi sehemu nyingine kwenye makala za ulyclinic
Punguza kiwango cha pombe unachokunywa
Kupunguza kiasi cha pombe unachotumia kwa siku kina mchango mkubwa katika kupunguza shinikizo la damu. Watu wanaotumia kiwango kikubwa cha pombe kwa siku wana hatari ya kupata shinikizo la damu kuliko wale ambao hawatumii pombe kabisa. Watu wanaotumia pombe kwa kupindukia kwa siku mfano wanaokunywa bia tano hadi sita ndani ya saa moja wana hatari kubwa Zaidi kuliko wale ambao wanakunywa kinywaji kimoja kwa siku.
Soma Zaidi kuhusu kiwango cha pombe kinachoshauriwa kiafya kwa kubonyeza hapa.
Kula vyakula vyenye matunda na mbogamboga kwa wingi
Kula vyakula vya matunda na mboga kwa wingi husaidia kupunguza shinikizo la damu, na pia husaidia kukukinga kupata shinikizo la juu la damu, si lazima uwe vegetariani, tumia Mbinu za DASH zilizoandikwa kwenye tovuti hii kwa elimu zaidi
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi
Vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi hupunguza shinikizo la damu. Unashauriwa kula gramu 20 hadi 35 za nyuzinyuzi kutoka kwenye chakula kwa siku. Vyakula vingi vya mbegu zisizokobolewa ni chanzo kuzuri cha nyuzinyuzi zinazotakiwa kwa afya ya binadamu. Taarifa Zaidi zoma kwenye Makala za vyakula vya nyuzinyuzi kwenye tovuti hii.
Kula samaki kwa wingi
Kula samaki kwa wingi pamoja na mazoezi husaidia kupunguza shinikizo la damu
Tumia mpango wa MSL
Fuata ushauri wa MSL unaopunguza shinikizo la damu pasipo kuumia dawa. Mlo wa MSL huzingatia taarifa zilizoandikwa kwenye Makala hii hapo juu, MSL ni mlo wenye matunda, mboga za majani kwa wingi, vyakula visivyo na mafuta na vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi. Wagonjwa wanaofuata mlo wa MSL hupunguza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa kwamba hawahitaji kutumia dawa kupunguza shinikizo hilo.
Mazoezi
Fanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa dakika 30 mfululizo katika kila zoezi, soma Zaidi sehemu ya mazoezi na shinikizo la damu.
Punguza uzito
Kuwa na uzito mkubwa inakuweka hatarini kupata shinikizo la juu la damu, kisukari na magonjwa ya moyo. Soma Zaidi kuhusu uzito, uzito mkubwa kupita kiasi na uzito unaoshauriwa kiafya kwenye Makala ya inayohusu BMI ndani ya tovuti hii.
Ili kupunguza uzito unatakiwa kula vyakula vya wanga kwa kiasi kidogo na kufanya mazoezi Zaidi. Kuna njia zingine pia za kupunguza uzito, zisome katika Makala ya mazoezi ya kupunguza uzito ndani ya tovuti hii.
Jiepushe kunywa dawa zinazoongeza shinikizo la damu
Dawa jamii ya NSAIDS kama vile Ibuprofen, naproxen n.k, vidonge vya uzazi wa mpango, Dawa za kuchangamsha mwili kama zile za kuzibua pua, kupunguza uzito na madawa ya kulevya pia huongeza shinikizo la damu. Kama ukinywa dawa hizi mara kwa mara, mwili wako unankuwa kwenye hatari kubwa ya kuongeza shinikizo la damu.
Kamashinikizo limeendelea kuwa kubwa licha ya kuzingatia yote ufanyaje?
Kama shinikizo limeendelea kuwa kubwa kupita kiasi, utashauriwa na daktari waki kuanza matibabu ya dawa. Soma Zaidi kuhusu dawa za kutibu shinikizo la damu la juu kwenye makala ndani ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 11:10:45
ULY Clinic inakushauri siku zote usichukue hatua yoyote ile inayoathiri afya yako bila kuwasiliana na daktari wako.
Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kutumia namba za simu chini ya tovuti hii kwa elimu suhauri na Tiba
Rejea za mada hii,
​
-
Beckett NS, Peters R, Fletcher AE, et al; HYVET Study Group. Treatment of hypertension in patients 80 years of age or older. N Engl J Med. 2008;358(18):1887-1898.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
SHEP Cooperative Research Group. Prevention of stroke by antihypertensive drug treatment in older persons with isolated systolic hypertension: final results of the Systolic Hypertension in the Elderly Program (SHEP). JAMA. 1991;265(24):3255-3264. ArticlePubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Institute of Medicine. Clinical Practice Guidelines We Can Trust. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Clinical-Practice-Guidelines-We-Can-Trust.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Staessen JA, Fagard R, Thijs L, et al; The Systolic Hypertension in Europe (Syst-Eur) Trial Investigators. Randomised double-blind comparison of placebo and active treatment for older patients with isolated systolic hypertension. Lancet. 1997;350(9080):757-764.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Hsu CC, Sandford BA. The Delphi technique: making sense of consensus. Pract Assess Res Eval. 2007;12(10). http://pareonline.net/pdf/v12n10.pdf. Accessed October 28, 2013.Google Scholar. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Institute of Medicine. Finding What Works in Health Care: Standards for Systematic Reviews. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Finding-What-Works-in-Health-Care-Standards-for-systematic-Reviews.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020
-
https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-in-adults-beyond-the-basics?topicRef=4415&source=see_link. Imechukuliwa 10.06.2020
-
https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-diet-and-weight-beyond-the-basics.Imechukuliwa 10.06.2020
-
Hypertension. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/1791497. Imechukuliwa 11.06.2020
-
Dash Diet- 365 Days of Low Salt, Dash Diet Recipes For Lower Cholesterol, Lower Blood Pressure and Fat Loss Without Medication ( PDFDrive.com )