top of page

Imeandikwa na ULY-CLinic

 

Ujauzito wa Mapacha

 

Mara ngapi wanawake wanaweza kupata mapacha?

 

Mapacha hutokea kwa mtu mmoja (1) kati ya wajawazito 1000 kwa wazungu, na 1 kati ya wajawazito 80 kwa wanawake wa ki Afrika na mmoja (1) kati ya wanawake 155 wa bara la Ulaya.

 

Kuzaa mapacha huwa haitegemeani na asili, kurithi, umri, na idadi ya uzazi wa mtu. Mapacha hata hivyo huathiriwa na vitu hivyo vilivyotaja hapo juu pamoja na dawa za uzazi. Mama mwenye mapacha ana nafasi kubwa ya kuwa na mapacha kwenye ujauzito zitakazofuata.

 

Uzazi wa kisasa (uchavushwaji wa kutumia mashine) huchangia pia kupata mapacha. Bahati ya kupata mapacha huwa asilimia 16- 40 kwa kutumia dawa  aina ya gonadotrophin. Asilimia 25-30 kwa kutumia dawa ya  superovulation na asilimia 7-13 kwa kutumia dawa ya clomiphen.

 

Wanawake wanaopandikizwa mayai yaliyochavushwa nje ya miili yao kwa mashine huwa na bahati ya kupata mapacha kwa asilimia 22. Kwa wanawake wanaotumia njia saidizi za kisayansi ili kupata mimba wana bahati ya asilimia 25-30 ya kupata mapacha, na asilimia 3 ya kupata watoto watatu na kupata zaidi ya mapacha wawili kwa asilimia 0.5 hadi 1.

 

Mapacha wa kufafana hutokeaje?

 

Mapacha wa kufafa hutokana na kugawanyika mara mbili kwa yai moja lililochavushwa na hivyo kuwa viumbe viwili. Muda wa kipindi cha kugawanyika kwa yai huwa na umuhimu mkubwa katika mapacha hawa kwani huweza kutoa mapacha wa sifa Fulani.

Kuanzia masaa 72 hadi siku 13, endapo mgawanyiko utafanyika basi mapacha wa kufafanana watatokea

​

Endapo mgawanyiko utafanyika wiki mbili baada ya uchavushwaji wa yai basi mapacha walioungana hutokea, ukubwa  wakutokea kwa mapacha wa kuungana bado haufahamiki lkini inasemekana ni mtoto 1 kati ya zao 60,000.

 

Mapacha wa kutofafana hutokeaje?

 

Mapacha wa kutofafana hutokea endapo mayai mawili yamechavushwa kwa pamoja katika uzazi.

 

Uchavushwaji wa mayai mawili unaweza kufanyika wakati mmoja  wa mzunguko wa hedhi kwenye vipindi  viwili tofauti vya kushiriki tendo la kujamiiana. Au mayai mawili kuchavushwa kwenye vipindi viwili tofauti vya mzunguko wa hedhi yaani yai jingine limechavushwa kwenye kipindi kinginine yai la kike linapotolewa kiwandani.

​

​

Sifa gani za ujauzito wa mapacha ziatofautisha na ujauzito usio mapacha?

 

Kujifungua njiti -karibia asilimi 50 ya watoto njiti(watoto wasiotimia umri kuzaliwa kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito), kujifungua kabla ya wakati ni kihatarishi cha mtoto kuugua na kufa kwenye ujauzito wa mapacha. Mimba mapacha huchangia asilimia 10 ya kujifungua njiti. Umri mkubwa kuishi tumboni mwa mama kwa mapacha ni wiki 35 na wa watoto watatu ni wiki 33 na wane ni wiki 31.

 

Kudumaa tumboni- 2/3 ya mimba mapacha hupatwa na hili. Ingawa mimba ya mtoto mmoja hufanana na mimba mapacha katika ukuaji hadi wiki ya 28-30, baada ya hapo kupungua kwa ukuaji kunaanza kuonekana na hutegemewa. Kutokuwa kunaweza kuonekana kwa pacha mmoja tu au na mwenzake. Kutokuwa kwa usawa kwa mapacha huonekana kwa asilimi 10-25 kwenye ujauzito mapacha na huwa chanzo za mtoto mmoja kufa baada ya kujifungua. Mtoto kutokuwa vema kwenye ujauzito mapacha hutokana na kutopata chakula vema kutoka kwenye kondo la mama, mtoto na mtoto kubadilishana damu na visababishi vingine vinavyoweza kusabisha mimba ya mtoto mmoja kutokua vema. Utofauti wa kukua huweza kuelezewa endapo kuna utofautiwa uzito zaidi ya asilimia 20 wakati wa kuzaliwa mapacha.

 

Kupoteza mtoto baada ya kujifungua mara tano zaidi kuliko ujauzito wa mtoto mmoja baada ya kujifungua. Hatari ni kubwa kwa watoto waliokuwa wanatuma kondo moja na wanatofautiana ukuaji. Ni sababu kuu ya kusababisha kichanga kufa baada ya kujifungu kwa vile huwa njiti. Mapacha huchangia asilimia 25 ya vichanga kufa baada ya kujifungua, sababu zingine za kusababisha njiti ni kama vile mtoto kuwa na madhaifu ya kiuumbaji, kujiongezea damu kwa mapacha tumboni, kondo kutolisha vema mapacha na ajali za uzazi au kukosa hewa safi kwa sababu ya kujifungua kwa shida.

 

Mimba kutoka yenyewe- huwa mara mbili zaidi ya ujauzito wa mtoto mmoja. Kuongezeka kwa matumizi ya ultrasound, kumeweza kuonyesha ushahidi wa kupotea kwa kichanga mmoja mmoja ama kutoka kwa mimba kwa asilimia 21-63 kwenye mimba mapacha zinazotoka zenyewe. Inakadiliwa kwamba mimba mapacha asilimia 50 tu zilizotambuliwa mapema zaidi katika kipindi cha ujauzito huendelea mpaka wakati muafaka wa kujifungua.

 

Matatizo ya kiuumbaji kwa mtoto-hatari huwa mara mbili zaidi ya mimba moja kwa watoto mapacha wa kufanana.

 

Shinikizo la damu la ujauzito- tatizo hili hutokea mara 3-5 zaidi kwenye ujauzito mapacha, hatarishi huwa kubwa zaidi kama mimba itakuwa na watoto zaidi ya wawili ukilinganisha na mimba ya mtoto mmoja. Hutokea kwa usawa kati ya mimba za mapacha wa kufanana au kutofanana.

 

Upungufu wa damu- kwa sababu ya upungufu wa madini chuma, hutokana na kuongezeka kwa matumizi ya watoto mapacha. Kwa kiasi kidogo uunfufu wa damu kutokana na upungufu wa madini ya foliki asidi hutokea kwenye mimba mapacha. Kwa nyongeza kifiziolojia kuongezeka kwa giligili ya plazima huchangia kupunguza madini haya.

 

Maji mengi kwenye chupa ya uzazi- kwenye kifuko kimoja au vyote hutokea sana kwa mapacha wa kufanana wanaotumia kondo moja kwa sababu ya kuongezeana damu.

 

Mtoto kulala vibaya- huchangia mama kujifungua kwa njia ya upasuaji.

 

Kondo la nyuma kunyofoka- huweza kutokea haraka baada ya kujifungua pacha mmoja, kujiachia kwa kondo la nyuma mapema zaidi huweza kusabaisha mtoto kufia tumboni kwa sababu hapati chakula na hewa safi kutoka kwa mama. Hali hii huweza kutokea pia kabla ya uchungu kuaza.

 

Kondo la nyuma kujishikiza chini ya uzazi karibu na shingo ya kizazi- hii husababisha mama kutokwa na damu wakati wa ujauzito pasipo kuwa na uchungu, dalili hii huwa hatarishi pia husababisha mama kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa kuogopa kwamba kondo la nyuma litanyofoka kabla ya mtoto kutoka na hatari ya mama kutokwa na damu nyingi na mtoto kufa pia.

​

​

Mambo gani ya kufanyika kwa mimba mapacha kipindi cha ujauzito?

 

Kwanza kugundua kwamba mimba ni mapacha kunatakiwa kufanyike mapema kwa sababu husaidia kupunguza vihatarishi na matatizo kwa mama na mtoto

 

  • Kuhudhuria kliniki vipindi vingi zaidi, angalau kila baada ya wiki mbili ujauzito unpofikia wiki 20-36

  • Chakula- nyongeza ya chakula inatakiwa kufanyika wanga inatakiwa kula kilokalori 300 protini kilokalori 80 kwa siku na madini chuma miligramu 60-100 kwa siku, madini ya foliki asidi milligram 1 kwa siku na uzito kama unapimwa unatakiwa kuongezeka kwa pound 35-45

  • Kupumzika mda mwingi

  • Mgonjwa anatakiwa kujua dalili na viashiria vibaya vya uchungu kabla ya mimba kutimia. Mgonjwa anatakiwa afahamu na afahamishwe kila anapohudhuria kliniki.

  • Zuia, tambua na tibu kwa uwezo umakini dalili za uchugu kabla ya umri wa mimba kutimia kwa kuwasilina na daktari wako

  • Kufanya kipimo cha ultrasound ili kutazama ukuaji wa mapacha na uzito, kwa kufanya hivi unaweza kutambua kama mtoto mmoja anakuwa kuliko mwingine na kunautafauti ya uzito zaidi ya asilimia 20 na matibabu yanatakiwa kufanyika kwa jinsi tatizo litakapoonekana

  • Chunguza na tibu shinikizo la damu la ujauzito na kifafa cha mimba.

  • Tazama na tibu madhira mengine yanayoweza kutokea kwa uchache kama, maji mengi kwenye chupa ya uzazi, watoto kujiongezea damu, kifo ndani ya uzazi

  • Pima na tambua matatizo kama mtoto kushindwa kukua, maji kidogoau mengi  kwenye chupa ya uzazi, kifafa cha mimba, matatizo ya kiuumbaji ya mtoto. Baadhi ya taasisi zimejiwekea utaratibu wa upimaji utambuzi wa mambo haya kwenye wiki ya 32-34 kwa mapacha kwa sababu huwa naongezeko la vifo wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua.

  • Wazazi wapange kuhusu mapacha wao wakiwa nyumbani baada ya kujifungua.

 

Namna gani ya kupunguza kujifungua kabla ya mimba kutimia umri kwa ujauzito wa mapacha?

 

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata uchungu kabla ya wakati kwa mimba mapacha kwa sababu ya kuongezeka haraka kwa tumbo, watoto kuzaliwa njiti kutokana na jambo hili la uchungu wa mapema huhusika na kusababisha vifo na madhara mbalimbali kwa kichanga. Kwa hiyo jitihada kubwa zinatakiwa kuwekwa ili kuzuia uchungu huu wa kabla ya wakati. Madhumuni kwa ujumla ni kwamba mbali na matatizo mengine, ni mimba kufikisha umri wa wiki 34 au zaidi, zaidi ya wiki 34 madhara ya njiti huwa hayatokei sana. Kipindi muhimu cha kuzuia madhara haya ni wiki ya 24 hadi 32 ya ujauzito.

 

Kupumzika, kulazwa, dawa kinga ya uchungu, uchunguzi wa shingo ya uzazi kila wiki na kinga ya kufunga shingo ya uzazi hutumiwa wakati wmingine ili kuongeza uwezo wa mimba kufika wiki 34. Si njia yoyote inayoaminika asilimia mia kupunguza uchungu kabla ya wiki hizo kwenye mimba mapacha.

 

Pia tafiti zimeonyesha dawa za kuzuia uchungu na utambuzi wa mapema kuwa haujatoa matokeo mazuri sana uzuia uchungu kabla ya wakati kwenye ujauzito wa mapacha.

 

Nini hutokea pacha mmoja anapofia ndani ya ujauzito?

 

Kama kichanga  akifia ndani ya ujauzito wa ujauzito mapacha wakati wa miezi mitatu ya kwaza, basi pacha huyo atafyonzwa na kupotea au anaweza kubaki na kuwa mdogo umbo la ubapa, lionyauka kwa jina huitwa fetus papyraceous. Kama mama hakufanya kipimo cha ultrasound kipindi hiki basi ujauzito hautatambulika kama ulikuwa wa mapacha.

 

Kama kifo kikitokea kwenye miezi mitatu ya pili au ya tatu ya ujauzito, pacha mwenzake anaweza kupata shida na madhara makubwa. Uwezo wa pacha wa pili kuishi hutegemea, kisababishi cha pacha mmoja kufa, sifa ya upacha na aina ya kondo, umri wa ujauzito wakati pacha mmoja anakufa, na mda kati ya kufa pacha mmoja na kipindi cha kujifungua pacha aliyebaki. Watoto wanaotumia kondo moja huwa hatarini kufa kama pacha mmoja akifia tumboni.

​

​

Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile dhidi ya  afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.

​

​

Imeboreshwa 9.11.2020

​

​

Rejea za mada

​

  1. Chasen ST, et al. Twin pregnancy: Labor and delivery. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 18.03.2020

  2. Porreco RP, et al. Delayed-interval delivery in multifetal pregnancy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 18.03.2020

  3. Frequently asked question. Pregnancy FAQ188. Multiple pregnancy. American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Multiple-Pregnancy. Imechukuliwa 18.03.2020

  4. Gabbe SG, et al. Multiple gestations. In: Obstetrics: Normal and Problem Pregnancies. 7th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 18.03.2020

  5. American College of Obstetricians and Gynecologists. Multiples: When it's twins, triplets, or more. In: Your Pregnancy and Childbirth Month to Month. 6th ed. Washington, D.C.: American College of Obstetricians and Gynecologists;2015.

  6. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) Committee on Practice Bulletins — Obstetrics. ACOG Practice Bulletin No. 169: Multifetal gestations: Twin, triplet, and higher-order multifetal pregnancies. Obstetrics & Gynecology.

​

Bonyeza hapa kusoma namna ya kupata ujauzito wa mapacha

​

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​​

​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

​

Ujauzito mapacha
bottom of page