Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Salome Adolf
Jumatatu, 2 Desemba 2024
Aina ya vipele vya UKIMWI
Utangulizi
Watu wengi waishio na VVU hupata vipele katika kipindi flani cha maisha ambavyo vimegwanyika katika mkundi kadhaa kwa kuzingatia kisababishi. Visababishi vya vipele ka wagonjwa wa VVU huwa pamoja na maambukizi ya kirusi cha UKIMWI, magonjwa nyemelezi, saratani zinazoambatana na UKIMWI na maudhi ya dawa za VVU.
Makundi ya aina ya vipele vya UKIMWI
Kuna aina nne za vipele vya UKIMWI kwenye makundi kulingana na visababishi, makundi hayo ni;
Vipele vinavyotokana na maambukizi ya VVU
Vipele hivi hutokea katika kipindi cha awali cha maambukizi pia huambatana na dalili nyingine kama vile mafua, homa, uchovu wa mwili nk, viepele hivyo huwa kama ifuatavyo;
VIpele vya kukauka ngozi
Mlipuko wa vipele vidogo vinavyowsha
Kuvimba kwa mashina ya nywele kutokana na chembe za esinofili
Vipele vinavyotokana na magonjwa nyemelezi
UKIMWI hushusha kinga ya mwili na kuongeza hatari ya mtu kupata magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi yanayosabahisha vipele kwa watu waishio na VVU ni kama ifuatavyo;
Vipele vya kirusi herpes simplex (HSV)
Vipele vya kirusi varicella zoster (VZV)
Vipele vya kirusi pox (molluscum contagiosum)
Vipele vya kirusi human papiloma (HPV)
Vipele vya TB
Vipele vya kaswende
Bacillary angiomatosis
Disseminated histoplasmosis
Disseminated cryptococcosis
Vipele vinavyotokana na saratani zinazoamabata na UKIMWI
Vipele hivi husababishwa na saratani zifuatazo;
Vipele vya kaposis sakoma
Vipele vya lymphoma
Vipele vya melanoma
Vipele vinavyotokana na maudhi ya dawa za UKIMWI
Baadhi ya dawa za UKIMWI husababisha mzio unaoleta vipele, mara nyingi hutokea siku kadhaa baada ya kuanza kutumia dawa na huisha ndani ya muda mfupi baada ya kuacha kutumia dawa hiyo. Aina hii ya vipele huambatana na dalili nyingine kama vile malengelenge, homa, maumivu ya misuli, mvurugiko wa tumbo nk.
Baadhi ya dawa za UKIMWI zinazosababisha vipele ni kama ifuatavyo;
Abacavir
Raltegravir
Dolutegravir
Nevirapine
Wapi utapata maelezo zaidi?
Kwa maelezo zaidi kuhusu vipele vya UKIMWI bofya hapa https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/vipele-vya-ukimwi kutazama vipele vya UKIMWI bofya hapahttps://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/picha-ya-vipele-vya-ukimwi
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
2 Desemba 2024, 18:26:34
Rejea za mada hii:
1. Comprehensive Review on HIV-Associated Dermatologic Manifestations: From Epidemiology to Clinical Management.National Institutes of Health (NIH) (.gov).https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC10368516/. Imechukuliwa 02.12.2024
2. HIV-related skin disease in the era of antiretroviral therapy: recognition and management. National Institutes of Health (t) (.gov). https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC6581453/. Imechukuliwa 02.12.2024
3.HIV Rash: Types, Related Symptoms, and Treatment.WebMD. https://www.webmd.com/hiv-aids/hiv-rash-causes-and-treatments. Imechukuliwa 02.12.2024
4. Cutaneous Manifestations of HIV. Medscape. https://emedicine.medscape.com/article/1133746-overview#a13. Imechukuliwa 02.12.2024