top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumatatu, 6 Septemba 2021

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline

HIV 1/2 SD BIOLINE 3.0 ni kipimo cha haraka chenye uwezo wa kutambua uwepo wa antibodi zilizozalishwa na mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maambukizi ya kirusi HIV1 au HIV2. Majibu ya kipimo ni sahihi kama yatasomwa ndani ya dakika 10 hadi 20, majibu baada ya muda huu si ya kuaminika.


Kipimo cha HIV SD bioline


Swali


Ukipima VVU kwa kwa kipimio cha HIV SD bioline na kikachora mstari mmoja kwenye C kisha baada ya masaa matatu ikachora mistari wa pili yaani mstari kwenye alama C na 1 au 2 na baada ya hapo akatumia kipimo cha unigold ikasoma mstari mmoja zaidi ya mwaka ikawa hivyo je mtu huyo ni mgonjwa au?


Jibu ni Hapana

HIV 1/2 SD BIOLINE 3.0 ni kipimo cha haraka chenye uwezo wa kutambua uwepo wa antibodi IgG, IgM na IgA zilizozalishwa na mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maambukizi ya kirusi HIV1 au HIV2. Majibu ya kipimo yatakuwa sahihi kama yatasomwa ndani ya dakika 10 hadi 20 kabla ya kutupa kipimo hicho sehemu salama kama ulivyoshauriwa na daktari wako.


Namna kilivyotengenezwa


Kipimo cha SD BIOLINE HIV-1/2 kimewekewa utando wa antijeni za kirusi cha HIV1 (glaikoprotini gp 41 na protini 21) kwenye mstari namba 1 na antijeni za kirusi cha HIV2 (glaikoprotini 36)kwenye mstari namba 2. Sampuli ya damu inapowekwa huanza kutembea kutoka kwenye kitundu cha sampuli kwenda kwenye mstari namba moja, mbili na mwisho kwenye mtari wenye alama C. msta C hutumika kuangalia kama kipimo kinafanya kazi, mstari huu utaonekana mara utakapoweka sampuli ya damu au ukaweka kizimulio cha sampuli (maji ya kipimo)


Mistari yote mitatu inatakiwa isionekane kabla ya kuweka sampuli au maji ya kuzimulia sampuli.


Wakati gani wa kusoma majibu


Majibu yanapaswa kusomwa ndani ya dakika 10 hadi 20. Baada ya kuongeza kizimulio, soma majibu yako baada ya dakika 10 lakini si zaidi ya dakika 20.


Ufanye nini kama majibu hayaonekani vema baada ya dakika 10?


Kama majibu hayasomeki vema baada ya dakika kumi kwa sababu ya rangi nyekundu kutawala, soma upya baada ya dakika 10 lakini isiwe zaidi ya dakika 20 toka umeongeza kizimulio.


Je kwanini kipimo kinasoma mistari mitatu?


Ni kwa nadra sana kwa binadamu kupata maambukizi ya HIV1 na d HIV2 kwa pamoja. Kuonekana kwa mstari wa HIV1 na HIV2 mara nyingi humaanisha mwitikio wa kipimo kwenye protini zinazoelekea kufanana kati ya HIV1 na HIV 2. Ili kuthibitisha kwamba mtu ana virusi vya aina zote mbili, vipimo zaifi vya uthibitisho vinatakiwa fanyika.


Kama majibu yakisoma mistari miwili au zaidi ufanyenini kupata majibu ya mwsisho?


Mara nyingi kipimo cha SD bioline kinaposoma mistari miwili au zaidi ambapo kati ya mistari hiyo lazima Mstari C uwepo ina maanisha kuwa mtu huyu ana uwezekano wa kuwa na maambukizi ya VVU au magonjwa mengine kama kaswende, lupus na ugonjwa wa lyme.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021, 04:44:51

Rejea za mada hii:

C. Chiu, et al. (2015): Possible results for the three-line SD Bioline HIV rapid diagnostic test (RDT) that presents indicator lines for control, HIV-2 and HIV-1.. PLOS ONE. Figure. https://doi.org/10.1371/journal.pone.0018294.g004. Imechukuliwa 06.09.2021

WHO. HIV RDTS. https://www.who.int/diagnostics_laboratory/evaluations/pq-list/hiv-rdts/170524_amended_final_pr_0027_012_00.pdf?ua=1. Imechukuliwa 06.09.2021

How HIV tests work. https://i-base.info/guides/testing/appendix-3-how-hiv-tests-work. Imechukuliwa 06.09.2021

WHO Prequalification of Diagnostics Programme PUBLIC REPORT Product: SD Bioline HIV Ag/Ab Combo Number: PQDx 0069-012-00. https://www.who.int/diagnostics_laboratory/evaluations/130322_0069_012_00_public_report_final_v1.pdf. Imechukuliwa 06.09.2021

Leslie Shanks, et al. Dilution testing using rapid diagnostic tests in a HIV diagnostic algorithm: a novel alternative for confirmation testing in resource limited settings. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4432962/. Imechukuliwa 06.09.2021

Tania Crucitti, et al. Performance of a Rapid and Simple HIV Testing Algorithm in a Multicenter Phase III Microbicide Clinical Trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3165239/. Imechukuliwa 06.09.2021

Test Accuracy of HIV SD bioline strips. https://www.verywellhealth.com/hiv-diagnosis-3132731. Imechukuliwa 06.09.2021

Avoiding false positives: rapid HIV tests vary in their accuracy, so need to be used in combination. https://www.aidsmap.com/news/may-2017/avoiding-false-positives-rapid-hiv-tests-vary-their-accuracy-so-need-be-used. Imechukuliwa 06.09.2021

bottom of page