top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

© Hairuhusiwi kukopi bila kibali cha ULYCLINIC
batholin uvimbe-ulyclinic
uvimbe-wa-batholini-ulyclinic

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

 

Uvimbe wa batholini

 

Uvimbe wa batholini katika makala hii pia unamaanisha jipu kwenye maeneo ya uke karibu na tundu la uke au tundu la uzazi(angalia picha kwa uelewa zaidi). Uvimbe huu huweza kuonekana kama uvimbe wa mashavu ya uke.

 

Uvimbe wa batholini ni uvimbe unaotokea mwanzoni mwa tundu la uke na pembeni kidogo mwa mashavu ya uke. Ukichora uke kwa sura ya saa ya mshale, uvimbe huu utaonekana kwenye mshale wa majira  ya sa 4 asubuhi na sa 8 mchana(angalia picha kwa maelezo Zaidi).

 

Uvimbe wa batholini  hutokana na kuziba kwa mirija ya kupitisha uteute unaotoka kwenye tezi za batholini. Endapo tezi moja imeziba uvimbe utaonekana mmoja na endapo tezi zote zimevimba, vimbe zitaonekana pande zote za uke. Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kutokea kwa uvimbe wa batholin ambazo zimeorozeshwa kwenye Makala hii.

 

Batholini ni nini?

 

Batholini ni tezi mbili za uke zinazozalisha uteute wakati wa kushiriki tendo la kujamiana, uteute huu husaidia kulainisha tundu la uke na kufanya uume uteleze kirahisi wakati wa tendo.

 

Dalili

​

Kama uvimbe wa batholini haujapata maambukizi, unaweza usiwe na dalili yoyote ile mbali na uvimbe, hata hivyo kama uvimbe ndo unaanza, hauwezi kuonekana kirahisi. Dalili ambazo utaziona zinaweza kuwa;

 

  • Kuonekna kwa uvimbe usiouma karibu na tundu la uke (kwenye mishale ya sa 4 asubuhi na sa nane mchana)

  • Kukosa uhuru wakati wa kukaa au kutembea

  • Maumivu wakati wa kujamiana

  • Kutokea kwa uvimbe sehemu moja karibu na tundu la uke

 

Dalili za uvimbe wa batholini iliyopata maambukizi

​

  • Uvimbe kuwa na maumivu ukishikwa/kuguswa

  • Kupata homa

  • Kutokwa na majimaji au usaha

​

Vihatarishi vya kupata vimbe hizi

​

  • Kutozingatia usafi wa maeneo ya siri

  • Kuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30

  • Kuwa kwenye kipindi cha kuona hedhi

 

Visababishi

 

Kisababishi kikuu cha vimbe za tezi ya batholini ni kuziba kwa mrija w akupitisha uteute unaozalishwa tezi hiyo. Kuziba huku kunaweza kusababishwa na maambukizi (maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa) katika mirija hiyo, uchafu au majeraha

 

Wakati gani wa kumwona daktari?

 

Mwone daktari endapo uvimbe hauponi ndnai ya siku tatu licha ya kujipatia matibabu ya nyumbani au endapo unaambatana na maumivu. Panga kuonana na daktari wako pia endapo umepatwa na uvimbe ambao haueleweki ukeni.

 

Matibabu

​

Kama hauna dalili yoyote ile, si lazima kupata matibabu ya hospitali. Endapo uvimbe una maumivu, unaweza kufanya matibabu mwenyewe kama vile kuloweka uvimbe kwenye maji ya uvuguvugu mara nyingi uwezavyo kwa siku(fanya mara tatu au nne kwa siku) na kunywa dawa za maumivu.

​

​

Unalowekaje uvimbe huu na kwenye nini?

​

Endapo unataka kuloweka uvimbe huu andaa maji yako ya uvuguvugu kwenye beseni, kisha kalia kiasi kwamba uvimbe uzame kwenye maji kwa muda wa dakika 10 hadi 15. Unawezaa kuweka pia deto kwa matokeo mazuri zaidi.

​

Mambo hutakiwi kufanya

​

Acha kushiriki kujamiana wakati uvimbe wako unaendele kupona

​

​

Kumbuka. Uvimbe ukipata maambukizi unaweza kupasuka na kuanza kutoa usaha, mategemeo ni upone ndani ya siku tatu hadi nne. Endapo uvimbe haujapona ndani ya siku hizo onana na daktari wako kufanyiwa upasuaji mdogo wa kutoa usaha wote.

​

Kama matibabu haya hayatafanya kazi, utatakiwa kaupata matibau kutoka kwa daktari wako kwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo. Upasuaji mara nyingi huwa ni mdogo na utafanyika nawe utaruhusiwa nyumbani isku hiyi hiyo.

 

Kinga

​

Mara nyingi hakuna njia ya kujikinga kupata vimbe hizi, hata hivyo zingatia kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu na uwe na tabia ya kufanya usafi maeneo haya ya siri.

​

​

Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

​

Rejea za mada hii,

​

  1. Bartholin gland cyst. Family doctor. https://familydoctor.org/condition/bartholins-gland-cyst/. Imechukuliwa 03.07.2020

  2. Smith RP. Bartholin gland: Cysts. In: Netter's Obstetrics and Gynecology. 3rd ed. Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 03.07.2020

  3. Chen KT. Bartholin glad cyst and abscess: Word catheter placement. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 03.07.2020

  4. NHS. https://www.nhs.uk/conditions/bartholins-cyst/. Imechukuliwa 03.07.2020

  5. MIchigan Medicine. Bartholin Gland cyst. https://www.uofmhealth.org/health-library/tw2685. Imechukuliwa 03.07.2020

bottom of page