top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi sita

Mimba ya miezi sita

Mimba ya miezi sita ni sawa na mimba ya wiki 21 hadi 24, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi sita.


Mimba ya wiki sishirini na moja (21)

Humaanisha miezi mitano na siku moja ya ujauzito.


Nini hutokea kwa mtoto?


  • Huwa na urefu wa ndizi

  • Kichwa huwa na nywele zilizokuwa vema, na mwili wote hufunikwa na vinyweleo laini

  • Ngozi yake huwa na utando mweupe unaozuia isijikunje

  • Mifupa laini hubadilika kuwa migumu kiasi

  • Korodani ambazo zilikuwa pamoja na matumbo huanza kushuka kuelekea kwenye mifuko yake



Nini hutokea kwa mama?


  • Kuanza kuhisi mtoto akicheza tumboni hasa kwa wanawake ambao ni ujauzito wa kwanza

  • Kuvimba miguu kutokana na kuongezeka kwa maji katika damu

  • Kupata kiungulia na chakula kutomeng’enywa vema

  • Kushindwa kulala vema kutokana na mgandamizo wa mimba

  • Matiti hujaa na Sehemu ya chuchu huwa nyeusi Zaidi na kuwa na vitu kama vipele, na wakati mwingine kutoa maziwa

  • Katika kipindi hiki mimba huendelea kukua kwa kasi na kuwa usawa wa kitovu, na kuongezeka kwa takribani inchi moja na nusu kwa wiki zinazofuata

  • Mstari mweusi chini ya kitovu hutokea na ngozi ya tumbo huanza kuwa na michirizi




Mimba ya wiki ishirini na mbili (22)

Nini hutokea kwa mtoto

  • Mtoto huwa na uzito wa gramu 430 na uzito kati ya sentimeta 27.8

  • Urefu wake huwa sawa na ukubwa wa papai na urefu wa machenza matano

  • Vinyweleo vinavyofunika mwili wake huanza kupata rangi nyeusi

  • Mifupa yake hukomaa

  • Uwezo wake wa kusikia huongezeka zaidi na anaweza kutambua sauti ya mama

  • Pia huweza kuhisi sauti na mijongeo kutoka nje na kuonesha muitikio, mfano anaweza kuamka anaposikia kelele



Nini hutokea kwa mama

  • Mama huendelea kuona mabadiliko kama

  • Kuhisi vitu vinatembea kwenye mikono

  • Kupata maumivu ya miguu

  • Kuvimba miguu kiasi

  • Kubanwa pua na mafua ya mara kwa mara

  • Kutokwa damu kwenye fizi



Mimba ya wiki ishirini na tatu (23)


Nini hutokea kwa mtoto
  • Mtoto huwa na uzito wa gramu 450 na uzito kati ya sentimeta 28 hadi 36

  • Vinyweleo vinavyofunika mwili wake huanza kupata rangi nyeusi

  • Mifupa yake hukomaa

  • Uwezo wake wa kusikia huongezeka zaidi na anaweza kutambua sauti ya mama

  • Pia huweza kuhisi sauti na mijongeo kutoka nje na kuonesha muitikio, mfano anaweza kuamka anaposikia kelele



Nini hutokea kwa mama
  • Mama huendelea kuona mabadiliko kama

  • Kuhisi vitu vinatembea kwenye mikono

  • Kupata maumivu ya miguu

  • Kuvimba miguu kiasi

  • Kubanwa pua na mafua ya mara kwa mara

  • Kutokwa damu kwenye fizi


Mimba ya wiki ishirini na nne (24)


Nini hutokea kwa mtoto
  • Hadi kufikia mwisho wa wiki ya 24 mtoto huwa na uzito wa kati ya gramu 600 hadi 700

  • Ubongo na mfumo wa fahamu huendelea kukua na kuwa imara

  • Mapafu huwa yamekomaa kwa kiasi kikubwa na endapo akizaliwa katika kipindi hiki anaweza kujaribu kupumua mwenyewe

  • Ngozi yake huwa na mikunjo na mafuta huendelea kutengenezwa kwenye ngozi



Nini hutokea kwa mama
  • Mama anaweza kuona ongezeko la miguu yake kutokana na viatu alivyokuwa akivaa awali kutokumtosha

  • Ngozi ya tumbo kuwa kavu na kupata muwasho kutokana na michirizi

  • Kuota nywele kwenye maeneo ambayo sio rasmi kama vile kuzunguka kitovu na chuchu

  • Ngozi ya sehemu za siri na maeneo ya chuchu kuwa nyeusi zaidi

  • Kukoroma

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:30:34 UTC

Rejea za mada hii:

  1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

  2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

  3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

  4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

  5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

  6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

  7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

  8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

  9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page