Imeandikwa na daktari wa ULYCLINIC
Uchafu wa rangi ya blue-kijani ukeni
Ni nini husababisha kutokwana uchafu wa blue ukeni?
Kutokwa na uchafu wa bluu au kijani ukeni husababishwa na sababu mbalimbali, kubwa ikiwani maambukizi ya bakteria au vimelea wengine ukeni au kwenye maeneo yanayozunguka maeneo ya maumbile ya mwanamke pamoja na mikunjo ya mapaja(kinena).
Dalili
Dalili hutegemea kisabaisha, unaweza kupata dalili kati ya zifuatazo
-
Nguo za ndani kuwa na rangi ya bluu au bluu-kijani
-
Kutokwa na uchafu wa bluu, kijani au blue kijani
-
Kupata miwasho maeneo ya kinena
-
Kubadilika kwa ngozi ya maeneo ya kinena na uke
-
Kujamiana kwa shida
-
Kukojoa kwa shida
-
Hisia za miwasho au kuungua ukeni
-
Harufu mbaya ukeni
Visasababishi vya uchafu wa blue-kijani ukeni
Kisababishi kikubwa huwa ni maambukizi, maambukizi hayo yanaweza kuwa ya;
Maambukizi ya bakteria
-
Pseudomonas aeruginosa- Uchafu huwa wa kijani au blue-kijani
-
Neisseria gonorrhea- Uchafu mara nyingi huwa wa kijani
-
Chlamydia trachomatis- uchafu mara nyingi huwa wa kijani
Maambukizi ya parasaiti
-
Trichomonas Vaginalis- Uchafu mara nyingi huwa na rangi ya kijani
Vihatarishi
-
Kuwa na ugonjwa wa ngozi ujulikanao kama Intertrigo inamuweka mwanamke kupata maambukizi ya Pseudomonas aeruginosa kwenye ngozi(bonyeza kusoma zaidi)
-
Kuwa na Kinga za mwili kidogo
-
Kuvaa nguo za kubana kama vile tight na chupi kwa muda mrefu hivyo kusababisha maeneo ya uke kutopata hewa na kutengeneza unyevunyevu
-
Misuguano maeneo ya siri, kwenye mapaja na mashavu ya uke yanayoweza kuletwa na nguo za kubana
-
Unene/obeziti
-
Kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa
Vipimo na matibabu
Vipimo mara nyingi huwa havihitajiki endapo daktari ametambua tatizo nini, hata hivyo kipimo cha culture and sensitivity hufanyika ili kutambua aina ya bakteria na vipimo vingine ambavyo daktari ataona afanye ili kutofautisha tatizo hili na mengine
Matibabu mara nyingi huhusisha dawa maalumu za kutibu maambukizi ya bakteria anayesababisha tatizo hili au kutibu maonjwa ya zinaa.
Kumbuka endapo sababu halisi haijatibiwa basi tatizo huweza kuendelea
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri na tiba kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile dhidi ya afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa mara ya mwisho, 25.10.2020
Rejea za mada hii
-
Healthline. what does discharge during pregnancy mean. https://www.healthline.com/health/green-discharge-pregnant#trichomoniasis. Imechukuliwa 25.20.2020
-
Journal of Pakistan Medical association. Greenish-blue staining of underclothing due to Pseudomonas aeruginosa infection of intertriginous dermatitis. https://jpma.org.pk/article-details/4645. Imechukuliwa 25.20.2020
-
Family doctor. Intertrigo. https://familydoctor.org/condition/intertrigo. Imechukuliwa 25.20.2020