Mwandishi:
Dkt. Lugonda B, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Jumatano, 19 Julai 2023
Muda wa kusubiri ngono baada ya kutoa mimba
Moja ya swali linaloulizwa sana baada ya kutoa mimba ni muda sahihi wa kufanya ngono baada ya kutoa mimba. Makala hii imeeleza jibu hilo kwa kuzingatia taarifa za tafiti.
Hakuna makubaliano ya kitiba ya lini ni muda sahihi wa kujamiana baada ya kutoa mimba kwa njia yoyote ile. Muda wa kusubiri unalenga kuzuia maambuki yanayoweza kuingizwa kwenye kizazi wakati wa kujamiana kwa sababu shingo ya kizazi huwa wazi wakati huu. Baada ya kutoa mimba, daktari atakufanyia uchunguzi na kukushauri usubiri kwa wakati gani kabla ya kushiriki ngono.
Wakati hakuna makubaliano katika tiba ya lini utaanza kujamiana baada ya kutoa mimba, muda huo wa kurejea kwenye ngono unaweza kubadilika kutokana na njia iliyotumika kutoa mimba.Â
Muda wa kutofanya ngono baada ya kutoa mimba kwa dawa
Kama mimba imetoka kwa kutumia dawa, inashauriwa kusubiria kwa muda wa siku 4 hadi 7 kabla ya kuanza ngono ili kuzuia maambukizi kwenye kizazi. Muda huu wa kusubiria hutoa nafasi kwa kizazi kujisafisha na kujiweka sawa kabla ya tendo. Hata hivyo kusubiria kunaweza kuendelea kwa kipindi chote ambacho damu zitaendelea kutoka ambapo inaweza kuchukua wiki chache na mara nyingi huwa hazizidi wiki 2.
Muda wa kusubiria ngono baada ya kutoa mimba kwa upasuaji
Kama umetoa mimba kwa njia ya upasuaji, utakuwa na kipindi kifupi cha kutokwa damu hivyo unaweza kurejea wakati wowote kufanya ngono mara damu itakapokatika na kutokuwa na maumivu ya tumbo. Hata hivyo daktari atakushauri kusubiria kwa siku kadhaa kabla ya kuanza ngono ili kuzuia hatari ya maambukizi kwenye kizazi.
Jumuisho
Unaweza kuanza ngono wakati wowote baada ya kutoa mimba, kipindi kizuri cha kuanza kushiriki ni pale endapo damu nyingi imeacha kutoka ukeni. Kuanza kwa ngono kutegemee pia hali yako ya kiafya ikijumuisha afya ya mwili na akili. Utoaji mimba mara nyingi huambatana na maumivu ya tumbo, kutokwa damu na msongo wa mwili na kihisia, utapaswa kuusikiliza mwili wako na pale unapokuwa tayari unaweza kushiriki ngono kwa kutumia kinga ili kuepuka mimba nyingine isiyotarajiwa.
Â
Ngono ikoje baada ya kutoa mimba?
Mara baada ya kutoa mimba unawez akupata uzoefu tofauti wa ngono ikitegemea mwanamke na mwanamke. Wanawake wachache hata hivyo huripoti mabadiliko hamu ya tendo la ngono baada ya kutoa mimba na hii ni kawaida na huchukua muda mfupi.
 Â
Mambo unayopaswa kufahamu baada ya kutoa mimba
Wakati wa tendo la kwanza baada ya kutoa mimba unapaswa kutumia kondomu
Unaweza kutumia kizuizi (dayaframu) kama njia ya kuzuia mimba katika tendo la kwanza baada ya kutoa mimba. Matumizi yanatakiwa kuzuia kwa muda wa wiki sita kama mimba iliyotolewa ilikuwa na zaidi ya wiki 14
Njia ya dharura ya uzazi wa mpango au kipandikizi cha ndani ya uzazi zinaweza kutumika ndani ya siku 5 baada ya kutoa mimba kama utashiriki ngono bila kutumia kinga ili kupunguza hatari ya ujauzito mwingine.
Kumwaga nje manii kunaweza kutumika kama njia ya uzazi wa mpango kwenye tendo la kwanza la ngono baada ya kutoa mimba
Kipandikizi ndani ya uzazi hakipaswi kuwekwa mapema baada ya kutoka kwa mimba kutokana na maambukizi
Njia za uzazi wa mpango za homoni kama vile( kipandikizi, sindano, na ringi inaweza kutumika mara baad aya kutoa mimba)
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Agosti 2024, 18:42:39
Rejea za mada hii:
1. Clinical Practice Handbook for Safe Abortion. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK190099/. Imechukuliwa 18.07.2023
2, Morotti M, et al. Changes in sexual function after medical or surgical termination of pregnancy. J Sex Med. 2014 Jun;11(6):1495-504. doi: 10.1111/jsm.12506. Epub 2014 Mar 18. PMID: 24636172.
3. Bianchi-Demicheli F, e tal. Termination of pregnancy and women's sexuality. Gynecol Obstet Invest. 2002;53(1):48-53. doi: 10.1159/000049411. PMID: 11803229.
Induced abortion and psychosexuality. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK68089/. Imechukuliwa 18.07.2023
4. Fok WY, et al. Sexual dysfunction after a first trimester induced abortion in a Chinese population. Eur J Obstet Gynecol Reprod Biol. 2006 Jun 1;126(2):255-8. doi: 10.1016/j.ejogrb.2005.10.031. Epub 2005 Dec 7. PMID: 16337729.