Imeandikwa na daktari wa ULY Clinic
Matatizo gani mtoto anapata kwa maambukizi ya streptococcal kundi B?
streptococcal kundi B husababisha maambukizi mapema zaidi kwa kichanga baada ya kuzaliwa yanayoambatana na kuwepo kwa sumu za bacteria hawa katika damu na pia huweza kusababisha maambukizi ya uti wa mgongo. Maambukizi haya hutokea sana kwa watoto njiti, lakini huweza kuwadhuru vivhanga waliokamilika siku.
Kinga huhusihsa upimaji wa kutambua na kupewa dawa za kupambana na bacteria. Kwa sasa kuna mipango miwili inayokubaliwa na mashirika ya ACOG, AAP na CDC kutumika kutambua maambukizi haya kabla ya kujitokeza.
1.Wanawake wote wenye ujauzito kwenye wiki kati aya 35 na 37 wapimwe kwa kipimo cha kuotesha bakteria na kasha wakikutwa nao wapewe dawa aina ya ampicillin au penicillin wakati wakiwa na uchungu.
2.Mpango wa pili ni kutotegemea uoteshaji na kuangalia wanawake walio katika hatarishi ya maambukizi haya kutokea kwa watoto. Hatarishi ni kama uchungu kabla ya wakati(chini ya wiki 37), kupasuka kwa chupa ya uzazi masaa 18 kabla ya kujifungua, homa wakati wa ujauzito(zaidi ya nyuzi joto 38 za selicious), au kuwa na historia ya moto kuathiriwa na bakteria hawa. Nyongeza ni kwamba kwenye mipango hiyo miwili wanawake wote wenye historia ya bakteria huyu kuonekana kwenye mkojo wao kwa sababu huwa na bakteria hawa kwa wingi. Mipango yote miwili husaidia kupunguza lakini sio kuondoa kabisa maambukizi kwa kichanga.
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020
​
ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
​
​​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​