top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

ULY CLINIC

Jumanne, 1 Agosti 2023

Klamidiasisi huonekana baada ya muda gani?

Klamidiasisi huonekana baada ya muda gani?

Klamidiasisi ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria Chlamydia trachomatis, ambaye huambukiwa kwa kufanya ngono ya uke, ume au njia ya haja kubwa na mtu mwenye maambukizi. Kwa nyongeza mama anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa kujifungua. Ugonjwa huu wazinaa huripotiwa mara kwa mara kwa wagonjwa wa magonjwa ya zinaa.


Madhara ya klamidiasisi

Endapo klamidiasisi isipotibiwa husababisha PID, ugumba utokanao na kuharibika kwa mirija ya uzazi kwa mwanamke, kutungwa kwa ujauzito nje ya mfuko wa kizazi na maumivu sugu ndani ya via vya uzazi.


Dalili za klamidiasisi huonekana baad aya muda gani?

Ugonjwa wa klamidiasisi huonekana siku ya 7 hadi 28 tangu kushiriki ngono. Wanawake wengi na wanaume wachache huwa hawaonyeshi dalili zozote zile za maambukizi.


Dalilili za klamidiasisi

Wanawake

Dalili kwa wanawake huhusisha:

  • Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi

  • Kuungua wakati wa kukojoa

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Maumivu ya tumbo la chini ya kitovu na wakati mwingine homa na kichefuchefu


Wanaume

Dalili kwa wanaume hujumuisha

  • Kutokwa na ute mweupe kwenye uume

  • Hisia za kuungua wakati w akukojoa

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Kuvimba kwa korodani au kuwa na maumivu


Utambuzi

Diagnosis: Chlamydia is diagnosed by obtaining either a vaginal swab or urine for women, and a urine sample from men, and are sent to a lab for diagnosis.


Matibabu

Klamidiasisi hutibiwa kwa dawa za antibayotiki, matibabu yake huhusisha matibabu ya magonjwa yote ya zinaa yanayosababishwa kutokwa na ute usio kawaida kwenye maeneo ya siri. Mgonjwa hupaswa kutofanya ngono katika kipindi chote cha matibabu. Kipimo baada ya kumaliza dawa kinapaswa kufanyika miezi mitatu ili kuangalia kama dawa zimefanya kazi. Wataalamu wengi wanashauri wenza wapate dawa ili kuzuia mnyororo wa maambukizi kuendelea.


Kinga

Matumizi ya kondomu huzuia maambukizi haya. Hatua zingine za kudhibiti maambukizi ni kuacha ngono, kupima kabla ya ngono, kutumia njia za vizuizi zinazozuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa, na kupunguza idadi ya wapenzi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Agosti 2023, 20:34:48

Rejea za mada hii:

Lytle-Barnaby R. Sexually Transmitted Diseases: An Overview. Dela J Public Health. 2016 Apr 18;2(2):26-31. doi: 10.32481/djph.2016.04.009. PMID: 34466839; PMCID: PMC8389050.

2. ULY CLINIC dawa za kutibu Klamydiasis. https://www.ulyclinic.com/dawa-na-ugonjwa-unaotibiwa/dawa-ya-kutibu-maambukizi-ya-chlamydia. Imechukuliwa 01.08.2023

3. NCBI. Chlamydia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537286/. Imechukuliwa 01.08.2023

bottom of page