Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt . Benjamin L, MD
16 Oktoba 2024, 10:17:38
Sindano ya uzazi wa mpango
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
Tarehe mwezi na mwaka na saa
ULY clinic inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia mawasiliano yetu.
Rejea za mada hii:
Depo provera. https://my.clevelandclinic.org/health/drugs/4086-depo-provera-birth-control-shot. Imechukuliwa 16.10.2024
Hatcher RA, et al., eds. Injectable contraceptives In: Contraceptive Technology. 21st ed. Ayer Company Publishers; 2018.
Kaunitz AM. Depot medroxyprogesterone acetate (DMPA) for contraception: Formulations, patient selection and drug administration. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16.10.2024
Kennedy CE, et al. Self-administration of injectable contraception: A systematic review and meta-analysis. BMJ Global Health. 2019; doi:10.1136/bmjgh-2018-001350.
Hatcher RA, et al. Progestin-only contraceptives. In: Managing Contraception 2019-2020: For your pocket. 15th ed. Bridging the Gap Foundation; 2020.
Hapgood JP, et al. Hormonal contraception and HIV-1 acquisition: Biological mechanisms. Endocrine Reviews. 2018; doi:10.1210/er.2017-00103.
Kaunitz AM. Depot medroxyprogesterone acetate for contraception: Efficacy, side effects, metabolic impact, and benefits. https://www.uptodate.com/contents/search. Accessed Oct. 13, 2019.
Long VE, et al., eds. Injectable contraceptives overview. In: Telephone Triage for Obstetrics & Gynecology. 3rd ed. Wolters Kluwer Health; 2019. http://ovidsp.ovid.com. Accessed Oct. 14, 2019.
Lopez LM, et al. Progestin-only contraceptives: Effects on weight. The Cochrane Database of Systematic Reviews. 2016; doi:10.1002/14651858.CD008815.
Lerma K, et al. Injectable contraception: Emerging evidence on subcutaneous self-administration. Current Opinion in Obstetrics & Gynecology. 2019; doi:10.1097/GCO.0000000000000574.
Medroxyprogesterone acetate: Uses, Interactions DrugBank.https://go.drugbank.com/drugs/DB00603. Imechukuliwa 16.10.2024
Sindano ya uzazi wa mpango huwa na kemikali aina ya medroxyprogesterone acetate ambayo hufanya kazi kama homoni progesterone kuzuia ujauzito.
Je sindano ya uzazi wa mpango huzuiaje ujauzito?
Sindano ya depo huzuia ujauzito kwa kudumaza uzalishaji wa mayai katika ovari pamoja na kufanya ute unaozalishwa kuwa mzito kutoruhusu manii kupenya na kuingia katika kizazi.
Je sindano ya uzazi wa mpango huzuiaje magonjwa ya zinaa?
Ingawa sindano ya uzazi wa mpango huzuia kupata ujauzito, kemikali hii haizuii kupata magonjwa ya zinaa hivyo utapaswa kutumia njia zingine za kujikinga na magonjwa ya zinaa.
Je, sindano ya uzazi wa mpango hutumikaje?
Sindano ya kwanza ya uzazi wa mpango hutolewa mara nyingi ndani ya siku 7 za kwanza mara unapoona damu ya hedhi. Hata hivyo inaweza kutolewa wakati mwingine pale ambapo wewe na mtoa huduma mnauhakika kwamba hauna ujauzito. Utapimwa kipimo cha ujauzito kwanza kabla ya kuchomwa sindano hii.
Baada ya kuchomwa sindano ya uzazi wa mpango, hakuna hatua zai ziada utakazopaswa kuchukua kuzuia ujauzito.
Utahitaji kuchoma sindano inayofuata kila baada ya miezi mitatu na unashauriwa usichelewe zaidi ya wiki mbili tangu kukamilika kwa miezi mitatu la sivyo unaweza kushika ujauzito.
Je sindano ya uzazi wa mpango huanza kufanya kazi baada ya muda gani?
Sindano ya depo huanza kufanya kazi mara moja baada ya kuchma kama ukichomwa wakati upo kwenye kipindi cha hedhi. Kama ikitoewa muda mwingine tofauti na huu katika mzunguko wako wa hedhi, utahitajika kusubiria kwa angalau siku 10 kabla ya kushiriki ngono bila kutumia kizuia ujauzito.
Je, mwanamke yeyote anaweza kutumia sindano ya uzazi wa mpango?
Hapana! Licha ya sindano hii kuweza kutumika kwa wanawake wengi, baadhi ya wanawake wenye hali na magonjwa yafuatayo hawashauriwi kutumia njia hii ya uzazi wa mpango kuepuka madhara. Wanawake hao ni wale wenye:
Kutokwa damu ukeni bila sababu
Ugonjwa wa ini
Saratani ya matiti
Lupasi
Kiharusi
Magonjwa ya moyo
Maudhi ya sindano ya uzazi wa mpango
Mwanamke anayetumia sindano ya uzazi wa mpango anaweza kupata miongoni mwa maudhi yafuatayo ambayo hutokea sana.
Kubadilika kwa mzunguko wa hedhi, unaweza kuwa mfupi au mrefu
Maumivu ya kichwa
Hofu
Huzuniko
Chunusi
Kubadilika kwa hamu ya kula
Kuongezeka uzito
Kuongezeka kwa vinyweleo vya mwili haswa uoni na kiwiliwili
Kukatika kwa nywele za kichwani
Ugonjwa wa udhoofu wa mifupa( osteoporosis)
Tafiti zinaonyesha kuwa, baada ya kutumia kwa mwaka mzima, asilimia 50 ya wanawake (yaani wanawake 50 kati ya 100) huacha kuona damu ya mwezi. Mwanamke anapaswa kupata period kila mwezi ili kuwa na afya njema na hurejea baada ya kuacha kutumia sindano.
Utachukua muda gani kupata mimba baada ya kuacha kutumia sindano ya uzazi wa mpango?
Kupata ujauzito ni suala linalotegemeana na mwitikio wa mwili wako kwenye kemikali ya sindano ya uzazi wa mpango (depo-provera). Tafiti zinaonyesha utaweza kupata ujauzito katika kipindi cha wiki 12(mezi 3) hadi 14 baada ya kuacha kutumia sindano ya uzazi wa mpango. Hata hivyo wanawake wengine wanaweza kupata mimba baada ya mwaka 1 hadi 2 kupita tangu kuacha kutumia sindano ya uzazi wa mpango.
Majina mengine ya sindano ya uzazi wa mpango
Sindano ya uzazi wa mpango hufahamika pia kwa majine mengine kama
Sindano ya depo
Sindano ya depo-provera
Sindano ya Medroxyprogesterone acetate
Uzazi wa mpango kwa sindano
Dawa ya kuchoma ya uzazi wa mpango