top of page

Imeandikwa na madaktari na mafamasia wa ULY-Clinic

 

 

Dawa aina kundi la thiazolidinediones(TZD)

 

Dawa kwenye kundi hili ni kama

  • Pioglitazone

  • Rosiglitazone

 

Matumizi

​

Kiongezo kwenye tiba mazoezi na chakula kwa matibabu ya kisukari aina ya 2

 

Jinsi zinavyofanya kazi

Huongeza hisia ya homoni insulin kwenye chembe za misuli, mafuta na ini.

 

Taarifa kwa mgonjwa

  • Husababisha kuongezeka uzito

  • Mwili kuvimba

  • Kushuka zaidi kwa kiwango cha sukari kwenye damu zinapotumiwa na madawa mengine ya kisukari ama homoni ya insulin(ila haitokea unapotumia metformin)

  • Huweza kusababisha au kuongeza kasi ya  moyo kufeli na hatari ya kutunza maji kwenye mwili

  • Michomo kwenye sinus na koo

  • Misuli kuuma

  • Kichwa kuuma

 

Tahadhari/madhara makubwa

 

Boksi jeusi Moyo kufeli sana inahusishwa na dawa ya rosiglitazone

  • Kufeli kwa ini

  • Upungufu wa damu

  • Kuisha kwa mifupa

  • Kutolewa kwa mayai kwa wanawake wanaoanza kuingia kipindi cha koma hedhi

  • Kwenye ujauzito ipo kitengo C

 

Kundi maalumu

Moyo uliofeli- anza kutumia kwenye dozi ndogo iliyokubaliwa. Matumizi hayatakiwi kwenye kundi la moyo kufeli dalaja la 3 au la 4

 

Usitumie endapo

  • Moyo kufeli daraja la 3 au la 4

  • Ugonjwa wa ini

imeboreshwa 5/11/2018

bottom of page