Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Jumatatu, 24 Julai 2023
Mimba ya miezi mitano
Mimba ya miezi mitano ni sawa na mimba ya wiki 17 hadi 20, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi mitano.
Mimba ya wiki kumi na saba(17)
Nini hutokea kwa mtoto
Mtoto huendelea kungezeka uzito na urefu
Mafuta hutengenewa katika Ngozi yake ili kumpa joto
Nywele za kichwa, kope na nyusi hujaa
Mifumo yake ya mwili huendele kuimarika Zaidi
Mtoto huanza kuazalisha maji ya chupa ya uzazi(amniotiki) kupitia mapafu
Nini hutokea kwa mama
Huongezeka uzito
Hamu ya kula huongezeka
Huwa na nguvu zaidi
Hushindwa lala vizuri kutokana na mimba kuwa kubwa
Mimba ya wiki kumi na nane (18)
Nini hutokea kwa mtoto?
Mtoto huendelea kuongezeka kimo na uzito
Mtoto huwa na ukubwa wa hoho
Mifumo ya mwili huendelea kuimarika
Mtoto huanza kupiga miayo na kwiki
Nini hutokea kwa mama?
Tumbo huendelea kukua kwa kasi
Matumizi ya damu huongezeka hivyo mama anaweza kuhisi kizunguzungu hasa akisimama kwa haraka baada ya kukaa. Hali hii husababishwa pia na mgandamizo wa mishipa ya damu kutokana na mimba kuwa kubwa
Mgandamizo huo husababisha pia maumivu ya mgongo na kiuno
Mambo ya kuzingatia
Epuka kulala chali
Kunywa maji ya kutosha
Endelea kutumia virutubishi vya madini chuma, pamoja na vyakula vyenye madini chuma
Fanya mazoezi ya viungo
Mimba ya wiki kumi na tisa (19)
Nini hutokea kwa mtoto
Figo za mtoto huanza kutengeneza mkojo
Uwezo wa kusikia sauti kutoka mazingira ya nje y a mama huongezeka
Mfumo wa ndani wa uzazi wa mtoto wa kike hukamilika na ovari zake huanza kuzalisha mayai
Via vya uzazi vya nje kwa mtoto wa kiume huonekana vema
Mtoto huwa na umbo lenye ukubwa wa embe
Nini hutokea kwa mama
Kuendelea kuhisi maumivu ya kiuno na mgongo
Kuendelea kuhisi mgandamizo kwenye nyonga
Mimba ya wiki 20
Humaanisha miezi mitano ya ujauzito, ambapo ni nusu ya safari ya ujauzito.
Nini hutokea kwa mtoto?
Huwa na urefu wa takribani inchi 11
Kichwa huwa na nywele zilizokuwa vema, na mwili wote hufunikwa na vinyweleo laini
Ngozi yake huwa na utando mweupe unaozuia isijikunje
Mifupa laini hubadilika kuwa migumu kiasi
Korodani ambazo zilikuwa pamoja na matumbo huanza kushuka kuelekea kwenye mifuko yake
Nini hutokea kwa mama?
Kuanza kuhisi mtoto akicheza tumboni hasa kwa wanawake ambao ni ujauzito wa kwanza
Kuvimba miguu kutokana na kuongezeka kwa maji katika damu
Kupata kiungulia na chakula kutomeng’enywa vema
Kushindwa kulala vema kutokana na mgandamizo wa mimba
Matiti hujaa na Sehemu ya chuchu huwa nyeusi Zaidi na kuwa na vitu kama vipele, na wakati mwingine kutoa maziwa
Katika kipindi hiki mimba huendelea kukua kwa kasi na kuwa usawa wa kitovu, na kuongezeka kwa takribani inchi moja na nusu kwa wiki zinazofuata
Mstari mweusi chini ya kitovu hutokea na ngozi ya tumbo huanza kuwa na michirizi
Imeboreshwa:
Jumatatu, 24 Julai 2023 20:30:58 UTC
Rejea za mada hii:
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]