Kutokwa na ute mweupe kwenye uume au uke unaoambatana na maumivu wakati wa kukojoa au hedhi katikati ya vipindi ni miongoni mwa dalili zinazoonekana siku ya 7 hadi 28 tangu kushiriki ngono zembe.
Gono inayosababishwa na Neisseria gonorrhea dalili zake huonekana siku ya 2 hadi 21 tangu kushiriki ngono hata hivyo wanawake huchelewa kuonyesha dalili za awali na hupata athari zinazotokana na maambukizi.
Mwongozo wa Tanzania na nchi zingine huhusisha matibabu ya magonjwa kadhaa yanayosababisha kutokwa usaha sehemu za siri, vipimo zaidi vya kutambua kisababishi na dawa yake hufanyika kama mgonjwa hatopona kwa dozi ya awali.
Dawa za PEP zinazotumika huwa na mchanganyiko wa dawa ambao ni tenofovir na emtricitabine na raltegravir au na dolutegravir au na darunavir na ritonavir.