top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

Jumanne, 4 Julai 2023

Kidonge cha calcium nyongeza

Kidonge cha calcium nyongeza

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeshauri wajawazito haswa wale wanaopata kiasi kidogo katika mlo kutumia vidonge vya calcium nyongeza miligramu 1500-2000 kwa siku ili kupunguza hatari ya shinikizo la juu la damu, shinikizo tangulizi la kifafa cha mimba na kifafa cha mimba yanayosababishwa na ujauzito.


Shinikizo tangulizi la kifafa cha mimba limeorodheshwa kusabaisha madhara ya kiafya kwa watoto wanaozaliwa ambapo linahusishwa na magonjwa yafuatayo;

  • Shinikizo la juu la damu utotoni (miaka 6-9)

  • Mtindio wa ubongo

  • Kiharusi cha ukubwani


Tafiti mbalilmbali zimefanyika kuangalia madhara ya matumizi ya vidonge vya calcium nyongeza kwa mtoto katika ukuaji mwili, umetaboli na ukuaji wa mfumo wa fahamu na kugundua mambo yafuatayo:


Madhara ya matumizi ya dozi kubwa ya vidonge vya calcium nyongeza wakati wa ujauzito kwenye ukuaji wa watoto bado hayajulikani kwa sababu ya taarifa za tafiti zinazokinzana na kukosa ushahidi wa kutosha.


Wakati matumizi ya vidonge hivi yanafanywa kuwa yakutumika kwenye kipindi chote cha ujauzito kwa wajawazito wote kwa sababu ya faida zake za kuzuia shinikizo la juu la damu na kujifungua kabla ya muda, utekelezaji wake hauwezi kukubalika kama kuna madhara yoyote kwa mzaliwa.


Taarifa zilizopo hata hivyo ni chache kuweza kutoa hitimisho kwamba matumizi vidonge vya calcium ya nyongeza husababisha matokeo chanya kwa vichanga na baada ya kipindi cha uchanga kupita na pia kutokuwa na madhara katika mwili haswa katika ukuaji wa mfumo wa fahamu na umetaboli.


Kwa nchi ambazo vidonge vya calcium nyongeza vinatakiwa kutumika kwa wajawazito, uchunguzi zaidi unapaswa ufanyike kwa wazaliwa wakiwa wachanga hadi ukubwani ili kugundua madhara ya muda mrefu.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

4 Julai 2023, 09:37:44

Rejea za mada hii:

1. Duley, L. 2009. The global impact of pre-eclampsia and eclampsia. Semin. Perinatol. 33: 130– 137.
View

2. WHO. 2013. Guideline: Calcium Supplementation in Pregnant Women. Geneva: WHO.

3. Hofmeyr, G.J, et al. 2018. Calcium supplementation during pregnancy for preventing hypertensive disorders and related problems. Cochrane Database Syst. Rev. 1: CD001059.

4. WHO. 2020. WHO Antenatal Care Recommendations for a Positive Pregnancy Experience: Nutritional Interventions Update: Vitamin D Supplements during Pregnancy. Geneva: WHO.

5. Goffin, S.M., et al. Groom, et al. 2018. Maternal pre-eclampsia and long-term offspring health: is there a shadow cast? Pregnancy Hypertens. 12: 11– 15.

6. Vatten, L.J., P.R. Romundstad, T.L. Holmen, et al. 2003. Intrauterine exposure to preeclampsia and adolescent blood pressure, body size, and age at menarche in female offspring. Obstet. Gynecol. 101: 529– 533.

7. Tenhola, S., E. Rahiala, P. Halonen, et al. 2006. Maternal preeclampsia predicts elevated blood pressure in 12-year-old children: evaluation by ambulatory blood pressure monitoring. Pediatr. Rev. 59: 320– 324.

Davis, E.F., et al. 2012. Cardiovascular risk factors in children and young adults born to preeclamptic pregnancies: a systematic review. Pediatrics 129: e1552– e1561.

9Ferreira, I., et al. Stehouwer. 2009. Preeclampsia and increased blood pressure in the offspring: meta-analysis and critical review of the evidence. J. Hypertens. 27: 1955– 1959.

bottom of page