Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Jumamosi, 15 Julai 2023
Homa ya kuota meno kwa mtoto
Je, Kuota meno kunasaabisha homa kwa mtoto?
Kumbuka: Makala hii imeandikwa kwa kutumia tafiti moja iliyofanywa kwa watoto 46 wenye afya njema waliofuatiliwa katika kipindi cha siku 20 kabla ya kuota meno ya awali.
Mazoea ya zamani kuhusisha ugonjwa mkali na kuota meno yalikuwa makubwa kiasi cha mwaka 1842 kuota meno kulirekodiwa kama chanzo cha kifo kati ya Watoto waliokufa chini yam waka mmoja huko Landon. Ingawa kwa leo uhusianishwaji huo hauna mashiko kufikiriwa, swali bado limebakia Je, dalili ndogo kama homa inasababishwa na kuota kwa meno au la?
Â
Maandishi mengi yaliyowahi kuandikwa kutoa jibu la swali hili yameandikwa kutoa maoni pasipo kuwa na msingi wa utetezi katika tafiti.
Mpaka sasa hakuna ushahidi wa mwisho kutetea kuwa kuota meno kunaweza kusababisha dalili za muda za ugonjwa kwenye mifumo ya mwili ambapo miongoni mwa dalili kuu ni kama homa kiasi, harara usoni na kuhara kiasi.
Hapo zamani ilikuwa kawaida kulaumu uotaji wa meno kusababisha homa ya baridi, kuharisha na homa.
Matokeo ya tafiti
Kati ya watoto 46, watoto 20 walikuwa na homa ya zaidi ya nyuzi joto za selishazi 37.5 katika siku hizi 20 za kufuatiliwa. Siku ya meno kuota, watoto 15 walikuwa na joto za zaidi ya nyuzi za selishazi 38. Uhusiano wa kuota meno na homa kitafiki ulikuwa mkubwa.
Taarifa za tafiti hii zinathibitisha kwamba, wazee walikuwa sahihi kwenye usemi wao kuota meno husabaisha homa. Hata hivyo kuna hatari kubwa ya kuweka kwenye fikra kwamba kuota meno ni chanzo pekee cha homa bila kufikiria na kuondoa sababu zingine zilizo magonjwa.
Â
Tafiti hii mwisho wake wa ufuatiliaji wa watoto hao ilikuwa pale meno yalipochomoza tu. Tafiti zinathibitisha kuwa watoto wengi huota meno kwenye umri wa miezi 6 hadi miaka 6, katika kipindi hiki inaweza kutokea mtoto ana ugonjwa mwingine ambao umetokea pamoja na kuota meno.
Â
Nini cha kufanya mtoto akiwa anahoma na anaota meno
Â
Jambo la msingi kufanya ni kumpeleka mtoto hospitali kwa uchunguzi na tiba. Hii itasaidia mtoto kufanyiwa vipimo vitakavyohakikisha kuwa hana kisababishi kingine cha homa mbali na kuota meno. Baada ya kuthibitisha, mtoto anaweza kutibiwa kwa dawa za kushusha homa nyumbani na kuhakikisha kuwa anapata mlo kamili.
Mada zingine
Unaweza kusoma zaidi kuhusu kuota meno katika makala zifuatazo
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Agosti 2024 18:17:32
Rejea za mada hii:
Jaber L, Cohen IJ, Mor A. Fever associated with teething. Arch Dis Child. 1992 Feb;67(2):233-4. doi: 10.1136/adc.67.2.233. PMID: 1543387; PMCID: PMC1793425.