top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Ukichaa baada ya kujifungua

​

Ukichaa baada ya kujifungua ni ugonjwa wa kiakili linalotokea kwa nadra sana. Hutokea mara nyingi mara baada ya mama kujifungua mtoto. 

​

Dalili kuu huwa ni mabadiliko ya hali moyo yanayokuwa endelevu, kwa kawaida mabadiliko haya hutokea kwa wamama wengi ndani ya wiki chache. Wanawake wenye ukichaa baada ya kujifungua huhitaji matibabu kwani wanaweza kujidhuru au kudhuru mtoto.

​

Ugonjwa huu huwa na jina jingine?

​

Ndio

​

Majina mengine ya ugonjwa huu wa kiakili ni pruperio saikosisi au postinato saikosisi au postipatamu dipreshen

 

Ni zipi dalili za ugonjwa huu wa akili?

​

Dalili huanza ghafla ndani ya wiki mbili baada ya kujifungua na kwa kwa nadra sana unaweza kuanza wiki zaidi ya mbili mara baada ya kujifungua mtoto.

​

Dalili hujumuisha;

​

  • Imani potofu dhidi ya mtoto au mambo Fulani

  • Hali za kimaniki- kuongea au kufikiria sana na pasipo umakini, kujihisi upo juu, kukosa nguvu na hamu ya kula, kuwa na ang’zayati na kupata shida ya kukosa usingizi

  • Kuona na kusikia vitu ambavyo watu wengine hawavioni

  • Kushidnwa kujizuia kufanya jambo Fulani

  • Kujishuku na au kuwa na hofu

  • Kutotulia

  • Kuhisi kuchanganyikiwa

  • Kupata tabia ambazo hukuwa nazo

 

Visababishi

​

Mpaka sasa hakuna uhakika kwamba ni nini kinachosababisha ugonjwa huu wa akili, hata hivyo vihatarishi huwa ni;

​

  • Kuwa na historia katika familia ya ugonjwa wa akili, haswa ugonjwa wa ukichaa baada ya kujifungua

  • Kuwa na historia ya ugonjwa wa madhaifu ya kibaipola au schizophrenia

  • Kupata majeraha ya kujifungua( kwa mama au kwa mtoto)

  • Kuwa na tatizo hili kwenye ujauzito uliopita

 

Wakati gani wa kumwona daktari

 

Ugonjwa huu wa akili huhitaji matibabu ya haraka kwani huwa ni hatari kwa mama na mtoto, utahitaji matibabu ya dharura. Mwone daktari haraka endapo unaona kuwa na shida hii kwa ushunguzi na tiba inayoendana na wewe.

 

Matibabu

​

Matibabu hulazimika kufanyika hospitali kwa wanawake wengi, utahitaji kuonwa na daktari wa magonjwa ya akili pamoja na mwanao.

​

Matibabu huhusisha matumizi ya dawa na ushauri wa kisaikolojia

​

Matibabu dawa

​

Dawa zinazotumika ni katika kundi la antidipresanti- husaidia kupunguza dalili za huzuniko

​

  • Antisaikotiki- husaidia kudhibiti dalili za mania, imani potofu na kuzuia kuona au kusikia vitu ambavyo wengine hawasikii au kuona

  • Dawa za kurekebisha hali ya moyo- husaidia kurekebisha mwitikio wa moyo na kuzuia dalili kujirudia

 

Tiba ushauri wa saikolojia

​

Ushauri huu huhusisha tiba ya tabia na kujitambua. Tiba hii huhusisha mazungumzo maalumu yanayoweza kukufanya ukabiliane na tatizo hili

​

Kujikinga

​

Kama upo kwenye kihatarishi kikubwa cha kupata ukichaa baada ya kujifungua, unatakiwa kuwa na uangalizi wa mtaalamu wa magonjwa ya akili wakati wa ujauzito.

​

Unatakiwa kukutana na daktari wako unapokaribia wiki 32 za ujauzito pamoja na yeyote Yule ambaye atakuwa akishirikiana na wewe kwenye uzazi wako ikiwa pamoja na mpenzi wako, marafiki, mkunga wako. Hii husaidia kuhakikisha kwamba kila mtu aliyekaribu na wewe anafahamu vema kuhusu hatari ya wewe kupata tatizo hili na kupanga namna ya kukuhudumia endapo hali  itatokea.

​

Wiki chachemara baada ya kujifungua unatakiwa pia kutembelea mtaalamu wako wa ugonjwa wa akili kwa mazungumzo.

​

Ni lini utapona ugonjwa wa akili baada ya kujifungua mara baada ya kuupata?

​

Kwa wagonjwa wenye dalili kali huchukua wiki 2 hadi 12 kupona, lakini hata hivyo tatizo hili huweza kudumu kwa muda wa miezi 6 hadi 12.  Endapo mama atapata matibabu, uponyaji utatokea na tatizo kupotea kabisa kwa wengi wa wanawake wanaopata tatizo hili.

​

Kipindi cha kuwa na ugonjwa huu wa akili huweza kufuatiwa na ugonjwa wa dipresheni, ang’zayati, na kutojiamini. Huweza kuchukua muda kidogo hali hizi kupotea. Baadhi ya wamama hupata ugumu kuungana na mwanawe au kuhisi amekosa muda mwingi wa kuwa pamoja na mtoto wake, endapo mama huyu atapata ushirikiano kutoka kwenye familia yake na mpenzi, hali hii ataweza kuishinda mapema zaidi na kupotea.

​

Wanawake waliopatwa na tatizo hili huweza kupata mimba kama kawaida, nusu yao huweza kupata tatizo hili tena kwenye ujauzito unaofuata

 

Ushirikiano kutoka kwa marafiki na mpenzi

​

Mgonjwa mwenye tatizo hili anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa mpezi wake na familia pamoja na watu wanaomzunguka ili kupona haraka, mpenzi na wanafamilia mnaweza kufanya mambo yafuatayo;

​

  • Kuwa mpole na kutoa ushirikiano

  • Kumsikiliza mke

  • Kumsaidia kufanya kazi za ndani na kupika

  • Kumpa muda wa kulala na kupumzika kwa jinsi inavyowezekana

  • Kumsaidia kufanya mahemeziya vitu vya ndani na kazi za nyumbani

  • Kuweka mazingira ya nyumbani kuwa tulivu na yenye ukimya jinsi inavyowezekana

  • Kutokuwa na wageni wengi nyumbani

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

 

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

 

Imeboreshwa mara ya mwisho,

​

Rejea zamada hii,

​

  1. Postpartum psychosis. https://www.app-network.org/. Imechukuliwa 31.07.2020

  2. Postnatal depression and perinatal mental health.Mind. https://www.mind.org.uk/information-support/types-of-mental-health-problems/postnatal-depression-and-perinatal-mental-health/postpartum-psychosis/#treatments. Imechukuliwa 31.07.2020

  3. Postpartum psychosis. NHS. https://www.nhs.uk/conditions/post-partum-psychosis/. Imechukuliwa 31.07.2020

  4. Postpartum psychosis.Royal College of Psychiatrists: https://www.rcpsych.ac.uk/mental-health/problems-disorders/postpartum-psychosis. Imechukuliwa 31.07.2020

bottom of page