top of page
sickle cell.jpg

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Sickle cell(SCD)- Seli mundu

​

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Utangulizi

​

Sickle cell ni nini?

​

Ni ugonjwa wa kurithi ambao huonekana kwa wingi katika nchi za Afrika magharibi India na visiwa vya mediterania, ugonjwa huu umehusianishwa sana na malaria katika maeneo hayo. Maelezo ya kutokea kwa ugonjwa huu ni kwamba kutokea kwa malaria kumesababisha mwili kujiundia njia za ulinzi dhidi ya maambukizi ya vimelea vya malaria, ulinzi huo hufanyika kwa mwili kubadili tabia ya umbo la chembe nyekundu za damu, mtu anapopata maambukizi chembe nyekundu huchukua umbo la mwonekano wa mundu, ndio maana watu wanaobeba vinasaba/ genes vya tatizo la sickle cell huwa  hawaugui malaria kirahisi.

 

Hata hivyo  watu wanaoumwa ugonjwa wa sickle cell wapo hatarini kupoteza maisha endapo mabadiliko ya chembe nyekundu za damu yatatokea na kuleta tatizo la chembe hizi kushikamana na kuharibiwa katika bandama au mishipa ya damu.

​

Kutokana na tafiti za shirika la centre for disease control and prevention -CDC zinaonyesha kwamba

​

  • Ugonjwa wa Sickle cell  ni ugonjwa wa damu wa kurithi unaotokea sana kuliko magonjwa mengine ya kurithi huko USA

  • Zaidi ya watu 70,000 huko USA wana ugonjwa huu

  • Ugonjwa huu unatokea kwa mtu mmoja kati ya watu 500 ya wa Afrika waishio Bara la Amerika

  • Asilimia nane ya waamerika wamebeba vinasaba vya ugonjwa huu

  • Watu milioni 2 wana vinasaba za ugonjwa huo

  • Na mtu mmoja kati ya 12 ya wa Afrika waishio amerika wana vinasaba za ugonjwa huo

  • Asilimia 5 ya watu duniani wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa seli mundu

  • Ugonjwa huu huambatana na kusababisha vifo kwa watoto wadogo walio na tatizo hili  kwa asilimia 50 hadi 90

​

Nani hupata ugonjwa wa seli mundu?

 

Mtoto yetote aliyezaliwa na wazazi wawili wenye vinasaba vya kubeba ugonjwa wa seli mundu huweza kusababisha mtoto akazaliwana ugonjwa huu wa seli mundu. Kwa kawaida wagonjwa wanaozaliwa na seli mundu, wazazi wao huwa hawana dalili zozote zile lakini mtoto anayezaliwa hupata tatizo hili. Hii ni kwa sababu wazazi hawa kila mmoja huwa amebeba vinasaba vya ugonjwa, kuungana kwa vinasaba kutoka kwa mama na baba hutengeneza mtoto mwenye ugonjwa wa seli mundu. Ni muhimu sana kwa wazazi haswa wanaoishi maeneo yenye maambukizi ya malaria kwa wingi kupima kama wanavinasaba au la kabla ya kuamua kuoana au kuwa na mtoto.

 

Dalili za seli mundu

 

Ugonjwa wa seli mundu husababisha ishara mbalimbali na madhara mwilini ikiwa pamoja na kuongezeka kwa hatari ya kupata maambukizi na kiharusi. Wagonjwa wenye tatizo la seli mundu huweza kupata uharibifu kwenye ogani mbalimbali mwilini, baadhi ya ogani zinazoathiriwa sana ni mapafu, figo na maungio ya mwili.Hata hivyo  wagonjwa hawa wanaweza kupata madhaifu ya nyurokognitivu.

 

Dalili hizi zote husababishwa na kushikamana kwa chembe nyekundu za damu ndani ya mishipa ya damu kwa neno tiba siko seli kraisisi. Wakati wa kutokea kwa siko seli kraisisi, mgonjwa hupata maumivu makalina ya ghafla.

​

Siko seli kraisisi huweza kutokea kwa kipindi kifupi au kudumu kwa masaa kadhaa au siku kadhaa. Dalili zifuatazo huonekana pia;

​

  • Maumivu makali ya mwili haswa maeneo ya kifua, maungio yamwili, na mifupa, wakati mwingine mwili wote

  • Kufa mapema- inasemekana watu wenye ugonjwa wa siko seli hufa mapema kabla ya kufikisha miaka 20, hata hivyo wanaovuka umri huu huweza kuishi miaka mingi zaidi. Watu wenye dalili kali za ugonjwa huu huishi kwa wastani wa miaka 50

  • Maambukizi kwenye mfumo wa mapafu hivyo kuja na dalili za kukohoa

  • Kuvimba kwa maungio ya kiwiko cha mkono haswa kwa watoto walio zaidi ya miezi sita na kuendelea

  • KUpata homa za mara kwa mara

  • Kuishiwa damu na dalili za kuishiwa damu kama vile mapigo ya moyo kwenda kasi, kuzunguzungu, maumivu ya kichwa n.k

  • Kupata dalili zingine za kuathirika kwa ogani mbalimbali

 

Namna ya kujikinga kupata siko seli kraisisi

 

Hakuna njia ya kujikinga kupata siko seli kraisisi, baadhi ya mambo unayoweza kufanya na yanaweza kusaidia ni kama vile;

​

  • Kupata hewa safi ya kutosha(oksjeni) kutoka kwenye mazingira

  • Kunywa maji ya kutosha

  • Jizuie kupata baridi sana au kupata joto sana- hii inaweza kuzuia seli zako zisishikamane

  • Zuia kupata maambukizi, tibiwa haraka iwezekanavyo unapopata maambukizi

  • Onana na mtaalamu wa afya kama ulivyopangiwa

  • Zuia kufanya mazoezi makali ili kuzuia kukosa hewa ya oksjeni

  • Zuia kujipa stresi za kihisia jifunze namna ya kukabiliana na mambo

  • Usiishi maeneo ambayo yanahewa kidogo ya oksjeni kama milimani na kwenye ndege ambazo hazina hewa ya oksijeni

  • Acha kuvuta sigara

  • Jikinge na vyanzo vya maambukizi vinavyofahamika

  • Jizuie kukaa juani kwa muda mrefu

  • Tembea na maji mkononi ukiwa nyumbani au ukiwa unatembea ili kunywa mara kwa mara kiasi cha maji kinachoshauriwa kitaalamu

  • Fahamu dalili za upungufu wa maji mwilini ili unapozitambua ufanye haraka kunywa maji ya kutosha au kutafuta msaada kutoka kwa daktari

  • Pata chanjo ya vimelea

  • Shirikishana taarifa hizi zilizoandikwa hapa kwa mwalimu wako au mtu anayekutunza

  • Pata huduma za dharura haraka endapo joto la mwili limepanda juu ya nyuzi joto 38 na zaidi

  • Fanya usafi wa mikono yako, nawa mikono mara kw amara kama unapiga chafya au kuwahudumia wagonjwa wenye mafua.

​

​

Imeboreshwa mara ya mwisho 20.06.2020

​

ULY clinic inakushauri sikuzote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ili dhidi ya afya yako.
​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri kupitia namba za simu zilizopo chini ya tovuti hii au kubonyeza neno Pata Tiba

​

Rejea za mada hii

​

  1. Sickle cel disease.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3708126/. Imechukuliwa 20.06.2020

  2. Sickle cel disease.https://www.afro.who.int/health-topics/sickle-cell-disease. Imechukuliwa 20.06.2020

  3. Sickle cel disease. http://www.sicklecelldisease.org. Imechukuliwa 20.06.2020

  4. Sickle cel disease. http://www.scinfo.org. Imechukuliwa 20.06.2020

  5. Sickle cel disease . http://www.nhlbi.nih.gov/new/sicklecell.htm. Imechukuliwa 20.06.2020

  6. Johns Hopkins. Sickle cel disease. https://www.hopkinsmedicine.org/Medicine/sickle/patient/. Imechukuliwa 20.06.2020

bottom of page