Mwandishi: ULY CLINIC
4/11/2021
Tarehe ya kushika mimba
​
Tarehe ya kushika mimba au tarehe ya kubeba ujauzito ni tarehe ambayo mwanamke anakuwa kwenye ovulesheni, kipindi hiki ni kifupi takribani masaa 24 tu. Kushiriki tendo la ndoa wakati huu kunamfanya kushika mimba.
​
Nini unatakiwa kufanya kwenye tarehe za kushika mimba?
​
Kama una afya njema na ukashiriki tendo la ndoa kisahihi, unatarajia kushika mimba katika tarehe za siku za hatari ambazo ni takribani 5. Unachotakiwa kufanya ni kushiriki katika siku za hatari tu na maandalizi ya mwili wako yanatakiwa kufanyika. Soma maelezo ya maandalizi kabla ya kushika mimba sehemu nyingine katika tovuti hii. Pia unaweza kusoma maelezo zaidi kuhusu siku ya kupata mimba.
​
Maelezo kabla ya kukokotoa
​
Weka chagua mwezi, tarehe na mwaka wa siku ya kwanza ya kuanza hedhi yako ya mwisho, kisha chagua idadi ya Siku za mzunguko wako wa hedhi moja hadi nyingine( mfano ni siku 22, 26, 28, 30, 32 n.k). Baada ya kujaza bofya Calculate na soma majibu kwa kulinganisha na aya zilizoandikwa hapo chini
Maelezo ya ziada kuhusu majibu ya kikokoteo
​
Aya ya kwanza inamaanisha kwamba, kama huna mimba utaingia hedhi inayofuata kuanzia tarehe ilioonyeshwa kwenye aya ya kwanza.
​
Aya ya pili inamaanisha kuwa kama huna ujauzito, tarehe za siku za hatari zinatarajiwa kuwa kati ya tarehe zilizoorodheshwa kwenye aya ya pili. Tarehe hizo ni siku ambazo unakuwa kwenye hatari ya kushika mimba)
​
Aya ya tatu inamanaisha, endapo umepata ujauzito tarehe yako ya matazamio ya kujifungua itakuwa kwenye tarehe hiyo iliyotajwa kwenye aya ya tatu.
​
Aya ya nne haipaswi kuonekana kama tarehe ulizoweka ni zile ambazo bado hujapata ujauzito.