Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Jumatatu, 24 Julai 2023
Mimba ya miezi minne
Mimba ya miezi minne ni sawa na mimba ya wiki 13 hadi 16 Katika makala hii utajifunza kuhusu nini kinatokea kwenye wiki ya 13 hadi ya 12 ya ujauzito. Kumbuka kuingia miezi minne ya ujauzito ni kuingia katika kipindi cha pili cha ujauzito.
Mimba ya wiki 13
Ni wiki inayoashiria kuisha kwa kipindi cha kwa cha ujauzi (mwezi wa kwanza mpaka watu) na mwanzo wa kipindi cha pili cha ujauzito (mwezi wa tano mpaka wa sita)
Nini hutokea kwa mtoto
Mtoto huendelea kuongezeka urefu na uzito, hata hivyo uzito huongezeka taratibu
Mifumo na viuongo mbali mbali huendelea kuimarika zaidi
Mtoto huendelea kucheza tumboni
Nini hutokea kwa mama
Uzalishwaji wa homoni za ujauzito hupungua na kupelekea dalili nyingi za ujauzito zinazomfanya mama kujisikia vibaya kuisha. Asilimia kubwa ya wajawazito hurejea katika hali ya kawaida na kufurahia maisha ya kila siku
Hamu ya kufanya ngono huongezeka japo si kwa wanawake wote
Mimba huanza kuonekana kwa nje
Kuanza kuongezeka uzito
Hatari ya kupata uti huongezeka
Nini cha kufanya
Kula mlo kamili na kufanya mazoezi kama inavyopendekezwa, na kuepuka matumizi ya pombe na sigara
Anza kuvaa nguo zenye nafasi zisizobana tumbo
Fanya kipimo cha ultrasound; itasaidia kubaini shida yoyote kwa mtoto na maendeleo kwa ujumla
Ongea na watoa huduma kliniki unapohisi dalili na viashiria vya U.T.I
Mimba ya wiki 14
Nini hutokea kwa mtoto
Jinsia ya mtoto inaweza kuonekana katika kipimo cha ultrasound (si wataalamu wote wa vipimo wanaweza kuona jinsia katika wiki hii, inahitaji uzoefu mkubwa)
Figo zinakuwa zimekamilika na mtoto huanza kukojoa
Misuli ya uso wa mtoto huanza kuonesha hisia mfano kukunja ndita na kukonyeza lakini macho yanakuwa yamefunga
Huanza kunyonya midomo, pia katika kipindi hiki mtoto huanza kunyonya kidole gumba
Nini hutokea kwa mama
Kwa mwanamke mwenye zao zaidi ya moja huanza kuhisi mtoto anapocheza tumboni
Tumbo huendelea kuwa kubwa
Mama huendelea kuongezeka uzito
Hamu ya kula huongezeka
Pia mabadiliko mengine hutokea kama vile kukojoa mara kwa mara n.k
Mimba ya wiki 15
Nini hutokea kwa mtoto
Uwezo wa mtoto kuonesha hisia za uso hungezeka
Mtoto huanza kunyonya kidole gumba
Masikio ya mtoto huwa yamekamilika na anaanza kusikia sauti kutoka katika mazingira na ndani ya tumbo la mama
Mtoto anaanza kuhisi mwanga unaotoka katika mazingira japo macho yake huwa yamefumba
Mtoto huanza kuchezesha miguu na mikono
Nini hutokea kwa mama
Mama huendelea kuona mabadiliko ya uzito na sehemu mbali mbali za mwili
Rangi ya eneo la matiti linalozunguka chuchu huwa jeusi Zaidi
Kutokana na kuendelea kutanuka kwa kizazi mama huhisi maumivu ya tumbo na kiuno
Mimba ya wiki 16
Nini hutokea kwa mtoto?
Mtoto huwa na ukubwa wa limao au parachichi dogo
Wiki hii huwa mwanzo wa ukuaji na kuongezeka kwa uzito wa mtoto ambako huonekana zaidi katika wiki zinaofuata
Sura yake huwa ya binadamu halisi, macho na masikio ambayo yalikuwa pembeni mwa kichwa hujongea na kukaa sehemu yake
Mtoto huanza kuonesha mijongeo ya misuli ya miguu, mikono na uso. Mijongeo ya misuli midogo ya uso huweza kuonesha hisia kama kukunja ndita na kukonyeza
Nini hutokea kwa mama?
Ongezeko la homoni za ujauzito katika wiki hii humfanya mwanamke kuwa na mabadiliko yafuatayo;
Kuwa na mn’gao ambao watu huweza kuhusianisha na ujauzito
Kutokwa na chunusi kutokana na ngozi kuzalisha kiasi kikubwa cha mafuta
Kuvimba kwa mishipa ya damu ya miguu au kuhisi maumivu na misuli ya miguu kukaza
Kuongezeka au kupungua kwa hamu ya kushiriki ngono
Tumbo la ujauzito huanza kuonekana, na mama huweza kuhisi kukojoa mara kwa mara
Mambo ya kufanya katika ujauzito wa wiki 16
Usitumie dawa za kutibu chunusi badala yake safisha uso kwa sabuni isiyo na kemikali na tumia losheni isiyo na kiwango kikubwa au isiyo na mafuta kabisa
Fanya mazoezi na nyoosha miguu endapo unahisi maumivu au misuli kukaza
Imeboreshwa:
Jumatatu, 24 Julai 2023 20:31:42 UTC
Rejea za mada hii:
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]